Madhara ya kujichubua na kujiklimu kwa wanawake na adhari zake

strong star

Member
Jul 15, 2021
36
42
Wadada wengi wa bara la Afrika asili yao ni ngozi nyeusi yenye kungaaa sana almaaluf " chocolate colour " Lakini kutokanana maendeleo ya sayansi na teknolojia waafrika wengi hujikuta wakitamani rangi sawasawa na watu wa ulaya ,Hivyo ni kutafuta njia mbali mbali nao kuwa weupe, kwa mfano mkologo, sindano, vidonge nk.

Baada ya kuvamiwa na wimbi kubwa la matumizi ya vidonge na sindano kwa watu wengi hasa vijana kwa nia ya kujichubua na kujiklim , leo twende tuone madhara yake mwilini :-

Ngozi kuwa nyepesi
Vidonge hivi vinaenda kutoa ngozi nyeusi ambao ndio mlinzi mkuu wa ngozi za ndani ya mwili na kusababisha wepese na uraini wa ngozi, Na kufanya iwe rahisi kwa vijidudu na bacteria kuingia ndani ya mwili na kuleta magonjwa, Sio hivyo tu ata michubuko na vidonda juu ya ngozi kuchelewa kukauka na kupona kabisa.

Vipele, michirizi na vidonda
Moja ya matokeo ya matumizi ya vipodozi vya kujichubua ni kuepo kwa vidonda na vipele hasa kwa wale wanaotumia vitu kama mkorogo, Ikiwa katika sehem za uso na mahari pa wazi zaidi humfanya ata alietumia kujutia kutokanana mwonekano atakao kuwanao.

Sumu mwilini
Hivi vidonge na sindano ambazo ndio zimeshamili sana kwa sasa ni sumu kubwa sana na kuleta magonjwa mbalimbali baadae, kama vile kansa, na mengine ambayo yatafupisha maisha yako na majuto zaidi. Kuna mifano ya wazi ya matokeo ya kutumia vitu hivi.

Huondoa mafuta muhim katika ngozi
Matumizi ya aina yoyote ya vitu vya kujichubua (yaani mkorogo, vidonge ama sindano) huondoa mafuta muhim sana katika ngozi (cholesterol ) na kufanya ngozi kuwa kavu, ngum, na kuzeeka mapema kwani mafuta hayo muhim ndio ufanya kazi hizo muhim.

Ni ghalama
Matumizi ya vipodozi vya kujichubua huwa ni ghalama kuanzia katika pesa, muda, ata uhai na kukuletea magonjwa mengine kama Kansa na pia yale ya virusi na bacteria .Hivyo kumfanya mtumiaji kujilaum na kujutia kabisa kwa maisha yake yote .

Kukosa kujiamini,wasi wasi na mashaka
Ukishatumia vipodozi vya kujichubua au vidonge na sindano matokeo yake ni kuwa na wasi wasi kwa wanajamii wengine na kukufanya ushindwe kufanya shughuli zako kwa uhuru na amani kwani ukufanya uhisi wanakusema na kukujadili wewe tu ata ukipita.

Hayo ndio matokeo ya kujikilimu na kujichubua kwa vijana hasa wanawake na wanaume Siku hizi. Changamoto hii inakuwa sasa hasa katika bara letu la Afrika na inchi yetu ya Tanzania, Hivyo yatupasa kusimama kidete kulipiga vita .
 
Back
Top Bottom