Nifanyaje huu uso niwe kama wengine

G M S

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
502
53
Madaktari humu ndani naomba ushauri maana nishaangaika nimefeli,, ngozi ya uso haijawahi kurelax huwa inakuwa kavu na rangi yenye mabaka nimeapply mafuta ya kila aina na ya bei tofauti kulingana na ushauri wa watu wa cosmetics sijawahi ona mafanikio zaidi ngozi yakumbwa na vipele kuonyesha imejaa mafuta,,, kutokana na roughness nimeapply pia hizi tube aina nyingi ila matokeo yanakuwa ya mda mfupi na kuongeza weupe,,, nimechoka je Nifanyaje kwa ushauri wenu?????
 
Kuna mafuta yapo hospital Hua yanachanganywa dawa,kama Kuna nesi au mfamasia unafahamiana nae muombe uwe unapaka ,ni mafuta ya mgando yatakusaidia ,PIA upime labda homoni zako hazijabalance
 
Kuna mafuta yapo hospital Hua yanachanganywa dawa,kama Kuna nesi au mfamasia unafahamiana nae muombe uwe unapaka ,ni mafuta ya mgando yatakusaidia ,PIA upime labda homoni zako hazijabalance
Thanks kwa ushauri
 
hizo cosmetics ndo zinakuharibu, tafuta sabuni ya zoazoa au dettol kisha paka mafuta ya nazi
 
acha kupaka mafuta. Kuanzia leo chukua banking powder ya maandazi yenye box la blue nadhani sio simba yenye jekundu. Sasa anza kupaka hiyo kitu unachanganya na maji kidogo ili iweze kupakika usoni . sungus sugua mpaka ikaike baada ya dakika tano ikikauka nawa namaji ya uvugu vugu. Basi, nunua mafuta ya watoto ya nazi yenye chupa ya blue
 
Acne free cream ndo suluhisho ya tatizo lako pia waweza tafuta sonaderm cream usitumie vipodozi vyenye mafuta mengi..tafuta lotion kavu kama perfect white lotion au yenye lemon
 
hayo machemical usikute ndio yanayozidisha, Halaf pia hujaeleweka ngozi yako ni ya mafuta au kavu, kwanza umesema ngozi kavu...halafu chini umesema imejaa mafuta, si kila unachoambiwa ndo ufanywe hasa hizo tube, labda vitu vya asili vinakuwa vingi havina madhara, kwa kifupi, mie nitakupa dawa za asili ambazo husaidia ngozi kuwa nyororo kwanza changanya Manjano na liwa (Msio) paka uson jisugue kama unatoa nongo na baadae paka halafu kaa nayo hata nusus saa hata lisaa kulingana na wewe unavyotaka au nafasi yako, halafu nawa uso wako paka mafuta unayotumia, ila kwa sasa paka lotion za kawaida ambazo sio kali.

Na pia unaweza changanya Asali, Mtindi na maji ya limao, jipake usoni kamaa muda wa dakika 15 halafu osha uso wako, au pia unaweza tumia mtindi na manjano pekee.
Jitahidi pia kunywa maji mengi, epuka kulala na mamake-up, na vipodozi vyenye machemical kwa sasa pumzisha fanya vitu vya asili. habba soda nayo ni nzuri kusugulia uso inakuwa kama ndo scrub yako, ila hakikisha ukisugua na habba soda, inabidi manjano na msio usijisugue paka tu na ikikauka osha. Na hata mapumba ya mahindi yale ukiyaroweka na maji halafu jipake usoni mpaka shingoni, yaache kidogo yakauke ila si sana halafu anza kujisugua ukimaliza kaoge, week tu au week 2 utaniambia jinsi sura itakavyokuwa nyororo.

Nadhani ukimaliza kupaka hivi vitu vya asili unaweza pia kutumia lotion au cream yoyote ya cocoa butter.

Wanawake wengi waki-comoro wanakuwa na ngozi lainiii nakupendeza sabab ya hii liwa kwao ni kama asili kwao.
 
Ni PM kuna sabuni moja inatokana na vitu vya asili nitakupatia bure,halafu utaleta mrejesho baadae!
 
Back
Top Bottom