Nichague kazi binafsi au TAKUKURU?

Nichague kazi binafsi au TAKUKURU?

kisana kiki

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2016
Posts
266
Reaction score
287
Wanajamvi mambo vipi?

Hivi karibuni, kama wiki moja imepita sasa nimepata ofa ya kazi kampuni kubwa ya binafsi (Jina Kapuni) inayoanza mwezi wa kwanza 2022.

Ofa yao ukiacha marupurupu mengine kadhaa ni milioni 2.2 kama Gross Salary kwa mwezi na kazi ni Dar es Salaam.
Sasa leo nimeona jina langu lipo miongoni mwa majina yaliyotolewa na TAKUKURU kwa ajili ya usaili wa Aptitude Test kwa kazi ya Afisa uchunguzi (Investigation Officer) utakaofanyika Jumamosi ya tarehe 8.1.2022 pale Dodoma ukifuatiwa na usaili wa ana kwa ana kwa watakaofaulu.

Natambua kazi za Serikali zina uzuri wake hususani kwenye security na mikopo katika kusukuma maisha.

Naomba ushauri wenu katika hili,

1. Je niipoteze nafasi ya kwenda Dodoma kufanya usaili wa TAKUKURU na niendelee na kazi hii niliyopata?

2. Niende nikafanye usaili na nisikilizie ofa yao itakuwaje?

3. Nielekeze nguvu kwenye kazi ya TAKUKURU na niachane na sekta binafsi kutokana na faida zake?

Ushauri wenu na busara unahitajika Wakuu.

Natanguliza Shukrani.
 
Sasa hata huko takukuru bado hujapita, fanya kwanza mtihani uvuke, uende oral na ukishapata ndio uje uombe ushauri

Kumbuka interview za TAKUKURU zinafanyika Dodoma Mkuu.

Kwahiyo kuna kusafiri na kujiandaa vile vile.

Mtu anaweza kuwa na uzoefu na haya mambo ya Serikalini na akakwambia mapema kabisa kuwa usiende au namna gani.
 
Nenda,.. ni muda mchache tu Kisha utaludi na mambo yako ya private ila kumbuka kuwa PRIVATE SECTOR HAWANAGA GRANTEE.
 
Niko na situation kama yako mtoa uzi

Ushauri nilioamua kuufuata ni kujikita kwenye sekta binafsi na kufanya kazi..

Naona pamoja na ushauri mzuri wa kuingia Serikalini, moyo unaniambia tofauti kabisa.

Ngoja tuishi huku tuone maisha yanasema nini.
 
Utakuwa mjinga wa Hali ya juu kuacha 2.2m halafu uhangaike na vilaki 6 au 7.....na utakufa na umasikini huku ukiwa mchawi ..

Ukipiga hesabu zako fresh ndan ya mwaka tu ushakuwa pazuri....huko private angalia aina ya mkataba km wa mwaka au lah...then ndan ya mwaka huohuo usilaze damu wekeza ...ishi mguu nje ndani utatoboa...

Ukifika huko ukaanza kula Bata utakuja kujuta...

Watumishi wa gvt Wana njaa na madeni 75% hawana furaha na kazi wanazozifanya...
 
yan hapo inatakiwa assave hio 2.2 angalau atumie lak 4 tu kwa mambo yote na kisha haraka aanze ujenz
 
Wanajamvi mambo vipi?

Hivi karibuni, kama wiki moja imepita sasa nimepata ofa ya kazi kampuni kubwa ya binafsi (Jina Kapuni) inayoanza mwezi wa kwanza 2022.

Ofa yao ukiacha marupurupu mengine kadhaa ni milioni 2.2 kama Gross Salary kwa mwezi na kazi ni Dar es Salaam.
Sasa leo nimeona jina langu lipo miongoni mwa majina yaliyotolewa na TAKUKURU kwa ajili ya usaili wa Aptitude Test kwa kazi ya Afisa uchunguzi (Investigation Officer) utakaofanyika Jumamosi ya tarehe 8.1.2022 pale Dodoma ukifuatiwa na usaili wa ana kwa ana kwa watakaofaulu.

Natambua kazi za Serikali zina uzuri wake hususani kwenye security na mikopo katika kusukuma maisha.

Naomba ushauri wenu katika hili,

1. Je niipoteze nafasi ya kwenda Dodoma kufanya usaili wa TAKUKURU na niendelee na kazi hii niliyopata?

2. Niende nikafanye usaili na nisikilizie ofa yao itakuwaje?

3. Nielekeze nguvu kwenye kazi ya TAKUKURU na niachane na sekta binafsi kutokana na faida zake?

Ushauri wenu na busara unahitajika Wakuu.

Natanguliza Shukrani.
Chagua kampuni binafsi ambayo tayari unauhakika nayo hiyo nyingine huna uhakika nayo kama utaipata
 
Kwa kweli private kama unapenda career growth na future nzuri unatakiwa uende huko ila kama unapenda kudumaa nenda serikalini private sector kwa miaka mitano au sita unakua umeshafika hata level ya umanager lakini serikalini ni changamoto sana ila ku survive private na kukua unatakiwa uwe mtu wa kukaa kampuni fulani miaka i.e miwili halafu unatafuta sehemu ingine ya cheo cha juu xaidi utaona maisha mepesi ila kama unataka ukae sehemu moja mpaka ufukuzwe huko private utapata tabu sana...
 
Nenda TAKUKURU kule mshahara mdogo ila rushwa njenje na ukikaa muda ukawekwa kitengo kizuri maisha yanaenda Safi kabisa.

Ila ndio ujue utaishi kwa rushwa sio mshahara otherwise kama huwezi uhuni Baki zako private sector mbona watu wameanzia maisha Private sector mpaka wanastaafu na wanakuwa gurus?

Pima upepo mkuu utaamua mwenyewe. Kama una mshahara wa 2.2 kwa sasa imagine ndani ya miaka miwili utakuwa wapi with all the experience?
 
Utakuwa mjinga wa Hali ya juu kuacha 2.2m halafu uhangaike na vilaki 6 au 7.....na utakufa na umasikini huku ukiwa mchawi ..

Ukipiga hesabu zako fresh ndan ya mwaka tu ushakuwa pazuri....huko private angalia aina ya mkataba km wa mwaka au lah...then ndan ya mwaka huohuo usilaze damu wekeza ...ishi mguu nje ndani utatoboa...

Ukifika huko ukaanza kula Bata utakuja kujuta...

Watumishi wa gvt Wana njaa na madeni 75% hawana furaha na kazi wanazozifanya...

Mkuu hii si kazi yangu ya kwanza na wala mimi sio mtu wa bata kabisa.

Niliuliza tu kupata ushauri wa wadau.

Nimekupata vizuri sana lakini.
 
Pitia mkataba wa iyo private kama hata angalau miaka 2 utakuwa pazuri uko TAKUKURU jiandae kula laki 7

Mkataba ni wa kudumu, hauna time limit unless niamue kuacha au wafanye termination Mkuu.
 
Back
Top Bottom