Nichagueni kuwa Rais wenu 2025 niwafanyie yafuatayo...

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,666
8,498
Kuna watu watadhani labda nafanya masihara ila ukweli nimejipanga kuchukua nchi kama watanzania mnataka kuachana na haya maisha magumu.

Yafuatayo ndio yatafanyika kwenye utawala wangu:

1. Mifuko ya hifadhi ya jamii NSSF na PSSSF nitaifyekelea mbali
Michango ya wafanyakazi itaenda kwenye account zao binafsi badala ya hii mifuko ya hifadhi ya jamii. Mfanyakazi atakuwa na uhuru wa kutumia hela yake muda wowote anaotaka. Hakuna mambo ya kumpangia mtu lini aitumie hela yake.

2. Elimu
Mfumo wa elimu kuanzia shule ya msingi hadi A-Level nitaubadirisha. Masomo yote yasiyokuwa na tija nitayafyekelea mbali. Nitaweka kipaumbele kwenye masomo ya hisabati na sayansi. Masomo ya sayansi na hisabati yatakuwa ya lazima. Nitahakikisha kuanzia darasa la kwanza wanafunzi wanapata msingi mzuri wa masomo ya hesabu na sayansi. Najua kutakuwa na upungufu wa walimu wa masomo ya hesabu na sayansi kwa miaka ya mwanzo ya utawala wangu. Kuziba pengo la ukosefu wa walimu wa hayo masomo nitatangaza nafasi za walimu wa hayo masomo duniani. Walimu wa hayo masomo kutoka kokote duniani watapewa kibali cha kuja kufundisha Tanzania. Mishahara ya walimu itakuwa ni mikubwa kuliko mishahara ya kada yoyote Tanzania. Kwa kifupi mwalimu atakuwa na maslahi mazuri kuliko mfanyakazi yoyote wa serikali Tanzania.

Nitaanzisha vyuo vya utafiti na ugunduzi. Kutakuwa na vyuo maalumu kwa ajili ya utafiti na ugunduzi. Wanafunzi wote wa vyuo vikuu wanaosoma taaluma zinazohusiana na sayansi lazima waende chuo cha utafiti na ugunduzi kabla ya kutunukiwa shahada zao. Mwanafunzi hatatunukiwa shahada bila kuja na ugunduzi wowote kulingana na shahada anayosomea. Lengo la kuanzisha hii taasisi ni kupata wahitimu watakaoleta mapinduzi kwenye nyanja ya tekinolojia na sayansi. Sio graduate anamaliza chuo hajui hata kutegeneza dawa ya mafua. Utafiti wa magonjwa kama Corona na chanjo zake utakuwa unafanyika kwenye hizi taasis.

Vyuo vya VETA
VETA nitaiboresha kwa kuajiri walimu waliobobea kwenye ufundi. Wanafunzi wakihitimu VETA watakuwa na uwezo wa kutengeneza kile walichojifunza na kujiajiri. Kama alijifunza umeme wa magari awe na uwezo wa kuifumua injini ya gari na kuitengeneza upya. Kama alijifunza umeme wa majumbani awe na uwezo na uelewa mpana wa umeme, aweze kutatua changamoto yoyote ya umeme. Awe na uwezo wa kuunda vifaa vinavyotumia umeme. Kiufupi wahitimu wa VETA watakuwa na uwezo wa kutengeneza au kuunda gari, TV, fridges na watakuwa kimbilio la matatizo yote ya kiufundi.

3. Ubunge
Ili uwe na sifa ya kugombea ubunge angalau uwe na elimu ya form six. Huwezi ukawa mtunga sheria zitakazoathiri maisha ya watanzania ukiwa huna elimu. Mbunge atakuwa mfanyakazi kama mfanyakazi mwingine wa umma. Mishahara ya wabunge itakuwa ya kawaida tu. Mbunge akitaka kununua V8 atanunua kwa hela yake sio kukopeshwa kwa hela ya umma. Mbunge akiugua atajitibu kwa hela yake au kwa bima kama anayo. Hii nchi bado ni maskini, sitaruhusu tabaka la watu watibiwe kwa hela ya umma wakati tabaka jingine wanajitibu kwa hela yao. Wananchi watakuwa na madaraka ya kumfukuza mbunge baada ya miaka 3 wakiona hafanyi yale aliyoyaahidi kuyafanya jimboni.

4. Utawala wa sheria na haki
Nitafuta sheria zote kandamizi. Mfano sheria ya kwanza nitakayoanza nayo ni hii ya miaka 30 ya kutembea na mwanafunzi. Haiwezekani mtu umfunge miaka 30 wakati hakumlazimisha mhusika. Kosa na adhabu ni mbingu na ardhi. Miaka 30 itabaki kwa wabakaji.

5. Uhuru wa kuvaa na mavazi
Nitapeleka mswada bungeni wa kulinda uhuru wa kuvaa. Kwenye utawala wangu kila mtu aliyepo ndani ya mipaka ya Tanzania atakuwa na uhuru wa kuvaa anachotaka. Hili swala la wanawake kuvaa nguo fupi na kuanza kuzomewa nitalikomesha. Ukimzomea mwanamke aliyevaa nguo fupi adhabu yake ni miezi 6 jela na faini juu. Haiwezekani mtu umpangie cha kuvaa, au amkoseshe uhuru wa kuvaa anachopenda. Mwili ni wake, hata akitaka kutembea uchi ni yeye. Wewe kama hupendi alichovaa acha kumwangalia. Kila mtu atakuwa na uhuru kamili wa kuvaa anachotaka ilimradi hasababishi maumivu kwa mtu mwingine.

6. Kuijenga upya Kariakoo na Posta
Mji wa Dar es salaam nitauvunja na kuujenga upya. Kariakoo imejengwa hovyo sana. Barabara zimekaa kama sambusa. Kariakoo nitaivunja na kujenga upya. Kuna wengine watasema itakuwa ni hasara kuyavunja maghorofa ya kariakoo, lakini nawaambia bora tuvunje sasa hivi kuliko kusubiri. Dunia inapiga hatua kwa kasi sana. Huko mbele miaka ijayo Karikoo itakuja kuvunjwa tu ili kuendana na mionekano ya majiji ya kisasa duniani. Hivyo bora tukaivunja sasa hivi badala ya kusubiri baadae. Faida ya kuivunja ni kubwa ukilinganisha na hasara ya kuendelea kubaki kama ilivyo.

7. Huduma ya maji safi na salama
Kila familia itaunganishwa na bomba la maji. Kutakuwa na mfumo wa maji safi na maji taka kwa kila sehemu ya Tanzania. Vyoo vyote vitaunganishwa na mfumo wa maji taka. Hakutakuwa na mambo ya kuchimba shimo la choo. Wewe ukijenga nyumba yako utawaita watu wa maji taka ili waje wakupe ramani ya kuunganisha choo chako na mfumo au bomba la maji taka. Maji taka yatakuwa recycled na kurudi tena majumbani na viwandani kwa ajili ya matumizi, hivyo shida ya maji itakuwa jambo la historia.

8. Huduma ya afya itapatikana bure kwenye hospitali zote za serikali
Hospital zote za kata zitaboreshwa. Madaktari wazuri wataajiriwa kila hospitali ya kata. Huduma za kujifungua salama kwa wajawazito zitatolewa kwenye hospitali za kata. Serikali itaweka utaratibu mzuri usioumiza wananchi wa kuchangia huduma ya afya.

9. Miundo mbinu,
Nchi nzima mpaka barabara za vijijini zitaunganishwa kwa lami. Mabasi yatasafiri masaa 24. Serikali itajenga high ways za kuunganisha mikoa. Dereva akiamua kutumia hizo high ways haruhusiwi kuendesha chini ya speed ya Km 120 kwa saa. Kwa wale abiria wanaosafiri kwa basi au usafiri binafsi, bei ya chakula njiani serikali itahakikisha haimuumizi mwananchi wa kipato cha chini.

Kwa sababu vipato vya Watanzania vitaongezeka na standard ya maisha itapanda, serikali itahamasisha uwekezaji wa shopping malls. Kila mji utakuwa na shopping mall kubwa za kisasa angalau mbili. Humo kwenye shopping malls kutakuwa na maduka, migahawa, sehemu za watoto kucheza, ice skating na kumbi za starehe. Nitataka watanzania wapate mambo yanayopatikana Ulaya na Marekani.

10. Kodi kwenye biashara
Kwa biashara mpya zitakazofunguliwa, hakuna kulipa kodi kwa muda wa mwaka mmoja, lakini mfanyabiashara atatakiwa kuweka kumbumbuku nzuri ya mahesabu ya biashara yake ili baada ya huo mwaka mmoja kupita serikali iweze kuanza kumtoza kodi. Kodi ya kampuni nitaishusha hadi 25% tofauti na sasa ya 30%. Koda ya VAT nitaishusha hadi 12% tofauti na sasa ya 18% ili kuongeza purchasing power ya mnunuzi.

11. Uwekezaji kutoka nje
Nitaanzisha sera nzuri ya uwekezaji. Mtu au kampuni yoyote inayotaka kuwekeza Tanzania itawekeza bila kukutana na ukiritimba wa aina yeyote. Sera ya uwekezaji itakuwa rahisi sana. Ukitaka kufungua biashara au kampuni serikali itahakikisha ndani ya wiki moja tu muwekezaji amepata vibali vyote vinavyomruhusu kuanza biashara.

12. Ajira
Wizara ya ajira, mimi rais wa nchi nitakuwa pia waziri wa ajira. Narudia, mimi rais wa nchi nitakuwa pia waziri wa ajira. Nitahakikisha shuguli za kiuchumi zinaongezeka, wawekezaji wa nje na ndani wanaongezeka, budget kubwa ya serikali nitaielekeza kwenye ajira kwa vijana. Nitahakikisha kila mhitimu anapata ajira ndani ya mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo yake. Nitatenga siku mbili kila mwezi kwa ajili ya kuongea na vijana wasiokuwa na ajira kwa njia ya simu. Namba yangu ya simu nitaiweka public. Hizo siku mbili kwa mwezi nitapokea takwimu za vijana wasiokuwa na ajira ili kujua ukubwa wa tatizo.

Haya kazi kwenu watanzania wenzangu.
 
Mkuu mawazo yako mazuri sana, shida ni kwamba katiba yetu mpya inataka aliekalia kiti atawale mpaka "AKINAI" hivyo nasikitika kwa 2025 haitowezekana! Labda miaka mingi mbele Siku za usoni huko!

Ila trust me, kuna mawazo mengine wataiba humu!
 
Hiyo namba 5 ndio yenyewe🤣🤣🤣, chukua uzito 👊🏼, alafu Tz utaiweza kweli, isije kushinda baadaye ukaikimbia ka vile ulimfanya Shem?... Mitano tena!!!
✌️
Namba tano ndio yenyewe sio? Hahahaha. Ila watoto wakivaa vimini wanapendezesha mji eeh?
 
Namba 1 usifyekelee mbali, boresha mifuko
Namba 5 nakubali
Kwenye ubunge hapo sifa zaidi zinatakiwa ziongezwe including ukomo wa ubunge.
Namba 10 nakupa big up next prezidaa
 
40 Reactions
Reply
Back
Top Bottom