Nia Yangu ya Kumfungulia Mashtaka Pius Msekwa hapa Nebraska

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,570
19,444
Mimi kama mmoja wa wanachama waandamizi wa Jamii Forums ambapo nimekuwa mwanchama kwa karibu miaka mitano sasa tangu ikiwa Jambo Forums kabla ya kubadili jina na kuwa Jamiiforums nimekerwa sana na matamshi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM kuwa forums hii ni ya vijana wa CHADEMA. Naona kuwa amenivunjia sana heshima yangu mbele ya wenzangu kwa kunipa image ya kuwa mimi ni mpiga propaganda wa CHADEMA.

Baada ya kutafakari kwa kina matamshi ya Pius Msekwa na jinsi yalivyoathiri image yangu kama mwanachama wa JamiiForums, nimeamua kumfungulia mashtaka ya defamation kwenye mahakama ya Douglas County hapa Omaha Nebraska nchini Marekani. Nimejadiliana na mwanasheria wangu ambaye amenipatia kifungu cha sheria kinachoniruhusu kumshitaki raia wa nchi ya nje kwenye mahakama hii, iwapo marekani ina uhusiano wa kibalozi na nchi ya mshitakiwa. Sasa hivi tuko katika hatua za mwisho mwisho za kukusanya ushahidi imara.

Nimeshapata nakala za magazeti ya kiswahili na kiingereza ila nimekuwa natafuta video clip yenye kumwonyesha Msekwa akiwa anasema maneno hayo. Vile vile bado tunashauriana kiwango cha malipo ya Punitive Damages na Compensatory Damages; mwanasheria anashauri kuwa viwango hivyo vipimiwe zaidi kwa kuangalia jinsi gani Msekwa binafsi na chama chake walivyofaidika au watakavyofaidika kutokana na matamshi yake hayo, na kwa kiasi kidogo jinsi gani yalivyoathiri image yangu binafsi kama mwanachama mwanadamizi ambaye hujitambulisha kwa wenzagu wote kuwa mimi ni Premium Member wa JamiiForums.

Tukikamailisha taratibu zote, nitawaarifuni au mtasikia kwenye vyombo vya habari Msekwa akiwa subpoenaed kwenye kesi hii ambayo pamoja na mambo mengine ninataka kuwadhibiti wanasiasa wasiwe wanaropoka mambo bila kuwa na uhakika nayo.
 
Na hivyo umepata imani kuwa una kesi nzuri ambayo una uwezekano mkubwa wa kushinda?

Itetegemea na ushahidi nitakaofikisha mahakamani; ndiyo maana nimesema kuwa tunakusanya ushahidi imara. Bila ya kuwa ushahid imara siwezi kupoteza muda wangu.
 
Hongera kwa ujasiri mkuu, endelea na maandalizi ya kesi. Ukiwa kiongozi unatakiwa kuwajibika na kauli zako.
 
Mkuu ni vema ukafile case hiyo ili Msekwa ajifunze kuwa makini. Ila sijapenda uliposema ...mpiga propaganda wa chadema ni kukuvunjia heshima, kwani kuwa mtetezi wa cdm ni nongwa? Ningependa kila mtanzania aitwe mwanacdm ili mafisadi wamwogope kila raia na hapo wangeacha ujangiri wao dhidi ya umma. Ikumbukwe kuwa aliko mwanacdm fisadi anapakimbia!

Mkuu, ukimaliza kesi hiyo file pia ya mafisadi wanaoua kikazi cha leo na kijacho kwa kuwaondolea raslimali muhimu! All the best!
 
Mkuu ni vema ukafile case iyo ili Msekwa ajifunze kuwa makini. Ila sijapenda uliposema ...mpiga propaganda wa chadema ni kukuvunjia heshima,kwani kuwa mtetezi wa cdm ni nongwa? Ningependa kila mtanzania aitwe mwanacdm ili mafisadi wamwogope kila raia na hapo wangeacha ujangiri wao dhidi ya umma. Ikumbukwe kuwa aliko mwanacdm fisadi anapakimbia! Mkuu,ukimaliza kesi iyo file pia ya mafisadi wanaoua kikazi cha leo na kijacho kwa kuwaondolea raslimali muhimu! All the best!

mkuu

hapo kwenye red kuna propaganda pia .... mimi nimemsoma
 
una kadi ya uanachama? jina lako halisi ni Kichuguu? wewe ni mwanachama au mwanzilishi, na kama sio mwanzilishi una uhakika haikuanzishwa na vijana wa cdm? unamshtaki msekwa au ccm, kama ni mskwa kwa nini uangalie manufaa watakayopata ccm? ......... ngoja niamke nikachinje kambuzi kangu nipate kisusio.
 
Wenye video clip ya hayo maneno mpeni kichuguu ili kuongeza ushahidi na kama state ya Nebraska itaweza kum-subpoena hata kama hatatii hiyo amri lakini italeta heshima jamiiforums kwasababu waropokaji wengine wataanza kuogopa kutoa maneno yasiyokuwa na mbele wala nyuma. Legal Damaging ya kesi kama hizi huwa kubwa sana.

Ieleweke kuwa kichuguu anahaki ya kulalamika (kama mwanachama wa JF) kwasababu jamiiforums iko registered godaddy.com (US company) na vilevile iko-hosted kwenye server za Chicago (US). Kutokana na federal laws sites zozote zilizokuwa registered/hosted US zinalindwa na sheria za Marekani. Kama mtu yoyote atafanya attack (cyber/damaging yoyote kama false claims) kwenye website hizo basi anaweza ku-sued.
 
una kadi ya uanachama? jina lako halisi ni Kichuguu? wewe ni mwanachama au mwanzilishi, na kama sio mwanzilishi una uhakika haikuanzishwa na vijana wa cdm? unamshtaki msekwa au ccm, kama ni mskwa kwa nini uangalie manufaa watakayopata ccm? ......... ngoja niamke nikachinje kambuzi kangu nipate kisusio.

Ukishamaliza kuchinja mbuzi jiandae kumsindikiza Msekwa tukutane hapo Omaha mahakamani. Wewe umejiunga mwaka 2010 tu, hujui njia ambayo wengine tulipitia kuipa uhai jamii forumas hadi wewe ukaikuta miaka minne baadaye na kuamua kujiunga nayo.
 
Kaka nadhani watambua vyema fitiza zifanyazo na chama chake pamoja na serikali ya chama chake. Nadhani angalia wasije kukutibulia mambo yako huko, isije ikawa ya ze utamu! Hili jukumu ni vyema km ingefanywa na sisi huku tz. Kifupi ni wazo zuri, na imeonyesha ni kwa kiasi gani umekereka, realy ur thinker and patriot. Tupo pamoja!
 
Back
Top Bottom