rafiki yangu
EMT.....
nimekusoma saana na post yako ndeefuuu. Umejitahidi sana kumfanya
gfsonwin aone anachotaka kukifanya ni haki yake na ni faraja kwake. well, ni mtazamo pia....
najua rafiki unajua kabisa gfs siyo mtoto wa kwanza kukataliwa na babake, wapo wengi sana, na sidhani kama kati ya hao woote waliokataliwa au ambao hawajui baba zao wameweza kukwepa kuoana, tena nina uhakika kuna watu wengi tu ambao wameoana mtu na dadake, sidhani kama hayo matatizo ya kiafya yanawakuta.
Na kuhusu gfs kuendelea kuumia kwa ajili ya wengine, mimi sidhani kama hili litamuumiza sana gfs kiasi cha kusema akadead au kuzimia..... yeye ni mtu mzima, kijana, ana nguvu, ni swala tu la kwenda kwa counsellor mara kadhaa na atapona. je ameshamfikiria mamake na babake ambao ni wazee sasa? je akienda kuwaambia anamtafuta baba waziri na babake mzazi akapata hear attack kwa ajili hiyo? unajua mzazi atawaza nini? kwamba labda sikuweza kumfanyia mambo anayotaka ndo maana anatafuta babake, au labda kuna kitu nimefanya ndo maana anatoka. unafikiri baba ataamini kuwa anataka ajue kuwa anaishi tu? hakuna jingine? sidhani kama baba atalikubali hilo.
All in all, afwate moyo wake. kama anaona amani ya moyo wake ni muhimu zaidi kuliko ya waliojitolea kwa ajili yake, fine..
sisi wote ni watu wazima na tunajua kabisa sadaka ni nini..... tena tunatoa sadaka kubwa sana kila siku sababu tu ya kuwakinga watu tunaowapenda na kuwajali sana. sidhani kama gfs atajisamehe akija kuona kwa sababu ya ubinafsi wa moyo wake tu, kawaumiza watu waliokuwa wamejitolea sadaka kubwa sana katika kuhakikisha amekuwa hivyo alivyo