NIDA imekosa mwelekeo kabisa

NIDA imekosa mwelekeo kabisa

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
14,138
Reaction score
33,524
Nimemsikia simba chawene kuanzisha vitambulisho vya NIDA chini ya miaka 18.

Yani kwa nilivyo safiri na kujifunza kwangu nchi za nje, Vitambulisho vya taifa vipo kwa ajili kisheria ukishatimiza umri wa kujitambua ndio unapatiwa.

Kingine zaidi mfumo wa nida umekuwa kama kitengo cha wasajili laini yani hakuna mamlaka kamili kati ya uhamiaji na nida.
 
CHANGAMOTO AMBAYO HUWA NAIONA KWA WAPINZANI

NI KUKOSA UELEWA WA MAMBO KWA KINA

WAZO LA SIMBACHAWENE NI WAZO BORA SANA

Ila ukishakuwa mpinzani unawekeza nguvu Latina kukosoa

N.B MAISHA YAKO NDO KILA KITU HAKIKISHA UNAKATAA MAANDAMANO
 
Mbona mtu mmoja kajibiwa na akaunt tatu tofauti. Moja ilifunguliwa mwaka 2014, zinapishan dakika tano tano kujibu. Login log out
 
Sasa boss mbona iko sawa kabisa kwamba kuwe na mfumo kanapozaliwa katoto punde kanaandikishwa kupata NIDA. Au pengine umetembea sana huko duniani na pengine umeanza kuamini kwamba kufanya kama wafanyavyo wao ni Bora zaidi?
Sometime lazima tujiepushe na mwigo wa kila kitu pale tunapoweza kufanya kwa utofauti
 
Mbona ni wazo zuri sana nchi zilizoendelea mtoto akizaliwa tu anapewa passport yake Sasa kama sisi bado hatujafika huko Kuna shida gani akipewa NIDA yake kabisa akifika miaka 18 anaenda ku update tu
 
Nimemsikia simba chawene kuanzisha vitambulisho vya NIDA chini ya miaka 18.

Yani kwa nilivyo safiri na kujifunza kwangu nchi za nje, Vitambulisho vya taifa vipo kwa ajili kisheria ukishatimiza umri wa kujitambua ndio unapatiwa.

Kingine zaidi mfumo wa nida umekuwa kama kitengo cha wasajili laini yani hakuna mamlaka kamili kati ya uhamiaji na nida.
Mchongo wa upigaji huo,hivyo vitambulisho vya nida kuna watu wazima wameomba toka april hadi leo havijatoka kwa madai bado avijaprintiwa halafu ghafla bin vuu waanze kutoa vya Watoto!
 
  • Thanks
Reactions: Fbn
Back
Top Bottom