Nicholas Mgaya anamwongoza nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nicholas Mgaya anamwongoza nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shansila, Feb 2, 2012.

 1. S

  Shansila Senior Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilipigwa na butwaa nilipomsikia kiongozi huyu mkubwa wa TUCTA taifa akibeza mgomo wa madaktari,akidai kuwa si halali,pamoja na mambo mengine.Pamoja na kuwa haya ni mawazo yake binafsi na anao uhuru wa mawazo,na pengine yuko sahihi,kauli aliyoitoa ni kauli isiyotegemewa kutoka kwa kiongozi anayeongoza taasisi yenye malengo ya kudai haki za wafanyakazi.Hajui kuwa iwapo madai ya madaktari yatafanyiwa kazi, hata wafanyakazi anaowaongoza wanaweza kufaidika.Kauli yake ni kielelezo cha uongozi wake,ambapo shirikisho hili limebakia likiwanufaisha viongozi tu,huku maslahi ya wafanyakazi yakipuuzwa licha ya gharama za maisha kupanda sana!Ni kauli ya kuvunja moyo,na no sawa na mtu anapovamiwa na wezi nyumbani na kupiga yowe ambapo jirani anajitokeza lkn badala ya kukusaidia wewe,anawasaidia wezi !Sielewi huyu jamaa huwa anachaguliwa na nani,ila mimi namwona kama kikwazo cha mustakabali na ustawi wa wafanyakazi
   
 2. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,825
  Trophy Points: 280
  Naye huyu ni hopeless guy ambaye hajawahi kufanikisha lolote la wafanyakazi. We are paying quite dearly from our salaries to run these hopeless unions.
   
 3. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  amejua njia za vurugu na migomo sio utaratibu wa taifa letu
   
 4. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,792
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  mgaya anapigania kima cha chini angalau kifikie 350,000/ hawa madaktari wanataka milioni saba hataelewana. Na nafikiri wafanyakazi wa umma wengine haya madai ya madaktari yamekuwa too much. Kwa wale wanaokumbuka unafanana na ule mgomo wa walimu uilotaka kuongozwa na raisi wa sijui mashanga wakati wa mwinyi!
   
 5. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,792
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  mgaya anapigania kima cha chini angalau kifikie 350,000/ hawa madaktari wanataka milioni saba hataelewana. Na nafikiri wafanyakazi wa umma wengine haya madai ya madaktari yamekuwa too much. Kwa wale wanaokumbuka unafanana na ule mgomo wa walimu uliotaka kuongozwa na raisi wao sijui mashanga wakati wa mwinyi!
   
 6. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  Huyu Mgaya, aligeuka nyuma na kuanza kulamba viatu vya Mkuu wa magamba; mara tu baada ya hotuba ile ya mbayuwayu! Shame upon him!
   
 7. wizaga

  wizaga Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu ndugu, alishaisoma serikali yetu ukipiga kelele unachukuliwa na kuwekwa kula manono ya nchi .namuona ,anatamani sana mgomo huu angeongoza yeye, lakini alituacha nyuma pale alipomkaribisha mkuu wa kaya kwenye sherehe ya waalimu kule songea ,baada ya kusogeleana meza moja basi makali yote yallisha .tuna sema yeye akae kimya ataona kiwango kitakacho lipwa.HIvi mtu ukisema ma dr wamedai kiasi kikubwa je unajua pato la nchi ? do you think dr are stupid to the extend ,think uot the box,or open your library(brain) before mmmmmmmmmm
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama vipi wakamate kitabu wasomee udaktari!
   
 9. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli hawakufuata taratibu za kugoma ikiwa ni pamoja na kumpa mwajiri siku 60 kabla ya kugoma
   
 10. L

  Lugeye JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 1,073
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  utaratibu upi? acheni kutumiwa
   
 11. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  wafanya mchezo na CCm nini? unaweza kuta wamefadhiri ukarabati unaendelea pale makao makuu yao!
   
 12. S

  Shansila Senior Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nashangaa mtu unapozungumzia utaratibu kutofuatwa.Madaktari ni wwanataaluma wanaojua wajibu wao,haki zao na taratibu za kudai haki zao pindi zinapokiukwa.Naamini wameanzia mwanzo na walipoona hakuna matumaini,ndipo wakafika hapa walipofika.Tuache ushabiki wa kizamani kana kwamba cc tunaishi sayari nyingine.
   
Loading...