lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,484
Utakubaliana na mimi kuwa Tanzania ilikua ina viwanda makini,na kama vingeendelezwa na kuwadhibiti viongozi wake waliokua wanaviendesha vibaya leo hii nchi yetu ingekua mbali kiuchumi na ingekua ni nchi ya viwanda? pengine ingekua kuikaribia south afrika?unakubaliana na mimi kuwa sera ya ubinafsishaji ilifanyika hovyo?
Kama ingefanyika vizuri leo hii tungekua hatukopi hata senti tano nje? sasa niambie viwanda vyetu viko wapi je unajua kuwa tulikua na kiwanda cha kutengeneza BISKELI zilizoitwa SWALA.Na hivi viko wapi? TAMCO kuunganisha SCANIA,General tyre kutengeneza magurudumu,Urafiki,Mwatex,Sungura tex,Mutex,Kilitex hivi vilitengeneza nguo,kiko wapi kiwanda cha kutengeneza majembe cha ubungo,Matsushita kilitengeneza radio,Tanganyika Parkers kilisindiks nyama za kopo,TIPER kilisafisha mafuta ghafi,Tz railways corporatiion na AIR TZ Corporatio hivi vilisaidia sana usafirishaji sio viwanda,Iko wapi Valmet.
Viko wapi wapi viwanda vyetu vya kutengeneza juice,tangold,liko wapi shirika la TZ Elimu suupplies,viko wapi viwanda vya sabuni za Gardenia,Lumi,Lux au hizi zilitoka nje?Unajua kiwanda cha chuma MANG'ULA,Viko wapi viwanda vya kuprocess pamba,tumbaku,chai,kahawa,katani na sukari?kiko wapi kwanda cha viatu Morogoro shoes na BORA,hivi ni vichache tu ndg zangu.
Je tangu zama hizo tusingekua tumeongeza vingine? Mwadui na Tancut almasi bado vyetu?nikumbusheni jamini bado vipo? na vingine vya siri na visivyo vya siri nimevisahau.tukumbushane tupate uchungu na nchi yetu.hii gesi haya madini tungeweza kuchimba wenyewe tu.unakikumbuka kiwanda cha mbolea Tanga TFC na kiwanda cha kutengeneza filamu ( sinema) TZ FILIM CORPORATION,hiki kisingewafaa akina Marehemu Kanumba,RAY,JB,na wengineo?Viwanda vingi China ni mali ya umma na sasa China ni world second largest economy.
Tukumbuke.
swali majibu yake yashajibiwa kitambo na yanaeleweka...watu washalalamika hadi vipara vikawatoka....so nikumizaa tu kichwa chake hyo mleta madaHapa hutapata wachangiaji.
Sikuhizi maswali haya hayana majibu.
kiwanda cha PHILIPS,Tanzania FOOD,kiwanda cha KIKO, NMCUtakubaliana na mimi kuwa Tanzania ilikua ina viwanda makini,na kama vingeendelezwa na kuwadhibiti viongozi wake waliokua wanaviendesha vibaya leo hii nchi yetu ingekua mbali kiuchumi na ingekua ni nchi ya viwanda? pengine ingekua kuikaribia south afrika?unakubaliana na mimi kuwa sera ya ubinafsishaji ilifanyika hovyo?
Kama ingefanyika vizuri leo hii tungekua hatukopi hata senti tano nje? sasa niambie viwanda vyetu viko wapi je unajua kuwa tulikua na kiwanda cha kutengeneza BISKELI zilizoitwa SWALA.Na hivi viko wapi? TAMCO kuunganisha SCANIA,General tyre kutengeneza magurudumu,Urafiki,Mwatex,Sungura tex,Mutex,Kilitex hivi vilitengeneza nguo,kiko wapi kiwanda cha kutengeneza majembe cha ubungo,Matsushita kilitengeneza radio,Tanganyika Parkers kilisindiks nyama za kopo,TIPER kilisafisha mafuta ghafi,Tz railways corporatiion na AIR TZ Corporatio hivi vilisaidia sana usafirishaji sio viwanda,Iko wapi Valmet.
Viko wapi wapi viwanda vyetu vya kutengeneza juice,tangold,liko wapi shirika la TZ Elimu suupplies,viko wapi viwanda vya sabuni za Gardenia,Lumi,Lux au hizi zilitoka nje?Unajua kiwanda cha chuma MANG'ULA,Viko wapi viwanda vya kuprocess pamba,tumbaku,chai,kahawa,katani na sukari?kiko wapi kwanda cha viatu Morogoro shoes na BORA,hivi ni vichache tu ndg zangu.
Je tangu zama hizo tusingekua tumeongeza vingine? Mwadui na Tancut almasi bado vyetu?nikumbusheni jamini bado vipo? na vingine vya siri na visivyo vya siri nimevisahau.tukumbushane tupate uchungu na nchi yetu.hii gesi haya madini tungeweza kuchimba wenyewe tu.unakikumbuka kiwanda cha mbolea Tanga TFC na kiwanda cha kutengeneza filamu ( sinema) TZ FILIM CORPORATION,hiki kisingewafaa akina Marehemu Kanumba,RAY,JB,na wengineo?Viwanda vingi China ni mali ya umma na sasa China ni world second largest economy.
Tukumbuke.
Ngorunde mimi nadhani hivi viwanda vilikuwa Tanzania na habari iliyopo ni kwamba vilichukuliwa na mafuriko. Wataalamu wanasema kuna uwezekani vimepotea kama ile ndege ya Malaysia na hata jana Lowassa alikuwa kwa TB Joshua kupata utabiri kama zitaonekana au la!!!!!Kama vile ulikuwa umefariki miaka ya themanini hivi...ukafufuka leo! Hiyo ndiyo Tz bwana..chezea ccm wewe!!
swali majibu yake yashajibiwa kitambo na yanaeleweka...watu washalalamika hadi vipara vikawatoka....so nikumizaa tu kichwa chake hyo mleta mada
Mie inaniuma sana mkapa alivyo iuza Nbc, hapo ndio alitenda unyama mwisho!
vyuo vya ufundi,watu wanasomea engineering watafanya kazi wapi mkuu,haya si ndo mambo ya Tunisia ,mtu anamaliza UNIVERSITY anajiajiri kuuza genge.Au tusubiri EA Watanazania wakafanye kazi katka viwanada vya Kenya halafu bidhaa zije ziuzwe Tanzania.achana na habari hiyo mkuuu utaumiza tu kichwa chako ....serikali yetu hiii wanaijuaaa wenyw
Ni kweli Madam lakini unaonaje suala la ajira kama hatuna viwanda? unasemaje kuhusu vijana wanaomaliza masomo ya ufundi na engineeringHapa hutapata wachangiaji.
Sikuhizi maswali haya hayana majibu.
Kama vile ulikuwa umefariki miaka ya themanini hivi...ukafufuka leo! Hiyo ndiyo Tz bwana..chezea ccm wewe!!
SPM kiwanda cha karatasi mgololo na sawala. walifosiwa kustaafu wakanyimwa mafao wanateseka sana[/QUO Nafarijika sana kuwa bado nchi hii ina watu wenye kumbukumbu kama wewe juu ya viwanda vyetu na maddhira waliofanyiwa wafanyakazi wazalendo.hata hivyo bado kuna watu watatamani mfumo ulioua viwanda uendelee kuwepo.
Mkuu umemaliza,lakini ajabu kuna watu wanataka mfumo ulioua viwanda,spirit ya kusoma masomo ya sayansi uendelee kutawala,tuna safari ndefu,hata hivyo darasa ulilotoa usiache kuwafumbua na wengine wataamka tu.TAZANIA, TAIFA LA WATU LEGELEGE.
watoto wenu mnawapeleka kusoma procurement,accountant, political science, administration, linguistic na ujinga mwingi, unategemea nini? hivi vitu wataviona ni chuma chakavu tu,, madarasa ya science siku hizo hayana watu, waumini wa bongo fleva na bongo movie wapo wengi,, tunategemea hata kesho tukifufua hivi viwanda ni nani atazalisha? tanzania kama nchi masikini inahitaji kuwekeza kwenye rasilimali watu, watu ambao moja kwa moja watakuwa na impact kwenye uchumi, na maanisha kuwa na namba ya kutosha ya matechnologist, vinginevyo mwendo huu wa watu kutaka kusomea manunuzi na uhasibu kuhesabu hela za wahindi hatuwezi kutoka kwenye tope hili...
ukiangalia sector nyingi ambazo zinatakiwa ziongozwe na watalaam husika zinapewa wapiga porojo, angalia mfano nishati na madini enzi zile na sasa ambapo yupo mtalaam husika.
kaka viwanda vilikufa Kwa sababu vilikosa usimamizi, kuajili kwa kujuana hata kama mtu si proffesional, siasa, upeo mdogo nk, kaka tanzania ina watalaamu wengi sana nje ya nchi ambao ni competent ila kujuana na kutokusaminiana ndio kunasababisha kutokubali kufanya kazi tanzania.
nchi zote zilizoendelea ziliwekeza kwenye vyuma (viwanda) zikawa na techologist wakutosha bandaye
walivyoendelea ndio ujinga mwingine ukafuata.
TANZANIA NCHI MASIKINI MILELE, MPAKA HAPO WANANCHI WATAKAPO AMKA NA KUJITOA KWA UZALENDO KUIPIGANIA NA KUFA KWA AJILI YA NCHI YAO.. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA WAZALENDO, AMSHA NA WALE WALIOLALA PEPO LA USINGIZI LIWATOKE. AMEN