Samwel Jr
JF-Expert Member
- May 9, 2020
- 1,362
- 960
Kwema wakuu, naombeni ushauri ili nipite kwa amani.
Mimi ni kijana wa miaka 25, nina familia na mtoto mmoja.
Mwaka huu mwezi wa 6 nilirudi, mzazi mwenzangu akaomba aende kwao, nikakubali. Nilipokuwa nyumbani nikaanza kutembelea marafiki. Rafiki yangu mmoja ambaye tunafanya kazi pamoja tukaamua kwenda kujipongeza. Vitu vilikwenda vizuri na hatimaye tukaenda nyumbani kwangu.
Tulipofika nyumbani tukaanza utani, hata tukampigia simu mzazi mwenzangu tukamdanganya kwamba nimekamatwa na nimepelekwa polisi. Alijibu kuwa kesho atakuja mapema. Baada ya hapo tukaanza story, tukaendelea kucheka mpaka tukalala.
Saa nane usiku nikasikia geti linagongwa. Nilipotoka nikakuta ni jirani yangu pamoja na mama mdogo na mume wake. Wakanuliza kuna shida gani kwa kuwa wamesikia nimekamatwa. Niliwaeleza ilivyokuwa na waliponiambia aliyesema hivyo ni rafiki yangu, nikacheka na kusema ilikuwa ni utani.
Siku kumi baadaye mzazi mwenzangu akarudi nyumbani, na ndipo matatizo yalianza. Alianza kununa kila mara. Nilipomuuliza alinieleza mambo mengi ambayo sikuyajua. Kitu kikubwa alichokisema ni kwamba:
"Nimeambiwa nilienda kunywa pombe kwa sababu nililazimishwa kuwa naye, kwamba simpendi ila najilazimisha."
Nilipomuuliza nani aliyemwambia hivyo, akasema ni yule jirani ambaye alikuja usiku, na jirani huyo kaambiwa na mama mdogo. Nilimwambia aachane na hayo kwa sababu ni kama kufukua makaburi.
Baada ya hapo akaanza kutaka kwenda kwa baba mdogo wake (anayekaa karibu), lakini nilikataa kwa sababu tayari aliwahi kukutana naye alipokuwa kwao. Usiku mzima akanuna, asubuhi nikatoka zangu. Ghafla akanitumia sms kuwa anataka aende kwao, hataki kukaa na mimi na nimwambie sehemu ya kuacha ufunguo. Nikamwambia akienda aache mtoto. Tukabishana, nikafunga mlango na geti nikatoka.
Baadaye mama mdogo akanipigia akisema nirudi tuongee, lakini nilichelewa kurudi. Niliporudi nikawakuta wanacheza. Mzazi mwenzangu akampigia simu baba mdogo wake akimwambia kuwa naogopa labda nitampiga. Baba mdogo akanitaka tuongee kwenye simu. Tuliongea vizuri, akanishauri nitulie. Lakini muda mfupi baadaye akampigia tena na kumwambia kuwa akikugusa tu, nitalipeleka polisi. Nilichukia sana.
Baadaye mzazi mwenzangu akaja kwangu, akalia na kuomba msamaha. Nikamsamehe ili mambo yaishe. Siku chache baadaye akaniomba tena aende kwa baba mdogo, nikampeleka mwenyewe na nikawaacha. Jioni akaniomba nimchukue, nikafanya hivyo.
Lakini siku moja nilichunguza sms zake na nikakuta ujumbe wa shangazi yake ukisema: "Tembea kidogo, kama haji nijulishe nikuitie toyo." Nikashangaa walikuwa wanazungumza nini kuhusu mimi, lakini nikapuuza.
Tangu amerudi kutoka kwao akaanza tabia za kutaka kila kitu akipate, kazi za nyumbani haziendi vizuri, chakula hakieleweki. Nikimwuliza analalamika kuwa namnyanyasa. Nilipuuza.
Kuna siku tulipanga kumwachisha mtoto kunyonya, lakini akasema ni mpaka mtoto awe na mwaka na nusu. Nilijiandaa kwa lishe ya mtoto, nikamnunulia unga na vingine. Lakini alipika uji wa ulezi akaweka mafuta ya alizeti. Nilipomuuliza akasema ni uji wa kawaida. Nikamwambia: "Huo siyo uji mzuri, umeweka mafuta ya alizeti, hamnazo kabisa." Akalia sana, akasema nimemdharau.
Siku nyingine akanitumia sms: "Naomba nauli niondoke, nimechoka haya maisha." Nikamjibu amuombe huyo anayemwendea. Akasisitiza nimpe nauli nimrudishe kwao. Aliposema nikiwa sina hela, akajibu: "Kama hutanipea nauli basi jiandae kwa yatakayoendelea humu ndani mpaka utanipa mwenyewe."
Nikamwambia nadhani na wewe umejiandaa. Akanijibu: "Ya kunywa pombe na kutunyima sehemu ya kulala." Kuna siku nililala kitandani katikati, akadai sitaki walale vizuri. Nilipuuza. Usiku nikawakuta wanacheka na mtoto, nikaingia chumbani. Kesho yake akaniambia ataondoka. Nikamwambia sina mafuta, tukaita toyo na akaondoka saa sita mchana kwenda kwa baba mdogo. Saa nane akanitumia sms: "Nitazoea tu haya maisha. Utaendelea kuharibu maisha ya wengine mpaka lini?"
Akanieleza pia anaenda kuanza maisha upya, na atambadilisha mtoto jina mpaka dini. Nikamwambia afanye hivyo kama anataka.
Kwa sasa muda wangu wa kurudi kazini umewadia. Ameondoka na ufunguo.
Naombeni mnishauri nifanye nini.
Poleni kwa gazeti hili refu, imebidi niandike yote ili mnielewe. Pia naomba msamaha kwa mwandiko wangu.