Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 5,149
- 14,488
Nicolae Ceaușescu alikuwa kiongozi wa Kikomunisti kuanzia mwaka 1965 hadi 1989 huko Romania.
Awali alionekana shujaa kwa kujitenga kidogo na USSR, lakini baadaye akageuka dikteta hatari. Aliamua kulipa madeni yote ya nchi kwa kuuza chakula nje. Wananchi wakabaki na njaa, foleni za mkate na sukari zilikuwa kawaida.
Wakati wananchi wakiteseka, yeye na mkewe Elena walijijengea majumba ya kifahari, ikiwemo “Palace of the Parliament” – moja ya majengo makubwa zaidi duniani.
Polisi wa siri (Securitate) walitisha watu kila kona, hakuna aliyethubutu kukosoa serikali.
Lakini mambo yalibadilika mwishoni mwa 1989: Maandamano yalianzia Timișoara, yakasambaa nchi nzima. Alipojaribu kuhutubia watu tarehe 21 Desemba, umati ulimzomea live, kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa dikteta huyu. Jeshi na polisi wakamgeuka, akakamatwa tarehe 22 Desemba.
Siku ya Krismasi (25 Desemba 1989), yeye na mke wake walihukumiwa haraka na kupigwa risasi hadharani.
Ceaușescu anakumbukwa kama mfano wa jinsi dikteta anavyoweza kuanguka ghafla. Kutoka kuwa “mfalme” wa taifa, hadi kunyanyaswa na wananchi wake, yote kwa sababu ya njaa, hofu na anasa za kifamilia.