Dumuzii
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 3,601
- 8,707
We unahisi kwa nini kakwambia uwapigie wazazi wake simu utoe ushuhuda wa ujinga ulio ufanya......?Kama mada inavyojieleza
Yapata wiki sasa nimesusiwa chumba nalala peke angu na nimenuniwa kabisa na mke wangu.
Ni hivi naishi na mke mbalimbali yani mikoa tofauti. Alikuja hapa maskani ila kuna kamgogoro kadogo kalitokea asubuhi yake nikagundua kosa langu nikamwomba samahani mke wangu lakini kilichotokea ni yeye kuhama chumba analala na watoto na ameninunia
Anaongea na wapangaji wangu eti ili yaishe niwapigie simu wazazi wake niwaombe samahani. Sasa najiuliza tugombane sie samahani nimwombe mamake katu siwezi kufanya huo ujinga
Kila unapotokea mkwaruzano mke anawahi kusema tuachane bora aishi msimbe na kuwa mdangaji
Sasa naona awamu hii kaamua kweli awe msimbe na mdangaji. Nimejaribu kutafuta suluhu naona mwenzangu kaamua kukaza
Basi nami nimeona niendelee na mishe zangu sibembelezi tena.
Ndoa zinachangamoto sana hasa ukiwa na mke mbishi mjuaji asietaka kukubali yaishe.
Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
Kifupi huyo mwanamke yupo kwako kwa sababu ya shinikizo la wazazi wake so anataka uwaambie wazazi wake ili apate sababu ya kukuacha
Na kukutoa tu wasiwasi huyo mwanamke alisha kuacha kitambo tu hivyo anatafuta sababu ya kuwaambia wazazi wake