Ni yupi adui namba Moja wa jamii ya Kimasai

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
664
829
NI YUPI ADUI NAMBA MOJA WA JAMII YA KIMASAI

Moja kati ya mbinu za kivita zilizowahi kuyapa ushindi mataifa mengi wakati wa vita, hapa nazungumzia vita 1 na ya 2 mathalan ni kumjua adui yako.

Theory hii sio tu unaweza kuitumia wakati wa vita, hata kwenye maisha ya kawaida, ukitaka mafaniko kwanza mtambue adui yako kisha chukua hatua.

Hapa namaanisha nini? kumekuwa na sintofahamu kubwa sana inayoendelea nchini ikiendeshwa na presha kubwa katika mitandao ya kijamii kwa kuwatumia watu walio maili zaidi ya 1000 kutapanya habari potofu kuhusu yanayoendelea nchini hapa nazungumzia mpango wa uhifadhi wa eneo la Loliondo na Ngorongoro.

Kundi hili ambalo kiuhalisia limejipa jukumu la kuhakikisha wanaleta social unrest kwenye maeneo hayo, linapewa ushirikiano na makundi mengine yaliyopo hapa nchini na hata wa nchi fulani jirani yenye interest na eneo la Loliondo.

Twende pamoja hapa! awali nilitambulisha falsafa ya kumtambua adui kwanza kabla hujaingia kwenye vita yoyote, hapa nitaanza kuchambua pande mbili tofauti ili mwisho wa siku tuisaidie jamii ya kitanzania kutambua ‘ADUI NAMBA MOJA WA MAASAI NI NANI’

Katika hoja ya kwanza nitaanza kuchambua hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyoitoa leo bungeni kuhusu PORI TENGEFU LA LOLIONDO pamoja na eneo la NGORONGORO.

Katika hotuba ya Waziri Mkuu alisema kwamba

1:Lengo la kuweka alama kwenye pori tengefu ni kuhakikisha eneo lile linalindwa na kuhifadhiwa na akasisitiza ulinzi wa eneo hili ni wa pamoja baina ya Serikali naWakazi wa vijiji 14. hili la kuweka alama za mipaka sio TanzNia tu au Loliondo ni utaratibu wa kawaida sana kuonesha demarcations iweje huku jambo liwe na vurugu

2: Uwekaji wa Alama hizi wala hauna husiano kabisa na kwa namna yoyote ile na uondoaji wa wakazi wa vijiji hivi 14, hapa pia akasisitiza kuwa wanachi wa vijiji hivyo waendelee na shughuli zao za kimaendeleo. Jambo lingine la msingi alilolisema hapa ni kuwa eneo linalowekwa alama lipo umbali wa takribani kilomita 8 kutoka kijijini.

3: Kubwa na la msingi hapa ni pia ni hili, pamoja na Serikali kuamua kuweka mipaka ya kulilinda eneo hili, wataalam wa Wizara za Mifugo na Maji wapo site, kikubwa kinachofanyika hapa ni kuchimba visima vya maji pamoja na ujengaji wa mabakuli ya kunyweshea mifugo na majosho.

NB: Eneo la pori tengefu la Loliondo ni chanzo cha maji na malisho ya wanyama kwenye ushoroba huo. Vilevile eneo hilo linalinda ikolojia ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti na ni chanzo muhimu cha maji cha mto Mara.

Tutoke hapa, hebu tuangalie namna Serikali ilivyolibeba lile suala la Ngorongoro ambalo ni moja ya tukio linalojumuishwa kwenye matukio haya yanayowahusisha wamasai.

Hapa tuanze na kuangalia uhamaji wa wakazi wa ngorongoro kwenda Msomera.

Leo wakati PM anawasilisha taarifa alisema kuwa tayari kaya 293 zenye watu 1,497 zimeshajiandikisha kwa ajili ya kuhama kwa hiari kutoka hifadhi ya Ngorongoro na kuhamia katika kijiji cha Msomera, Handeni, Tanga ili kupisha uhifadhi wa Hifadhi ya Ngorongoro.

Pamoja na haya PM alionesha namna wanavyojenga miundombinu hapa alitaja ujenzi wa visima, shule, hospitali, majosho, mabakuli ya kunyweshea mifugo, utoaji wa mashamba na maeneo tena na hati kbs ambazo zinaweza hata kuombea mikopo, hapa pia zinatekelezwa huduma nyingine za kijamii tena haya yote yanafanyika kwa gharama za Serikali, na hawa waliokubali kuhama naskia upo mpango wa kuwapa kifuta jasho (Patamu hapa)

Kwa kifupi wakati jitihada hizi zinafanyika lipo kundi lililojipa kazi ya kushinda kwenye mitandao ya kijamii na mengine kwenda kwenye maeneo ya maficho huko Loliondo na pengine Ngorongoro kukusanya vikundi vichache vya unidentified so called LOLIONDO MAASAI DWELLERS na kuhamaisha vurugu.

Kundi hili linashinikiza wamasai wasikubali kupisha uwekaji wa alama bila kujali uhifadhi wa pori tengefu la Loliondo, kundi hili limekuwa likiandika haya kwa kutumia lugha ya kingereza hapa lengo lipo wazi ni kwamba wanafikisha ujumbe kwa watu waliowatuma kutekeleza haya.

Pia hoja ya kuliua pori hili tengefu la Loliondo huwezi kulikwepa, hapa wasiwasi wa jirani kutaka kunufaika na uharibifu wa eneo hili huwezi puuza! hapa lazima tuwe makini.

Kwa lililofanyika leo la kusambaza picha nyingine za matukio ya miaka ya nyuma pamoja na picha za majeraha ambayo kwa uhalisia inaonekana ni majeraha ya silaha za jadi kama marungu na mishake na si risasi kama wanavyodai wenye kupokea ‘MTEE’ tena kwa pesa za JOE BIDEN 😀😀

Hapa ndugu zetu wamasai lazima wajiulize , hawa wanaowashinikiza kufanya haya wengi wapo Ulaya na wengine wapo kwenye majumba ya kifahari wamekaa kwenye viyoyozi huku Hennessy ipo pembeni, kashika 13 pro max anatweet, anaspace na kuCLUBHOUSE akisubiri malipo tena kwa yanayokipwa kwa pesa za kigeni yaani za JOE BIDEN yasomeke.

Hawa wanaowashinikiza wasihame kwenda kutumia fursa kule Msomera wao wapo mjini wanachagua kiwanja cha kwenda kutumia pesa walizovuna kutoka kwenye kampeni ya kuhamasisha vurugu..

Kwa leo tuishie hapa, na baada ya hapa tujiulize ADUI YA MASAI NI YUPI? huyu anayejenga miundombinu na kutengeneza mazingira safi ya kisasa ya kuishi au huyu anayehamaisha vurugu yeye akiwa Ulaya na wengine kwenye majiji na kushinda mtandaoni kuchochea uvunjaji wa sheria.

Wasalaam

Mussa Mtike
Mzalendo Halisi
 
Huwa nikiona mtu anajiita Mzalendo huwa nampuuza hata kama ameandika vitu vya maana na kimantiki.

Mtu mwenye upendo na roho nzuri hana sababu ya kujiandika hivyo, matendo yake yatamtambulisha.

Kuna jitu linatoka ukoo wa Ngedele tena liuwaji na limejaa roho mbaya na lenyewe lilijiita Mzalendo.

Nachukia sana ninapoona mtu anajiita Mzalendo hizi ni lugha za watu malaghai, Bongo Zozo mzungu ni mzalendo kuliko nyinyi watu wa fursa.
 
Adui namba moja ni vijana wa kimasai waliosomeshwa na NGO za kenya wanaodanganya baba zao na kutweet "ngorongoro ni ardhi ya masai"
 
Adui wa raia wa Tanzania kwa ujumla wake sio masai pekee ni CCM. Kumbukeni waliyowatenda watu wa Mtwara kwenye gas na korosho! Watu walikimbilia hadi Msumbiji kujificha.
Huyo Majaliwa mwenyewe aliambiwa shangazi zake watavunjwa viuno.
 
Adui wa Loliondo sio CCM, kuna kikundi cha wachache ndani ya CCM ndio adui wao, ndio maana kila wakishika hatamu kelele za Loliondo zinaanza tofauti na wengine wakishika hatamu.
 
Umeandika vingi ambavyo vinaweza kumake sense. Ila swali langu ni moja, Biden anapotoa pesa za kufadhili vurugu ananufaika vipi?

Kwa mimi navyoona ni kama wapinzani ndio wanaochochea vurugu kwa kuwapa sumu wa masai na kuwachochea kua ni eneo lao, na naamini wanafanya ivyo kwa sababu zao za kisiasa kama walivyogo. Sasa wewe unapokuja na habari za Biden inabidi utuambie Biden anafanya hivyo kwa sababu gani
 
Back
Top Bottom