Ni wapi wewnye mapenzi ya dhati jamani

BUMIJA

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
5,818
11,000
Wanawake wasomi na ambao ni wa kawaida yani walioishia la saba tu,na ukilinganisha na wenye elimu za juu,ni wpi weny mapenzi ya dhati na waaminifu zaidi
 
Kuwa au kutokuwa na mapenzi ya dhati ni suala la mtu mwenyewe, wala halihusiani na kiwango cha elimu alichonacho!! IMO.......mtu aweza jifunza/kuiga mambo mbalimbali ktk mapenzi (ambayo yanaweza kujenga au kubomoa) kutokana na sehemu anazokwenda au watu anaokutana nao (iwe ni shule, safarini, au makazi mapya)......... regardless his/her level of education lakini SIO REALLY LOVE!!!
 
Darasa la saba wanaburuzwa sana na wanaume kwa vile hawajui kiukamilifu haki zao. Halafu kukosa elimu ya kutosha kumewafanya wawe tegemezi sana kwa wanaume. Sasa utasema hayo ni mapenzi ya dhati au uaminifu. Wanakumbatia penzi ili maisha yaende na mara nyingi wanafake.
 
unanikumbusha jamaa mmoja aliwahi kuniambia, baada ya kutendwa na warembo wengi (maana yeye alikuwa anago after the most beautiful ones) ameamua kususa, na akaamua kutafuta dada mmoja mbayaaa kinoma alafu akaamua kumpenda kupita maelezo.
hata hiyo haikumsaidia.
therefore this proves that mapenzi hayana formula mwaya.
 
Elim ya mtu siyo kithibitisho cha mapenzi ya dhati bali tabia ya mtu tu
 
Ukitaka mke wa kumbuluza asiye na maamuzi, kumkanya mtot akikosa mpaka "Ngoja baba arudi". Asiyeweza kuchangia chochote kwa maendeleo ya familia. Acha woga wa maisha ndg. wewe drs la 7, ukioa prof hakuna taabu
 
mapenzi hayana formula,na kupenda kuna anzia kwako wewe mwenyewe. Na siku zote mapenzi kati ya watu 2. Na uwezi ukasema kuwa mapenzi yanaendana na kiwango cha elimu ambacho mtu anacho. Kwa sababu elimu uliyonayo haiwezi kukuwezesha kumpenda mtu kwa dhati au kutompenda mtu kwa dhati. Unaweza ukawa na mpenzi ambaye elimu yake ni darasa la saba na akakupa mapenzi ya dhati kuliko hata yule mwenye elimu ya PHD.
 
Elimu haina uhusiano na mapenzi ya dhati...Mappenzi ya dhati yanatokana na hofu ya Mungu, kiasi cha upendo alichonacho umpendaye kwako, jinsi unavyompenda huyo uliyeko nae na wakati mwingine malezi aliyolelewa. Kuna wenye degree wenye mapenzi ya dhati na wasiokuwa nayo na kuna wenye elimu ya msingi wenye mapenzi ya dhati na wasiokuwa nao...:juggle:
 
Aweza kuwa hajasoma lakini hana mapenzi ya kweli, so far siku hizi hakuna mapenzi ya kweli bali kuna mapenzi ya kutamaniana ya kweli. Pesa ndo inatamanisha uwepo wa mapenzi hayo.
 
mapnz ya that hayana uhusiano na kiwango cha elimu,ni swala la mtu binafsi na mhusika anaweza acwe na mapnz kwako akampenda mwingine and virse versa.
 
Back
Top Bottom