Ni wimbo gani unaokuboa?

Single mbili za Rahisi Jk ziitwazo hotuba kwa wazee wa Dar kuanzia ile ya kwanza na hii remix ya leo
 
Msiompenda JD mna wivu,lakini hata mm cmpend ni nyimbo moja 2 aliyoimba na Blue at least bt all in all Cmpend
 
1. Unanijuaaaa! Unanifahamu?!!!
2. Kuna taarabu mpya ya MwanaFA na Lina inaitwa-Yalaiti! Clouds wanaipiga sana mpaka nimefunga redio hii kwa miezi kadhaa kwanza.
 
Nyimbo zote wa bana pua na wapaka karolaiti wa kibongo. Upuuzi mtupu.
 
kweli hawa waimaji wa ijili walio wengi wamedivert kutoka kwenye uimbaji wa kiroho na kuingia kwenye biashara zaidi. Na wanatumia 'uelewa' wetu kuvuna kinachowezekana na naweza kukuhakikishia kuwa nyimbo nyingi hutaweza kuzisikiliza miaka 15 ijayo tofauti na nyimbo za zamani kama Nkinga Choir, Ulyankuru, Makongoro, Tumaini na nyinginezo zilizokuwa zikirekodiwa na Radio Habari Maalumu.
Hasa huyu Bonny Mwaitege ukiangalia na hata kusikiliza nyimbo zake zinatumia falsafa za kidunia zaidi badala ya kiroho.
Napenda kuwasalimu wana jf ASALAAM ALEYKUM na wengine BWANA YESU APEWE SIFA. Kwa upande wangu wimbo ambao kila ninapousikia unaniharibia siku ni wimbo wa Bony Mwaitege unaokwenda kwa jina "njoo ufanyiwe maombi" na sababu kubwa ni kwamba unahamasisha watu kuamini juu ya binadamu wenzao kuponya kimiujiza. Swali la kujiuliza kama wanaombea, ili yule anayeombewa apone anatakiwa awe na imani, sasa kama anaimani na MUNGU ndo yuleyule kwa nini wasihamasishe watu kuomba wao wenyewe ili waponywe? Maana mungu anasema ombeni lolote kwa jina langu(YESU) nanyi mtapata. Handsome wa mama nawasilisha kama ifuatavyo.
 
Back
Top Bottom