Nichagueni kuwa Rais wenu 2025 niwafanyie yafuatayo...

Umeongelea uhuru wa mavazi ila upande wa uhuru wa faragha ujagusia ( mashoga)
Kabisa hilo litakuwepo kwenye ilani ya uchaguzi. Labda kwa kudodosa kidogo. Serikali yangu haitaruhusu ushoga maana serikali yangu japo haitakuwa na dini ila wapiga kura wangu wana dini. Na hakuna maandiko yeyote ya dini yanayoruhusu ushoga. Hivyo kitakachofanyika ni kifuatacho.

Mtu yeyote akithibitika kuwa ni shoga au anajihusisha na mambo ya ushoga atakamatwa na kupelekwa kwenye rehabilitation centre. Serikali yangu itakuwa inaamini kuwa ushoga ni ugonjwa.

Hakuna mwanaume mwenye akili timamu anayeweza kujihusisha na ushoga hivyo shoga yeyote ni mgonjwa wa akili na anahitaji matibabu. Hivyo atapelekwa kwenye hizi centre kutibiwa.
 
Kabisa hilo litakuwepo kwenye ilani ya uchaguzi. Labda kwa kudodosa kidogo. Serikali yangu haitaruhusu ushoga maana serikali yangu japo haitakuwa na dini ila wapiga kura wangu wana dini...
Swali langu: Je, kuna dini inaruhusu kutembea uchi/nusu uchi?
 
Ndio mkuu. Adamu na Hawa hawakuwa na nguo.
Hahahahaha sawa ila sababu nahisi walikuwa uchi nawala hawakutambua kuwa nitatizo kuwa uchi ila uliona walipomuhasi Mungu nini kilitokea???

Umeongelea kuhusu mifuko ya hifadhi kama NSSF kuwa utaifuta Je unalifahamu lengo la uwepo wa mifuko hiyo??
 
Lengo la hiyo mifuko ni kumsaidia mstaafu atakapokuwa hana uwezo tena wa kufanya kazi. Lakini hilo halifikiwi. Watu wanakufa bila kupata hela zao. Watu wanaacha kazi au kuachishwa kazi kabla ya umri wa kustaafu.

Kijana wa miaka 30 au 40 anapoacha kazi halafu unamwambia asubiri hela yake ya NSSF atakapofikisha miaka 60 ni uwendawazimu. Serikali yangu haitakupangia lini unataka kutumia hela yako. Hiyo ni hela yako unatakiwa uitumie upendavyo.
 
Sawa tupo pamoja, mimi nadhani badala yakuwaza kuifuta nadhani ungerekebisha baadhi ya sheria ya hiyo mifuko.

-Mtu anapoachishwa/kuacha kazi basi awe nahiari yakuchukua pesa zake au pesa hizo iwe dhamana yakukopea mkopo bank. Nahili liwe linafanyika ndani ya miezi mitatu toka mtu anapoachishwa kazi au kuacha kazi.

-Mstaafu anapostaafu basi pesa yake aweze kupewa kwawakati isizidi miezi mitatu. Na hicho kipindi anaposubiria mafao yake basi aendelee kupokea mshahara uleule aliokuwa anapokea akiwa kazini.
 
Kuna watu watadhani labda nafanya masihara ila ukweli nimejipanga kuchukua nchi kama watanzania mnataka kuachana na haya maisha magumu.
Yafuatayo ndio yatafanyika kwenye utawala wangu....
Unaweza kuwa umeandika ukiwa unatania labda lakini imeongea points kubwa mno ambazo zote hamna Rais anaye weza kuzitekeleza. Hata wewe ukiwa Rais haiwezekani pia kuyatekeleza 😂 kwa budget ipi kwanza na uchumi wetu huu 😂😂😂.

umeyachambua mambo mazito ambayo hayafanyiki naamini ndiyo mambo ambayo unatamani yafanyike. Kungekuwa na namna ya kusajiri ungesajiri Hoja zako maana wahuni watapita nazo. Nimependa hasa kwenye NSSF, kwa wabunge wananchi kuwatoa na kujitibia wenyewe, kwenye biashara, kubomoa kariakoo, na Veta na watu kutoajiriwa bila kuonesha tafiti 😂😂.

Ulicho kisahau ni kuwa na wewe kama Rais usipo tekeleza wananchi tukukatae na tuweke makubaliano ya maandishi kabla ya kuapishwa 😂😂😂🤗
 
Una sera za kuvutia sana, sema mkishapewa mamlaka... haya uliyoyasema yanaishia kwenye maandishi utekelezaji ni sifuri.
 
Sawa tupo pamoja, mimi nadhani badala yakuwaza kuifuta nadhani ungerekebisha baadhi ya sheria ya hiyo mifuko....
Kwani kuna shiga gani mtu kujihifadhia hela yake mwenyewe? Serikali yangu itakuwa ya kujenga Tanzania mpya. Haya mambo ya kuona kuna watu hawawezi kujiwekea akiba wenyewe hadi mtu mwingine awawekee hela zao nitayafutilia mbali.

Kwanza itasaidia watu kuwa wabunifu na kunoa akili zao. Utaratibu wa sasa licha ya kuumiza wastaafu na waliaochishwa kazi pia unadumaza akili. Mtu awe responsible na hela yake.

Atakuwa makini kwenye kuitumia au kuiwekeza maana atakuwa anajua akiitumbua atahangaika uzeeni, japo hata sasa wastaafu wanahangaika licha ya kuwa walihifadhi hela zao NSSF.
 
Una sera za kuvutia sana, sema mkishapewa mamlaka... haya uliyoyasema yanaishia kwenye maandishi utekelezaji ni sifuri.
Mkuu nikigombea wewe nipe kura tu, mengine niachie mimi. Nakuhakikishia kura yako haitaenda bure.
 
Huyu mwaandishi kichwa sana. Sayansi itakuwa lazima serikali ya mapinduzi ya sayansi Tanzania.
 
Back
Top Bottom