Nifanye nini niwe na furaha?

Nifanye nini niwe na furaha?

Smith Rowe

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2018
Posts
4,513
Reaction score
9,553
Habari wana jukwaa,

Moja kwa moja kwenye hoja. Kwa siku za karibuni naona nazidi kupoteza amani na furaha bila sababu. Na sina majukumu yoyote ya kutegemewa wala mawazo yoyote sijui tatizo nini.

Wajuvi wa mambo, naombeni ushauri wa kunitoa kwenye hii shida niwe na furaha na amani.

Nawasilisha.
 
Kwanza jipende.

Jikeep bize. Amka mapema, safisha chumba chako na kikipanga vizuri. Upende mwili wako. Jitengeneze unavyopenda. Vaa vizuri nguo safi, lala sehemu safi. Fanya kile moyo wako unapenda. Epuka kukaa bila shughuli yoyote na kuanza kutafakari visivyowezekana.

Laifu is guudo eeeee bi hapiiii
 
ooh nalilia raha
ooh nalilia raha
mbona siipati, mwenzenu mie
shida na, nashaka ndio yanipatayo duniani.

sijui bendi gani waliimba, sisi wazee wa bakulutu ni liwazo mujarabu
 
Id yako iko opposite na jinsi ulivo , maana kwa kabila letu Msangarufu ni mtu aliyechangamka, yaani mwenye furaha...

Ushauri wangu; Penda kufanya kitu unachokipenda mfano, kucheza mpira, kuangalia muvi, kuogelea, kuimba nk..na usipende kukaa peke ako muda mwingi, Jichanganye kitaa na wana...mi nakosaga furaha pale tu mama mwenye nyumba ananipigia nimlipe kodi yake...😀😀😀
 
Habari wana jukwaa,

Moja kwa moja kwenye hoja. Kwa siku za karibuni naona nazidi kupoteza amani na furaha bila sababu. Na sina majukumu yoyote ya kutegemewa wala mawazo yoyote sijui tatizo nini.

Wajuvi wa mambo, naombeni ushauri wa kunitoa kwenye hii shida niwe na furaha na amani.

Nawasilisha.
Kama una mpenzi jaribu kufanya naye tabia mbaya angalau mara tano kwa siku. Asubuhi, mchana jioni na usiku mara mbili kisha uone kama furaha yako mnara hautapanda!
 
Id yako iko opposite na jinsi ulivo , maana kwa kabila letu Msangarufu ni mtu aliyechangamka, yaani mwenye furaha...
Ushauri wangu; Penda kufanya kitu unachokipenda mfano, kucheza mpira, kuangalia muvi, kuogelea, kuimba nk..na usipende kukaa peke ako muda mwingi, Jichanganye kitaa na wana...mi nakosaga furaha pale tu mama mwenye nyumba ananipigia nimlipe kodi yake...😀😀😀
Nashukuru kwa kunifahamisha sikuwa najua maana ya hilo jina nilichukua tuu kwa rafiki yangu

Nashukuru kwa ushauri
 
Back
Top Bottom