NIDA: Tunaanza kutoa vitambulisho kwa watumishi wa Umma

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,467
513
Wanajamvi, hawa jamaa wanaboa, inawezekanaje waseme wataanza kutoa vitambulisho vya uraia kwa wafanyakazi wa serikali, au ndo watu kutaka waonekane wamefanya kazi, hivi anaehitaji kitambulisho hasa ni huyu mfanyakazi wa serikali mwenye kitambulisho cha kazi wengine na passport juu na kadi za benki zinazomtambulisha unawaacha wananchi ambao tunatakiwa tuwatambue. Tena ningefikiri wangeanza na mkoa kama kigoma ambako wageni ni wengi. Au ndo vichwa nazi?
 
Mkuu, nakumbuka wakati wanaanzisha agency hii walisema kuwa wataanza watumishi wa umma sababu database yao imekaa vizuri, ie wanalipa paye,etc. Am sure baada ya hapo wakwenda kwa awamu kwa watz wa makundi mengine. Tuwape muda na tuwavumilie sbb haya mambo mageni huku tanganyika ingawa wenzetu znz wana uzoefu nayo at least.
 
Mwanzo mbaya from the design stage, watu kupenda mteremko tu. Vitambulisho vilipaswa kuwafikia wakulima kwanza ili iwasaidie ktk utambulisho na access to finance na inputs. Sasa kama pilot inaanza na data base kamili then hakukuwa na haja ya international tendering
 
Mkuu wapi napata hii kitu exkyuuzi?wakulima na wafanyabiashara ndo wanatakiwa kuhudumiwa kwanza make wanashindwa hata kukopesheka,nachelea kusema siasa ya kupiga kura 2015 isije ikawa imehusishwa hapa
 
Kweli kabisa walitakiwa waanze na wakulima tena wananchi..sasa wafanyakazi wa wanini?

Hawako makini wanataka waenze na kitu rahisi halfu waseme pesa imeisha na mradi uishie hapo..
 
Mkuu, nakumbuka wakati wanaanzisha agency hii walisema kuwa wataanza watumishi wa umma sababu database yao imekaa vizuri, ie wanalipa paye,etc. Am sure baada ya hapo wakwenda kwa awamu kwa watz wa makundi mengine. Tuwape muda na tuwavumilie sbb haya mambo mageni huku tanganyika ingawa wenzetu znz wana uzoefu nayo at least.
Issue hapa naona ni kujifanya tu wameanza kazi, pilot study katika nyanja zote unatakiwa usample ili uweze kupata representative sample. Kuwapa watumishi wa umma unatoa kabisa maana ya National Identification kwasababu kimsingi hawa tunadata zao mpaka za ndani mno. ni kama wako identified tayari, wangeanza kuwatambua wakulima na wafanyabiashara walioko kwenye informal sector then ndo wangepata picha ya zoezi na ugumu wake, hapa labda uniambie watakuwa na kazi tu ya kuprint kwasababu hii database yao mbona iko tayari? sasa hapo mkuu si hata ile stationery yako wakikupa tenda na software unapiga hii kazi? we wape muda mi sikubaliani nao from the scrach, ingetosha kusema zoezi litaanza 2014.
 
Back
Top Bottom