Nifanyeje baba yangu mzazi ajue kwamba mimi ni mwanae?

Nifanyeje baba yangu mzazi ajue kwamba mimi ni mwanae?

Lakini kwa nini uumie? Kwani yeye kwenda kumtafuta baba yake mzazi ni kosa? Kwani akienda kumtafuta baba yake mzazi katika umri wake wa utu uzima itapunguza upendo wake kwako au heshima yake kwako?

Na wakati mnaanza maisha na mama yake hukuliweka kichwani jambo la uwezekano wa yeye siku moja labda kutaka pia kujua upande wa baba yake?

Ni nini hasa kitakachokufanya uumie kiasi hicho?

Elewa tu kwamba nitaumia. Basi!
 
There are currently 2115 users browsing this thread. (43 members and 2049 guests)

Naona wahishimiwa na kaya zao matumbo moto, chech uzi ulivyosheheni guests, kama wa unga.
mm najiuliza hawa guest wanatafuta nini??
basi wajiunge waniulize maswali kuliko kukaa pembeni wakisubiri majibu ambayo hawatayapata
 
kama mama yako bado hajakueleza, sasa hayo unayoyahisi yanatoka wapi? Anayejua uhalali wa mtoto ni mama yako sasa wewe unasikiliza ya barabarani au unataka kujipendekeza kwa kuwa huyo baba ni waziri? ridhika na huyo aliyekulea na kukusomesha, usimuumize huyo mzee kwa kumueleza kuwa siyo baba yako baada ya tabu yote aliyoipata sababu ya wewe.
 
Uko sahihi kabisa. Ndio maana wewe ni Nyani Ngabu, na mimi ni Masaki, watu wawili tofauti kabisa. Binafsi ningeumia sana, of course ningemsamehe, lakini upendo wangu kwake hautakuwa tena kama ulivyokuwa mwanzo.

wengine tupo kwenye situation kama hiyo na wala hatuhangaiki kutafuta sijui baba, baba gani asiyejua umuhimun wa wanae? alimzalisha mama watoto wawili hakugeuka nyuma, kwanini umjali asiekujali? nakumbuka kuna siku mama alituuliza hivi nyie hamnaga hamu ya kumfahamu baba yenu? aliambiwa tu kwamba na yeye angekuwa na hamu ya kutufahamu angetutafuta, tutamtafutaje mtu asie na shida/hamu na sisi?
 
Muulize kwanza bi mkubwa,wenzio tulishakumbwa na makubwa zaidi ya hayo,ila kiukweli hata kama kweli huyo waziri ni baba yako haitasaidia chochote,huyo aliekulea ndie mshua wa ukweli,hukukosa chochote kwake,onyesha na wewe upendo wako,its your time now,stand up and appreciate for what he has done for you.
 
Jambo moja nililo jifunza kupitia hii true story ya maisha yangu ni kwamba watu wengi sana wanaogopa kuambiwa ukweli. Lakini nina amini ukweli hata kama ni mchungu ni afadhali manake utakuweka huru.

unapolea mtoto (of which baba yangu mlezi alijua sio mwanae) lazima ujue kwamba ipo siku atataka tu kuwa huru tena sio kwa nia mbaya.

wengi wananishutumu na kuona kana kwamba nataka kumuumiza baba mzazi, ama natafuta malli ama status lkn hayo yote ningayataka ningeabza toka siku anagombea ubunge ama alipochaguliwa tu kuwa waziri kwann nije nimsake leo hii tayari isha kuwa saa kumi na mbili alfajiri??

sijui kwann watu wamenihukumu sana lkn wameshindwa kabisa kuelewa wapi ambapoa napita kwasasa. na leo hii mimi naona naweza kujinasua ila nawaone huruma sana wale ambao ni watoto (KIUMRI) ambao wanaangukia kwenye kundi kama langu kwa mtazamo wa harakaharaka tu watapata shida sana kwenye kujikomboa.

inaumiza lkn yote haya baba ndio chanzo pengine angenitafuta yy haya yasingalitokea. NIMEKUBALI KUWA VICTIM WA HALI YYTE ALIMRADI NITIMIZE HAJA YANGU.
 
mm najiuliza hawa guest wanatafuta nini??
basi wajiunge waniulize maswali kuliko kukaa pembeni wakisubiri majibu ambayo hawatayapata

hebu chukua ushauri wa kiranga! amenena vizuri sana, sijui watu mna roho nyepesi kiasi gani aise, mie nagota 31 dada yangu 34 tunaishilia kumwona baba kwenye picha zake na mama zamani walizopiga akipita Arusha kwenda monduli jeshini na hakuna alie na taimu nae, hajawahi kututafuta, hatujawahi kumtafuta maisha yanaenda poa kabisaaa!
 
Itakuwa vizuri kama ukiongea na mama yako juu ya hili yeye atakupa jibu la ukweli wala usiende hatua ya mwisho bila wazazi wako kujua na ikiwezekana wao ndo watakupa support kama wakiridhia na suala lako.
 
muulize kwanza bi mkubwa,wenzio tulishakumbwa na makubwa zaidi ya hayo,ila kiukweli hata kama kweli huyo waziri ni baba yako haitasaidia chochote,huyo aliekulea ndie mshua wa ukweli,hukukosa chochote kwake,onyesha na wewe upendo wako,its your time now,stand up and appreciate for what he has done for you.
yaani hakuna mtu nimpendaye kama baba mlezi manake ukweli ni miongoni mwa wanaume wachache sana wa ukweli wasiokuwa na ubaguzi wala choyo. Atabaki kuwa the true babu wa wanangu na ananidai heshima kubwa zaid ya hii nimpatiayo kwa sasa.
 
hebu chukua ushauri wa kiranga! Amenena vizuri sana, sijui watu mna roho nyepesi kiasi gani aise, mie nagota 31 dada yangu 34 tunaishilia kumwona baba kwenye picha zake na mama zamani walizopiga akipita arusha kwenda monduli jeshini na hakuna alie na taimu nae, hajawahi kututafuta, hatujawahi kumtafuta maisha yanaenda poa kabisaaa!
dah!! Sasa mimi hili shetan nimelitoa wapi?? B4 sikuwa hivi kabisa lkn kwa sasa naona nasukumwa kwa sana something is wrong
 
Jambo moja nililo jifunza kupitia hii true story ya maisha yangu ni kwamba watu wengi sana wanaogopa kuambiwa ukweli. Lakini nina amini ukweli hata kama ni mchungu ni afadhali manake utakuweka huru.

unapolea mtoto (of which baba yangu mlezi alijua sio mwanae) lazima ujue kwamba ipo siku atataka tu kuwa huru tena sio kwa nia mbaya.

wengi wananishutumu na kuona kana kwamba nataka kumuumiza baba mzazi, ama natafuta malli ama status lkn hayo yote ningayataka ningeabza toka siku anagombea ubunge ama alipochaguliwa tu kuwa waziri kwann nije nimsake leo hii tayari isha kuwa saa kumi na mbili alfajiri??

sijui kwann watu wamenihukumu sana lkn wameshindwa kabisa kuelewa wapi ambapoa napita kwasasa. na leo hii mimi naona naweza kujinasua ila nawaone huruma sana wale ambao ni watoto (KIUMRI) ambao wanaangukia kwenye kundi kama langu kwa mtazamo wa harakaharaka tu watapata shida sana kwenye kujikomboa.

inaumiza lkn yote haya baba ndio chanzo pengine angenitafuta yy haya yasingalitokea. NIMEKUBALI KUWA VICTIM WA HALI YYTE ALIMRADI NITIMIZE HAJA YANGU.

hivi unajikomboaje kwa mtu asiekujali/kukudhamini na wala hajui uwepo wako duniani hapa?
 
rafiki yangu EMT.....
nimekusoma saana na post yako ndeefuuu. Umejitahidi sana kumfanya gfsonwin aone anachotaka kukifanya ni haki yake na ni faraja kwake. well, ni mtazamo pia....
najua rafiki unajua kabisa gfs siyo mtoto wa kwanza kukataliwa na babake, wapo wengi sana, na sidhani kama kati ya hao woote waliokataliwa au ambao hawajui baba zao wameweza kukwepa kuoana, tena nina uhakika kuna watu wengi tu ambao wameoana mtu na dadake, sidhani kama hayo matatizo ya kiafya yanawakuta.
Na kuhusu gfs kuendelea kuumia kwa ajili ya wengine, mimi sidhani kama hili litamuumiza sana gfs kiasi cha kusema akadead au kuzimia..... yeye ni mtu mzima, kijana, ana nguvu, ni swala tu la kwenda kwa counsellor mara kadhaa na atapona. je ameshamfikiria mamake na babake ambao ni wazee sasa? je akienda kuwaambia anamtafuta baba waziri na babake mzazi akapata hear attack kwa ajili hiyo? unajua mzazi atawaza nini? kwamba labda sikuweza kumfanyia mambo anayotaka ndo maana anatafuta babake, au labda kuna kitu nimefanya ndo maana anatoka. unafikiri baba ataamini kuwa anataka ajue kuwa anaishi tu? hakuna jingine? sidhani kama baba atalikubali hilo.
All in all, afwate moyo wake. kama anaona amani ya moyo wake ni muhimu zaidi kuliko ya waliojitolea kwa ajili yake, fine..
sisi wote ni watu wazima na tunajua kabisa sadaka ni nini..... tena tunatoa sadaka kubwa sana kila siku sababu tu ya kuwakinga watu tunaowapenda na kuwajali sana. sidhani kama gfs atajisamehe akija kuona kwa sababu ya ubinafsi wa moyo wake tu, kawaumiza watu waliokuwa wamejitolea sadaka kubwa sana katika kuhakikisha amekuwa hivyo alivyo

Yes, ni haki yake na hakuna atakayemzuia kama akitaka kuonana na baba yake aliyemzaa. Atakachoamua hakuna mwenye haki ya kumzuia including mama yake. Hakuna mwenye haki ya kumtishia au kushutumu baba yake mzazi eti kwani alikuwa wapi wakati huo wote. Kama ni baba yake mzazi alikuwa anataka kuonana na mtoto wake labda hiyo argument ingekuwa na uzito kidogo. Lakini hapa is just an innocent daughter wants to meet her biological father. What is the problem?

Wanadamu tunatofautiana of course, na kama nilivyosema awali, kama ningekuwa ni mimi wala nisingeona shida. Kuna tatizo? If yes, hili tatizo linanisumbua kiasi cha kuathiri maisha yangu na shughuli zangu za kila siku? If yes, then I must address the problem ASAP kabla halijaniathiri zaidi.

Lakini wapo wengine wapo tayari kulea matatizo hata kuathiri maisha yao ya kila siku simply because hawataki kuwaumiza watu wengine. I totally respect that way of life.

Pia wapo watu ambao they don't really give a damn; I mean wale wa potelea mbali liwalo na liwe. I respect that way of life as well.

But when it comes to me silei matatizo. Kama nina tatizo na ninaona linaniathiri au linaweza kuniathiri maisha yangu ya sasa au hapo baadae, lazima nilitatue once and for all. Sitaki kuumiza kichwa kwa kuishi na matatizo yanayoweza kutatuliwa.

As human beings, we have different ways of either solving or living with our problems. Nyie mnamshauri aendelee kuishi na tatizo linaloonyesha ku-afftect hata maisha yake ya kawaida kwa faida ya wengine. Wengine wanamshauri kwa vile amesha identify tatizo, then the next step to find ways of how to address the problem. Pia wapo wanaohoji why should she even bother thinking of the problem anyway? Pia wapo ambao wametoa mpaka case studies zao which is good. Lakini pia matatizo yanatofautiana and should be addressed based on their particular facts.

Tunaweza kumshauri A, B, C na D lakini at the end of the day yeye ndiye akayeamua baada ya kupima faida na hasara zake za uamuzi wowote atakaochukua. Neither am I going to judge her on the decision she takes. It is entirely up to her. The best we can do is to make sure that she make an informed decision. That's all. We can't decided on her. We aren't judges. And, of course, we should respect her autonomy and feelings.
 
hivi unajikomboaje kwa mtu asiekujali/kukudhamini na wala hajui uwepo wako duniani hapa?

hivi kuwa na mazito nafsini ambayo huwez kuyasema kwa kuhofia watu unaona huo sio utuwa??
 
Mtoto hana kosa,yeye anatakiwa kujua biological parents wake,ni train inakuja kwa full force,haizuilikii meeen....kwavile upo na mama anatakiwa afanye hilo jukumu...ni lake kabisa...mtoto una jukumu la kumuuliza mama,ni jukumu la mama kutoa majibu sahihi....yeye pia akuelezee baba mlezi anajua nini about this,kama alimdanganya all along akuchane wazi,itafutwe solution ya kumuweka sawa.....ila kwa baba mlezi nayo ni another train,haizuiliki,mbaya sana kama kuna mahali alidanganywa,atakuja kujua tuuu one day ndio itakua issue......ni very complex....ila watu wawili ndio wanatakiwa wasolve hii maneno,mama na baba mzazi...wakutane,waongee kiutu uzima maana wanajuana hawa tangu wakiwa vijana,wenyewe ndio wanajua walikupataje pataje...huyu mtoto na baba mlezi ndio wanapata effect...kusolve hii maneno,mtoto muweke mama kati,mchane[hamna cha sijui mama ataumia sijui nini,ndio medicine hiyo],afunguke[kweli waziri ndio biological father?baba mlezi anajua au alidanganywa?etc,etc],na wewe mtoto funguka,set mipango na mama hapo...kamata waziri,weka kati,lipeni michano,akizengua shauri yake,ila kama umepindia zaidi unampandisha kwa pilato then atie akili asifanye mchezo na watoto anaowaleta duniani halafu anaamua kukimbia.....kuhusu baba mlezi wewe huwezi jua,mama ndio anajua wana deal gani mezani,huwenda alidanganywa all along,au anajua black and white.....nachojua hii maneno itakuja kuwa wazi na kila mtu atapata hukumu kadri ya makosa yake,aidha usifatilie au ufatilie,ni nature ina move,huwezi izuia,kama sio wewe utafatilia kwa uoga au nini,kuna kitu kitatokea na ukweli utajulikana tu,tunajikopesha muda tu.
 
hivi kuwa na mazito nafsini ambayo huwez kuyasema kwa kuhofia watu unaona huo sio utuwa??

mie kwanza sipendi kuishi kwa hofu, kama nina langu huwa nalibwaga hapo hapo, na wewe una uhuru huo pia na mpaka thread ilipofikia nadhani wewe fuata moyo wako unavyokuambia/unavyotaka, watu tupo tofauti sana my dear, si unaona kama nyamayao wala hakumbuki kama ana baba chini ya jua, lakini wewe lina kuumiza, kukosa raha/amani ya moyo ni kitu kibaya, fuata moyo wako, hapa ni mawazo/mchango tu ya watu mbali mbali mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe, nikuombe tu ukifanikisha utupepo ka " feedback"...Goodluck my dear.
 
gfsonwin Baba yako (waziri) lazima ajue kuwa wewe ni mwanae regardless reaction yake. cha msingi ongea kwanza na mama na baba yako kuhusu idea yako usije kuwaudhi kwa kufanya jambo hili behind their back. Hata kama asingekuwa waziri, still anahitaji kufahamu hili jambo. WAZIRI OR NOT, HE IS STIL YOUR FATHER.
 
Last edited by a moderator:

Twaib!
 
na mimi siend kwake kisa ni waziri nina kwenda kwake kwasababu ni baba yangu. manake jamani miaka yote hii yupo tu hivi huwa anassume kitu gani juu ya mtoto wake?? ama ndo hivyo ukizaliwa na baba na asipomwoa mama yako basi wewe unafutwa kwenye ramani yake??
 
hebu chukua ushauri wa kiranga! amenena vizuri sana, sijui watu mna roho nyepesi kiasi gani aise, mie nagota 31 dada yangu 34 tunaishilia kumwona baba kwenye picha zake na mama zamani walizopiga akipita Arusha kwenda monduli jeshini na hakuna alie na taimu nae, hajawahi kututafuta, hatujawahi kumtafuta maisha yanaenda poa kabisaaa!

Da Mkubwa Nyamayao nimefurahi kukuona. Case yako wewe ni tofauti na pengine na ya gfsonwin pia but zipo case nyingine ambazo kwa sababu tu ya mazingira baba mzazi anakuwa amedhulumiwa haki ya kumjua mwanae. Na akaishia tu kusikia kuwa kuna mwanao sehemu flani na ikahappen na huyo mtoto akajua uwepo wa babake huyo, je hastahili kumfahamu? Hata kama huyo baba hana uwezo wa kumtafuta?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom