Nia ya Kuishitaki EWURA

Nia ya Kuishitaki EWURA

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,471
Reaction score
1,578
Wakuu, nawaza tu, hivi nikipata mwansheria mzuri sana nikafungua kesi ya kikatiba dhidi ya EWURA kwa ubaguzi na upendeleo wa baadhi ya wananchi nitakosea?

Yaani bei ya mafuta haifanani nchi nzima wakati tuko nchi moja? Sisi wananchi tulio mbali na bandari tunakosa gani ndo tubebeshe bei ya juu? Kwa nini bidhaa zingine zinatoka Dar huko huko lakini zinauzwa kaa bei sawa na ya Dar?

Hii si ni kinyume cha katiba na ubaguzi wa waziwazi kwa wananchi kutokana na mahali wanakoishi?
 
Kutoka bandarini ambapo ndio point A labda hadi dar es salaam ni sawa na kutoka point A hadi Mbey au hadi Bukoba kila sehemu ina umbali wake kuna gharama za kusafirisha hiyo bidhaa lazima iwe inajumuishwa kwenye mafuta
 
Washtaki pia wakurudishie nauli ya Dar moro iwe sawa na Dar mwanza kwa basi maana wanacharge tofauti
 
Back
Top Bottom