Nia ya Mchungaji Uchaguzi Mkuu 2015

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
Uchaguzi 2015:

Itikadi kuu ya kitaifa iwe ni kujenga upya Tanzania, kama Taifa huru yenye kuzingatia vipaumbele vifuatavyo : Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uwajibikaji, Uadilifu Uimara na Umoja wa Kitaifa

Wenye Nia Urais, Ubunge, Udiwani wapimwe si kwa kauli zao tuu, bali kwa matendo yao kama wanaweza kujenga: Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uadilifu, Uwajibikaji, Uimara na Umoja

Tusipime wagombea kwa utamu na ntiririko wa ufahamu wa kuongea au maneno tunayotaka kusikia, tusikubali kuwapa dhamana na majukumu makubwa kutonkana na umahiri wa kampeni zao, kujaa kwa umati wa wafuasi au vilio vyao vya kulilia dhamana ya kumkomboa Mtanzania.

Tukague Ufanisi wa utendaji wa wagombea katika miaka yao ya uwakilishi na kulitumikia Taifa na kuzioanisha na kauli walizozitoa miaka hiyo ya nyuma. Je tuwape dhamana na kwaamini wataweza sasa? Kama walishindwa kujenga mfumo fanisi wa maendeleo na uwajibikaji katika ngazi za wilaya, je kwenye duru za Kitaifa watatuaminishaje wana uwezo kufanikiwa?

Tuhoji uimara wao na utendaji wao mpaka sasa katika miaka mitano iliyopita, wamewafanyia nini cha maendeleo wananchi wachache waliowapa dhamana ya uwakilishi na uongozi? Je kama katika wilaya na majimbo, wamepata matatizo ya ushawishi kustawisha jamii iliyo imara na yenye maendeleo endelevu na si ya maneno,tuaminije wanaweza kuongoza Taifa zima?

Tuhoji umadhubuti na uimara wa wagombea kusimamia haki, kujenga demokrasia ya kweli, kukubali upinzani, kukemea na kuwajibisha uhujumu. Je matendo yao yameonyesha msimamo unaoeleweka kujenga jamii yenye demokrasia ya kweli yenye ushirikishi?

Tuhoji, je wamekuwa wawazi bila woga kupiga vita uhujumu ambao una sura mbali mbali kama uvivu, uzembe, matumizi mabaya ya dhamana na fedha, uhujumu, rushwa na uonevu?

Uimara wa Tanzania na maendeleo yake ya kijamii, kiuchumi na kisiasa si wingi wa rasilimali na ahadi za kuneemeka bila kuzingatia: Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uadilifu, Uwajibikaji na Umoja katika kujenga Uimara wa Taifa na Utaifa!

Taifa letu, haliwezi kupiga hatua mbele kushinda vita dhidi ya Ujinga, Umasikini, Maradhi na Uhujumu bila kuzingatia malengo haya ya msingi.

Hatutaweza futa ujinga na maradhi tusipothamini Utu, Uzalendo, Uadilifu, Uwajibikaji, Ufanisi na Umoja.
Ni kujidanganya eti utajiri wa rasilimali na mapato ya uzalishaji yatutasaidia kutatua matatizo ya Taifa huku nguzo kuu na tunu za Utaifa wetu zinapuuziwa na kutokupewa kipaumbele kama dira iliyo kuu ya kujenga jamii shirikishi.

Vita kuushinda Uhujumu havina faida kwa Umoja hatuna Uzalendo, Utu, Ufanisi, Uwajibikaji na Uimara kupambana na ufisadi, rushwa , ujangili, utegemezi na utovu wa nidhamu!

Haitawezekana kufuta Umasikini pasipo kuwa na kipumbele cha Uzalendo, Utu, Ufanisi, Uwajibikaji, Uadilifu au Umoja pamoja na rasilimali zote tulizonazo na kujitangaza kwa majisifu.

Tuliposema ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi Siasa Safi na Uongozi Bora, ni wakati huu ambapo tunahitaji kuchagua siasa safi na uongozi bora ulio wazi nawenye dhamira ya kulitumikia Taifa kwa dhati kuzingatia vigezo hivi vya : Utu, Uzalendo, Ufanisi, Uadilifu, Uimara, Uwajibikaji na Umoja.

Watanzania tuachane na mazoea ya kuamini maneno ya Wanasiasa ambao hawajengi Umoja au Ushirikishi kutokana na Amani tuliyonayo.

Tanzania na Watanzania ni lazima tujisahihishe mwaka huu wa uchaguzi kwa kutoa dhamana kwa watu wenye hekima, busara, ujasiri na uimara wa kutafakari, kufanya kazi na kufanya maamuzi yenye matokeo chanya: bora na endelevu. Tuwape dhamana watu ambao ni wepesi kujisahihisha na kufanyia kazi mapungufu yao.

Watanzania tukatae kupewa viongozi wasiojiheshimu, waongo, wazandiki, wanafiki na wenye tamaa na uchu wa madaraka na mamlaka. Hawatufai Ng'o!

Tanzania itajengwa na kuongozwa na viongozi waadilifu, wasikivu, wavumilivu, wachapa kazi wenye kukubali kukosolewa na kufanyia kazi kwa moyo maoni tofauti na mawazo yao.

Nami natangaza rasmi: Nia yangu ni kuleta na kupata Uongozi utakaoongoza kuzingatia: Uzalendo, Utu, Uadilifu, Ufanisi, Uwajibikaji,UImara na Umoja kwa Taifa letu na Watanzania wote kwa ujumla bila kujali tofauti zozote zile!
 
Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,535

Mimi ningewaomba wakuu wa JF Maxence Melo iweke mada hii pia kule Uwanja wa SIASA maana lengo kuu ni kusambaza Ujumbe huu muhimu sana kwa wananchi wasomaji.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom