Utofauti kati ya Toner, Serum na Moisturizer: Jinsi ya kutumia na namna zinavyofanya kazi

Feb 9, 2023
5
9
TONER
• Kazi kubwa ya Toner ni kubalance pH ya ngozi, kutoa uchafu wote uliobaki baada ya kuosha uso (kuosha uso pekee kwa maji na sabuni haimaanishi umetoa uchafu wote usoni), inazuia bacteria kwa kiasi fulani, inasaidia kufungua pores na kulainisha ngozi ya uso.

AINA ZA TONER
Tutazungumzia aina tatu za TONER

1. Hydrating Toner
• Hii ni aina ya Toner inasaidia sana kwa wale watu ambao uso hupauka baada ya kuuosha, uso ukakamaa, wale wenye ngozi kavu pia wenye sensitive skin

• Husaidia kuupa uso unyevu na kuruhusu products utakazotumia baada ya toner kufanya kazi kwa haraka na urahisi zaidi.

• Aina hii ya Toner unaweza kutumia kila siku (asubuhi na jioni)

2. Exfoliating Toner
• Hizi mara nyingi zinakua na active ingredients kama AHA & BHA
• Inasaidia kutoa ngozi iliyokufa (dead skin calls)
• Inasaidia kuzibua uchafu kwenye pores
• Zinawafaa sana watu wenye ngozi za mafuta,chunusi na vipele.

MATUMIZI: Mara 2 hadi 3 kwa week.

3. Treatment Toner
• Hizi ni zile toner ambazo zinakua na Active ingredients ya kutibu kitu fulani mfano makovu, fine lines & wrinkles, vipele etc
• Hizi zinafaa ngozi zote kutokana na shida yako

MATUMIZI: Inategemea na malekezo ya kwenye product

SERUM

• Serum ni muhimu katika skincare zote
• Inakuaga na ingredients zenye nguvu ambazo zinaenda kutibu tatizo fulani la ngozi mfano fine lines, makovu, uzee, hyperpigmentation etc.
• Serum ni nyepesi sana hivyo zinazama zaidi kwenye ngozi na kuleta matokeo ya haraka na mazuri ambayo huwezi kuyapata kwenye moisturizer
• Tumia serum inayoendana na shida yako ya ngozi pia na aina ya ngozi yako.

NB: Namna ya kuchagua serum inayoendana na ngozi yako:
• Unyevu - Hyaluronic acid
• Vipele & Oily - Niacinamide & salicylic
• Dead skin & Dullness - Vitamin C
• Uzee na makunyanzi - Retinol etc

MOISTURIZER
• Hii husaidia kuupa uso wako unyevunyevu
• Hulinda kupauka au kukakamaa kwa uso especially kwa wale wenye ngozi kavu au kama unatumia product za kuondoa chunusi au mafuta mengi usoni
• Unaweza kutumia kila siku asubuhi na jioni

Jinsi ya kuzitumia
Unaanza na Toner baada ya kusafisha uso wako kwa sabuni au face wash>>>Inafatia Serum>>> kisha Moisturizer

Kwa ushauri zaidi wa products zipi unaweza kutumia kutokana na shida,aina ya ngozi yako wasiliana nasi +255 769 081 492
 
Asante kwa somo,

Hii inawahusu hadi wanaume au ni wanawake tu?maana mwanaume kuwa na makopo manne au matatu unapaka hili unafunga,unahamia lingine unafunga,unahamia lingine tena
Face wash>toner>Serum >moisturiser ni ngumu

Wanaume tunataka kopo moja lenye mambo yote yaani ukitoka bafuni ni kopo moja unapaka habari imeisha.
 
Back
Top Bottom