Ni zaidi ya kinga ya UKIMWI - TAFAKARI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni zaidi ya kinga ya UKIMWI - TAFAKARI

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WomanOfSubstance, Jun 18, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]TAKWIMU HIZI ZIMENIFANYA NITAFAKARI.NDOA HUWEZA KULETA HATARI ZAIDI KULIKO KINGA DHIDI YA UKIMWI:
  "According to the data from Tanzania HIV AIDS and Malaria Indicator Survey (THMIS) 2007-2008, the national prevalence among the sexually active populations (between 15 and 49 years of age) is reported to be 5.7 %. The data shows more women (6.6 %) are infected than men (4.6%). HIV prevalence is higher among women than men in both urban and rural areas and highest among married couples. Amongst ‘HIV-discordant couples’, there are more male-positive-female-negative couples than vice versa. Among certain older age groups, men have higher HIV prevalence than women."

  Hapo kwenye blue hapo!
  1. Inaonekana walio kwenye ndoa ndio wenye kuambukizwa/kuambukizana zaidi kuliko baina ya wasio na ndoa.
  2. Walio kwenye ndoa, kuna wanandoa ambao mmoja ameambukizwa wakati mwingine hana maambukizi.Na wengi wasio na maambukizi kati ya wana ndoa wanawake ndio wengi.
  3. Katika makundi yenye umri mkubwa, wanaume wengi wameambukizwa kuliko wanawake.

  Kuna dhana kwamba waliooana wanalindana dhidi ya UKIMWI kwa vile kutakua na uhakika wa mpenzi mmoja, asiye na maambukizi! Lakini kwa ukweli wa maisha ya siku hizi, inaonekana dhahiri kuwa ndoa yaweza kuwa chanzo kikubwa cha kuangamia kwa gonjwa la UKIMWI.

  Je nini kifanyike? watu wasioane? waliooana watumie kinga? au inakuwaje? TUJADILI


  [/FONT]
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani ni both ways inaweza kukuangamiza ama kukuokoa kutegemeana na uhusiano wa wanandoa. Ni kweli sio rahisi kutumia kinga ndani ya ndoa. Lakini ni kweli pia kwamba watu wengi wasio na uhusiano wa ndoa wanajamiiana bila kutumia kinga. So hata tukisema watu sasa wasiingie kwenye ndoa bado hilo haliwezi kuondoa maambukizi ya VVU. Kwa mfano ndoa nyingi za sasa hivi, bi harusi anapanda 'madhabuhuni' akiwa tayari ni mjamzito!
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Swala ni kuacha ngono zembe ,mme /mke mpende mwenzi wako hasa ukijua ukichepuka kidogo na kwenda nje ukafanya ngono zembe unamletea na mwenzi wako hili gonjwa....
  Tuheshimu ndoa zetu.
  Kwa wale single nikuambana na Condoms popote pale kama hawawezi kujizuia ...
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Haya mambo memngine ni yakufikirika zaidi kuliko kiuhalisia.
  Chimbuko la upendo ni kujipenda mwenyewe kwanza...ukijipenda, utajilinda, ....sasa kama wewe mwenyewe hujipendi kwa kiasi cha kutoona hatari ya kuambukizwa VVU, unafikiri unakuwa na upendo wa kumlinda mwenza wako?

  Kama unajipenda, hata ukitoka nje ya ndoa utahakikisha wewe mwenyewe huambukizwi...kwa namna yoyote ile, then, automatically utakuwa umemlinda mwenza wako.
   
 5. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,072
  Trophy Points: 280
  kumbe asilimia ya wenye ngoma ni ndogo hivyo?
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Ndugu yangu... hii takwimu usiione ndogo hasa kwa kuzingatia aina ya ugonjwa wenyewe.
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Swadaktaaaa!Bigirita umenena ukweli.... kwenye mahusiano kuna mengi... kuna ubinfasi .. mtu atataka kujifurahisha mwenyewe bila kujali athari kwa mwingine. Kibaya zaidi yule anayejiachia free style huko nje, anakuwa hajali kumlinda yule aliye naye kwa maana ya mwenzi wa ndoa.Inashangaza zaid kulivyo na resistance katika kutumia kinga ndani ya ndoa!
  Lakini cha kujiuliza... kwa hao discordant couples ( wanandoa ambao mmoja ana maambukizi ilhali mwingine hana) ni kwamba hawahusiani tena au inakuwaje? na je hao wenye umri mkubwa, ina maana wanaume wanaendelea kuambukizwa hata kwenye umri mkubwa zaidi ya wanawake kwa sababu zipi?
   
 8. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mi naona hakuna kinga ya HIV, zaidi kila mmoja kuwa mwaminifu kwa Mungu kiroho na si kimwili,

  nimesema kiroho na si kimwili kwa maana moja, watu ni waaminifu kwa Mungu kimwili kwa kuhudhuria
  sana ibada na si kulitendea kazi neno la Mungu ambalo ni msaada mkubwa kwa mwanadamu kujikinga na kuzishinda tamaa za mwili ambazo ni chanzo kikubwa cha uzinifu na uasherati,

  ukiwa mwaminifu kwa Mungu kiroho ina maana wewe unalifanyia kazi neno lake, hasa kwa kuenenda kwa hofu ya kumtii sana yeye, umekubari kuufisha mwili na kuuadhibu kwa kuukosesha starehe zote za
  dunia, ili kuistawisha roho yako na kuyafanya mapenzi ya Mungu, maana tusingejua kuwa kuzini ni dhambi, kama asingelisema usizini, huwezi jua kuwa kuiba ni dhambi kama asingelisema usiibe,
   
 9. mwanakwetu

  mwanakwetu Member

  #9
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tatizo la msingi kabisa ni mmomonyoko wa maadili na wala sio kuwa kwenye ndoa au kutokuwa kwenye ndoa, maana waliopo kwenye ndoa ndio hao wanatoka na kwenda kutafuta walio nje. Ukiangalia vizuri hizo takwimu zinaonyesha wanaume walio na umri mkubwa na wasichana walio katika umri mdogo ndio hasa wanaongoza kwenye maambukizi. Hiyo inatoa picha kwamba kina baba wanatoka kwenye ndoa zao na kufuata mabinti wadogo, mabinti nao wengi wao wanaendekeza tamaa na kushindwa kuthamini utu wao.
  Nadhani ipo haja sasa ya kukinusuru kizazi kijacho kwa kuanza kutoa elimu ya kujitambua kuanzia shule ya msingi. Hapa serikali inatakiwa kuwa mstari wa mbele kabisa kusimamia mitaala ya shule zote na kuacha hii 'akademia syndrome' maana kwa tathmini isiyo rasmi watoto wengi toka kwenye mchepuo wa aina hizi za shule za siku hizi ndio wamepoteza muelekeo kabisa kwa visingizio vya uzungu wanaofundishwa huko mashuleni.
   
 10. mwanakwetu

  mwanakwetu Member

  #10
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sio ndogo hivyo hao ni wale waliopima kwa hiari au kupimwa kwa lazima kutokana na hali za afya zao. Sasa asilimia ya waliopima kwa hiari sidhani kama inazidi 10% ya watanzania wote, fanya hesabu.
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  uko sahihi kabisa mkuu,
  lakini haya maadili tuayalindaje yasimomonyoke? ikiwa watu sasa kwa kiasi kikubwa tumejitenga na upendo wa Mungu kwa kuitawala na fahamu zetu za kimwili? kwa mwanadamu akijiendesha kwa akili zake mwenyewe, daima yu katika hatari sana maana hofu ya kumwogopa Mungu moyoni mwake hamna, usishangae Mtu anajaribu kumwuua mwanadamu mwenziye au ana mlawiti mtoto na pengine ni mwanae kwa madai hicho kitakuwa chanzo cha yeye kuwa tajiri, hii ni kwa sababu hekima ya Mungu haimo ndani yake bali ametawaliwa zaidi na akili za kibinadamu

  sasa ili maadili yasimomonyoke ni lazima tumuishie Mungu maana yeye ndiye chanzo cha maadili mema
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,045
  Likes Received: 23,820
  Trophy Points: 280
  Dawa ni kutubu na kufuata mapenzi ya Mungu.
   
 13. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hakika ndugu,
  tukitubu na kufuata mapenzi ya Mungu, uasherati hautatajwa kwetu, wala uchafu wowowte wa kutamani,
  kwa kuwa tutakuwa tumedhibiti miili yetu juu ya tamaa, kwa kuwa kweli ya Mungu itkuwa ndiyo kiongozi wetu, tutawapenda wake zetu kama ilivyoamuliwa na Mungu nao watatutii na kututhamini kama sehemu ya miili yao katika upendo
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Chris,
  Una point muhimu sana..lakini laiti ingekuwa rahisi kihivyo basi tungekuwa tunauzungumzia UKIMWI kama historia alongside Bubonic plagues na magonjwa mengine ya kipuku!
  Tatizo kubwa ni kwamba ugonjwa huu umegusa penyewe...kwenye udhaifu wa binadamu. Kila mtu anapataka eti.
  Mungu ametupa amri 10 kwa wale wenye kuamini hivi na katika amri hizo ya sita inagusa ishu hii.
  Amri hii ya 6 na ile ya 9 na 10 nadhani zinavunjwa zaidi kuliko mara nyingine ni kwanini?
   
 15. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  ...He he heee..... Mutu ya lojistiks... point lakini (sasa tunaanza kuelewana)
   
 16. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,045
  Likes Received: 23,820
  Trophy Points: 280
  Hakyanani huu ugonjwa umeingia pahala pabaya, pachafu na patamu sana..... Hakuna njia ya kuukabili huu mdude zaidi ya kuepuka ngono zembe. Uaminifu kwa sasa lazima tukubali umeshashindikana. Unaweza kuwa mwaminifu wewe lakini mwenzio asiwe.

  Infidelity, ambayo kwa sasa ni kama sheria lazima ifanyike kwa kinga... Vinginevyo kama nilivyosema. Tutubu na tumrudie Muumba wetu
   
 17. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ni kweli dada angu
  lkn tambua kuwa Mungu aliumba vitu vyote kwa mpangilio ulio mwema, na akatuandalia namna njema ya kuishi kwa utii mbele zake, hebu soma kitabu cha

  Mwanzo 2 : 24, inasema hivi; kwa hiyo mwanaume atamwacha baba na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

  kama utakuwa umeelewa vizuri, hapo ni mme mmoja, na mke mmoja

  sasa tumeyaacha hayo na kufuata akili zetu kibinadamu mwanaume anataka kuwa na wake saba, mwanamke naye anata kuwa waume saba sasa kwa mantiki hiyo sasa ina maana jumla ya ndoa moja ina wanaume 8 na wake 8 na kufanya kuwa na jumla ya watu 16 kwenye ndoa moja, kwa nini kwa sababu tumeacha maagizo ya Mungu nyuma na kufuata akili zetu zaidi
   
 18. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  :fish2:
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Kama kweli wote tungenuia kutafuta solution ya kupunguza maamuki kwa kuachana na cheating na ngono zembe, that could be fine.Corruption is so high in our hearts to the extent that cheating is a distant reality.
  What a sad part of story.....
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,045
  Likes Received: 23,820
  Trophy Points: 280
  Hivi maaskofu wanaupataje huu ugonjwa?
   
Loading...