beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Bila shaka sura hii sio ngeni kwenye tasnia ya filamu na muziki nchini! Msanii huyu ni maarufu sana kwa watayarishaji wa videos za muziki wa Bongofleva nchini na hata wasanii husika. Ni mwanadada anayefanya poa pia upande wa filamu!
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa muziki na filamu; ni wazi utakuwa umeshamuona kwani ameshauza nyago kwenye videos za wasanii wakali kama vile Steve WW feat Diamond Platnumz (Nyota), Bamuyu 'Funga Mdomo' pamoja na 'Sungura' wake Madini.
Upande wa filamu, ameshashiriki kwenye kazi nyingi, ila kubwa ni hizi projects 4 zinazokaribia kutoka chini ya Gabo.
Naweza kusema msanii huyu 'Bado anajitafuta'. Kwani anamudu kufanya kazi hizi mbili kwa ufanisi mkubwa. Kwa sasa, anaandaa mradi maalum wa kubadilisha upepo wa tasnia mojawapo kati ya hizo ili awe Nembo ya kipekee hapa nchini atakayetuwakilisha kimataifa.
Namleta JamiiForums, mumpe maono yanayojenga. Kwa mwonekano wake na kupitia kazi hizo tajwa; ni upande upi anaweza kuleta mapinduzi?
Karibuni..