Swala la kuchangia elimu ndilo bora tatizo huu ni utamaduni ambao sisi wabongo bado hatuna. Elimu kwetu ni privilage for the few wakati wenzetu Wakenya its something they fight for. Tusubiri mikakati ya Shirikisho itakapo kamilika na no boarder labour migration itakapo sainiwa, raia wa jumuiya kufanya kazi popote bila vibali, tutashangaa mpaka secretarial jobs zitakavyozolewa na form four leavers wa Kenya.
Bado hatuna mwamko wa kuchangia elimu, hata ukiitisha harambee hiyo, utapata poor response. Ila lazima tufike mahali tuanze.
Kuchangia sherehe kuna aina nyingi, kuna wanaochangia kwa sababu ni wahusika wa karibu na michango yao ni ya mandatory kama sehemu ya obligation kwa muhusika.
Kuna wanaochangia kwa ajili ya social participation na interaction, yaani unachanga tuu ili ustahili kupata kadi ya mwaliko. Maranyingi hawa huchanga ile minimum required donation lazima aje tena ale na anywe kuliko hata kale kamchango kake. Ndio hawa wenye kelele sana, "mbona mbia hazipiti...?"
Kuna wanaochangia ili kusaidia kufanikisha sherehe, hawa ndio wachangiaji wanaotoa michango ya maana na hawana makuu, wanaweza hata wasije kwenye sherehe. Hata akija ni bia moja au mbili baada ya zawadi hujiondokea mapema kwenda kunywa mahali pengine au kujirudia kwake mapema.
Pia kuna wachangiaji mabishoo kutoa maahadi makubwa ili kuonyesha jeuri ya pesa. Hawa kwenye vikao, wana kelele sana. Wengine ili kutafuta masifa, wanatoa ahadi nzito mwishowe huishia kuingia mitini. Hawa ni wachangiaji hatari.
Yote tisa kumi ni sisi wenyewe wahusika wa sherehe kushindwa kusoma dalili za nyakati, kutaka kufanya mambo makubwa huku uwezo hatuna, matokeo ni sherehe za vichekesho, mambo haya huwakumba sana masuper star wa Bongo.
Sherehe tufanye jamani, shirikisha marafiki ndugu jamaa na majirani, ni aibu mtu hamjuani ndio kwanza umetambulishwa leo alafu anakutolea kadi ya mchango kama fund raising campaign ya issue muhimu. Siku hizi ndio mambo yanazidi, kuanzia michango ya ubatizo, arobaini, maulid, kumtoa mtoto sunna,ngoma, kumunio ya kwanza, kipaimara, engegement, kitchem party, back party, mpaka birthday!.
Tufike mahali mtu ujikune unapofikia, kwani kila sherehe lazima mchango?. Twende kwenye elimu sasa.