Nielimisheni tafadhali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nielimisheni tafadhali

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by jobseeker, May 30, 2012.

 1. j

  jobseeker Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana JF,

  Huko nyuma niliwahi kuleta suali linalofanana na hili ninaloliuliza hapa ila hili ni kwa pembe nyengine.
  Naomba kuelimishwa ni vipi raia wa nchi nyengine anaomba kibali cha kufanya kazi tanzania? jee kuna
  masharti yeyote ambayo anahitaji kuyatimiza au rangi ya ngozi yake, briefcase na suti tu?

  I am serious, nataka kujua hasa maana hili linanisumbua mno!!!!
   
 2. v

  vitongoji New Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kufahamu hilo lazima ujipange vizuri, lakini taratibu za kisheria zipo kuhusu ajira. pia, inategemea aina ya kazi na mkataba ulivyowekwa kama ni kazi za mkataba.
   
 3. v

  vitongoji New Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hilo ni la kujua kwa wataalamu wa vibali. lisikusumbue hata kidogo.
   
 4. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hapana ndugu jibu lako ni WRONG kabisa. Yaani umeshindwa kumfahamu muulizaji, Kinachomsumbua mchangiaji ni kuwa watanzania tele wenye kisomo wako mitaani hawana kazi, lakini wazungu wanashuka kila siku na kupata nafasi kirahisi, kazi ambazo vijana wa kitanzania wanaweza kabisa kuzifanya.

  Pia mentality yako hiyo ya kuwa kila jambo lisikusumbue au lisitusumbue kwa kuwa tu kuna wataalamu au watu fulani wa majukumu hayo ndio yanayoturudisha nyuma Tanzania na kuwapa nafasi mafisadi kufanya watakayo, kwa maana hakuna wa kuwauliza.
   
 5. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye bold mkuu......... sio suali ni swali.
   
Loading...