Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 36,155
- 30,836
Ni wazi polepole alikua na nafasi nzuri mno ya kushauri anachosema sasa ambacho kwa wengi kinaonekana kama ni unafiki mtupu. Ni afadhalli angeshauri wakati akiwa na nafasi halafu ushauri wake ukataliwe kwa vielelezo angalau leo hii angelionekana mtu wa maana kiasi.
Hivi sasa,
historia ina muhukumu kwa fedheha tena mbele ya umma huku akiwa mafichoni pekeyake bila msaada. Maisha matamu ndani ya V8 yalimpumbaza na kuendekeza unafiki wa kuona kila kitu kiko sawa wakati akiwa na nafasi, hali ya kua hawa wanainchi anaojaribu kuwashawishi wamuelewe leo, walikua wakipiga mayowe kutwa kucha juu ya mambo mballimbali ambayo polepole aliona hayakua tatizo kwasasababu hakutaka kuwaudhi waliompatia nafasi ile.
Mateso ya kisaikolojia na upweke anayoyapitia polepole ni fundisho kwa wanafiki wengine wenye tabia za nidhamu za uoga kama huyo msukule. Huenda anaelekea kuchanganyikiwa akiwa huko huko mafichoni.
Kama taifa,
Twendeni kwenye uchaguzi mkuu wa kihistoria kwa amani, tukaamue mustakabali mwema wa Taifa letu Tanzania bila kuyumbishwa na waliopoteza uelekeo kisiasa kama polepole. Na hakuna haja hata kidogo ya kubabaika na msamaha wa shetani ambae anataka kubadili jina na kua ibilisi, huko ni kujidanganya kinafiki tu.
Mwalimu J.K.Nyerere aliwahi kusema, ukishazoe kula nyama ya mtu, kamwe huwezi kuache. Hamphrey Polepole hawezi kuacha nidhamu ya uoga, kujipendekeza kwa wakubwa anaowapenda na unafiki hata kama ataomba msamaha wa damu na moto 🐒
Mungu Ibariki Tanzania