Ni wimbo gani unaokuboa?

Napenda kuwasalimu wana jf ASALAAM ALEYKUM na wengine BWANA YESU APEWE SIFA. Kwa upande wangu wimbo ambao kila ninapousikia unaniharibia siku ni wimbo wa Bony Mwaitege unaokwenda kwa jina "njoo ufanyiwe maombi" na sababu kubwa ni kwamba unahamasisha watu kuamini juu ya binadamu wenzao kuponya kimiujiza. Swali la kujiuliza kama wanaombea, ili yule anayeombewa apone anatakiwa awe na imani, sasa kama anaimani na MUNGU ndo yuleyule kwa nini wasihamasishe watu kuomba wao wenyewe ili waponywe? Maana mungu anasema ombeni lolote kwa jina langu(YESU) nanyi mtapata. Handsome wa mama nawasilisha kama ifuatavyo.
unaonichukiza ni wataifa, tanzania tanzania,viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza,kulinda maliasili na kuwatetea wananchi ameshindwa kuufanya wimbo uwe hai,ndo mana siupendi
 
Nimeishi uswahilini na ndiko naishi hivi sasa, lakini huyu jamaa sijamkubali japo watu wengi wa uswazi wanampenda!
Anazingua sana huyu jamaa,kama ule wimbo wake wa Ugali,huyu jamaa inawezekana ana kizizi cha kupendwa. Nalog off
 
bila kusahau siwapendi wanamuziki wote wa USA.UK.ZAIRE,KENYA,UGANDA,RSA,yaani wanamuziki wote wa nje. Nalog off
 
1. '' Kilimo kwanza''
2.''Uchumi wetu unapaa''
3. ''Tusiichezee amani yetu''
4. ''Tumethubutu tumeweza sasa tunasonga mbele''
Nyimbo zote hizi zimeimbwa na msanii JK.
 
Nyimbo zote za prof J, rais wa masharobaro(oyoyo), tilalila wa mr.blu, nyimbo zote za dudu baya, flora mbasha, uko juu wa lady jay d, zote za miaka50 ya uhuru.
 
Mie hata sizijui majina ila nyimbo zilizoimbwa kwa kubana pua.

Kuna wimbo wa Mpoki unanikera sana.
 
Nyimbo zote za soro mmoja anayeitwa rais wa masharobaro, nyimbo zote za taarabu, nyimbo zote za diamond, blu, bongo fleva kwa ujumla..nying znapotosha kuhusu maadili na utamaduni wa m2 mweusi...
 
Back
Top Bottom