Nifahamisheni viwanda hivi viko wapi?

Nifahamisheni viwanda hivi viko wapi?

soma historia ya ulaya na marekani, historia ya nchi zote zilizoendelea utaona kuna watu wengi saana walikufa kwenye production kwa niaba ya vizazi vyao vipya,,, je ni mtanzania gani ameshakufa kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii? (namaanisha kwenye production kwa ajili ya nchi) jibu utaona hakuna, Kwa hiyo utaona kuna stage tumeiruka ambayo bado inatutafuna,,,

INABIDI TUPATE KIONGOZI WA JAMI
HITTLER ATUTAWALE KAMA MIAKA 20 ILI TUFE SANA KWENYE KAZI, BAADA YA HAPO KIZAZI KIJACHO 2098 na kuendelea KITAKUWA SI KIZAZI CHA WATU LEGELEGE,DHAIFU NA WAZEMBE KAMA HIKI.

EEEEH MUNGU IBARIKI JAMII YA WATANZANIA WAZALENDO NA SHUPAVU. TUONDOLEE WANAFIKI, WABINAFSI,WEZI, WATU LEGELEGE, NA WALE WOOOTE WANAOJIPENDEKEZA NA KUSHABIKIA WANAUME WENZAO ILI WAO WALE..

mungu akubariki na wewe kwa kuyaona ambayo wengi wameshindwa kuyaona. watu wanasema hawapigi kura kwa chama au mtu asiotoa chochote,ubarikiwe sana mkuu.
 
kibaya kuliko yote ni kwamba Tanzania imekua soko la kununua vijibidhaa vidogovidogo kutoka nje vingine vilikuwa vinatengenezwa hapahapa na vingine tungeweza kutengeneza.tulichotakiwa kununua toka nje ni mitambo ambayo hatuna uwezo wa kutengeneza lakini sio viatu,nguo,viberiti ,toys n,k
 
Najisikia kulia ungekuta hata tatizo la ajira hakuna ,r,i.p.tanelec,kiko meerschaum,teco,
 
Ndugu,
Usitegemee kupata wachangiaji kwenye thread kama hii! watu wamejikita kwenye kugombania madaraka ili watawale yote hayo. Wauze gesi na madini kirahisi. Sijui katiba mpya inasemaje kuhusu mali za serikali na mfumo wa kuzibinafsisha. Viwanda vyote vimegeuzwa magodown au kubadilisha matumizi na kuweka Bar. Sasa viwanda vilivyobaki ni Sigara na Bia unategemea nini hapo? Mabenki ndio usiseme kuna ile tuliyoambiwa ni kubwa sana na mpaka leo nafikiria sipati jibu ukubwa wake ni upi?
La msingi ni kwamba tumetambua tulipojikwaa sasa ni wakati wa kuanza upya katika sekta zote tukijikita zaidi kwenye elimu. Wako wapi watanzania tunaeweza kujisifia ujuzi wao. madaktari mpaka leo tatizo dogo tu unatoa kiasi upelekwe india. Makandarasi ndio kabisa! ukiuliza mwananchi engineering (MECCO) ilipopotelea sijui kama kuna mwenye kumbukumbu! .......................

Ni kweli kabisa mkuu
 
kiwanda cha PHILIPS,Tanzania FOOD,kiwanda cha KIKO, NMC

Kiwanda cha ALPHI kilichotengeneza miswaki na dawa za bonamed sasa hivi ni kanisa kuuubwa!! Tunajisalia huko kwa raha zetu kiwanda cha pareto, majembe (arusha) vyote vimeishia kwenye matumbo ya ma bwana wakubwa wa ccm.
 
Ndugu zanguni tunahitaji mapinduzi ya kifikra. Tunajua mbaya wetu katika haya mambo..CCM..! Hiki chama kimetuongoza kwa kipindi cha miaka hamsini, matokeo yake ni hayo. Mimi sishabikii chama chochote cha siasa ila kwa CCM ambayo ndiyo imetufikisha hapa, sina budi ila kuichukia sana. Haionyeshi kukerwa wala kuwa na mbinu mbadala kukabiliana na hali hii. Na mbaya zaidi imewapa vijana elimu ya ajabu ambayo haiwaruhusu kuwaza namna ya kuiondoa madarakani kwa KURA. AJABU KABISA!!
 
waheshimiwa nakumbuka nikiwa mdogo miaka ya 80 hadi 90 kuna kiwanda cha kusindika ngozi, mashirika kama ya usafirishaji, kauma ,kauru, kaudo na mengine mengi kam sukita,n.k
 
Halo, inasikitisha sana, kila nikipita pale General tyre roho inauma sana nikisogea mbele nakutana na Fibre Board, nakumbuka ABB Tanelec, TEMDO, NMC (unga ltd),TFA,ACU,TPRI na vingine. Ndugu na jamaa zetu wengi zamani walikuwa wanafanya kazi humo, ajira zilikuwepo. Wakati tunaenda shule asubuhi tunaona mabasi makubwa yakikusanya wafanyakazi vituoni. Natamani enzi zile zijirudie bt haiwezekani tena. Loh?
 
Back
Top Bottom