Ni wakati wa Kanisa Katoliki kusimama na kukemea,Askofu Shoo ameonesha njia.Waumini wana manung'uniko

Halafu kuna watu hudhani Cardinal Pengo ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania
Yeah, baadhi hudhani hivyo kama ilivyo KKKT; kwamba Askofu Mkuu wa KKKT ndiye boss wa wote. Hierarchy ya viongozi wa kiroho wa Roman Catholic, iko complex kidogo.
 
Yeah, baadhi hudhani hivyo kama ilivyo KKKT; kwamba Askofu Mkuu wa KKKT ndiye boss wa wote. Hierarchy ya viongozi wa kiroho wa Roman Catholic, iko complex kidogo.

Na hiyo complexity ndiyo inalifanya liwe taasisi imara.

Mfano, watu wengi hawajui nafasi Askofu Ruwaichi wa Jimbo Kuu la DSM. Ruwaichi ni Askofu Mwandamizi, Pengo ni Askofu, Nzigirwa ni Askofu Msaidizi.

Ila kimamlaka, Ruwaichi ndiye Mkubwa, maana yeye yupo pale kuchukua madaraka baada ya Pengo kustaafu. Nzigirwa anabakia kuwa msaidizi.

Maaskofu wote wanateuliwa na Papa wawe Jimbo Kuu au Jimbo. Na hawapigiwi kura!
 
Katoliki sio kama vikanisa vya uchochoroni mnavyojua, sisi huwa haturopoki ropoki kwenye minor ishuz.

Kumbukeni katoliki ndilo kanisa lenye ujasusu wa hali ya juu sanaa duniani.

Kupitia majasusi wake waliotapakaa kuanzia kwenye ngazi za jumuiya huwa wanakusanya taarifa na kuchambuliwa kwa undani zaidi na mwisho wa siku wanafanya tathimini juu ya ishu kama ina mantiki au ina interest kwao na taifa,

Ndio maana huwa hawaropoki ropoki kwani wana baseline nzuri ya taarifa .
 
Askofu Shoo namuelewa sana yule Mzee ni mtu mwenye busara sana na hapendi Watanzania wote wasumbuliwe bila kuwabagua kwa dini zao au makabila...
 
Tatizo askofu shoo ana elements za UPINZANI ndo wasiwasi unaanzia hapo
Hahah according to your logic. Anaesema ukweli = mpinzani.
Sijaona element zozote unless labda huwa huendi kanisani kila jpili.. au sio mkristo.
Kila jpili tunakanywa na kuonywa tuache dhambi.. maovu. Ni utaratib wa kanisa
Sasa cha ajab hapo ni kipi?
 
Mawazo yapo yako sahihi na yanaheshimika.Lakin na wewe kuna mahali unajichanganya.Unadhani Katoliki,KKkT,Anglican ndio makanisa makini yenye uwezo wa kukemea na nchi ikasimama lakin haupo sahihi.kwa sababu kanisa lote lina nguvu na linatumia approach tofautitofauti katika kuwaonya hawa watu,lakin mfano mtu kama Makonda na Magufuli,Happy,na wengineo wana kiburi cha uzima.Hao hata akishuka Mussa na manabii wengine hawawezi kushuka na kubadili kujiona wao wako juu.

Ukimchunguza Makonda ni mtu mnyenyekevu kwa baadhi ya watu hasa wa dini anaowaogopa yeye(pretender)lakin kwa wengine kama akina shoo na katoliki Makonda hawezi kuwaheshimu.Makonda anaheshimu wachungaji wa Kilokole na waislamu tu.wengineo anawaona kama wako wrong katika dini yao hivyo hawawezi kumfundisha kitu kwa kuwa hawapo nae katika imani moja.Lakin akija kwenye madhehebu yake mfano EAGT,FPCT,FGBF,TAG na mengineyo anawaheshimu na wakimwambia kitu anawaelewa vizuri na hawezi hata kubisha.Ila hawa kinga shoo na Munga anachukulia kama watu tu wa kawaida.

kuwafanya watu kama hawa wakawa na adabu ni kuwaambia ukweli wa waziwazi na hadharani ili nao wajione zi kitu unawaonesha kuwa kiburi chao zi kitu na kwa kuwa ukweli unashinda ubaya basi lazima mambo yawe shwarii kwako.Ila ujiandae kwa figisu na mishale ila usipoyumba wanashuka.
 
askofu shoo alipaswa kuwaita faragha na kuwapatanisha...huwezi patanisha km hujawapa muda wa kujadili wakiwa huru...huo ni ukandamizaji katika maamuzi na si kwa askofu tu ni kwa sisi watanzania kuanzia makanisani hadi majumbani hatutoi uhuru wa majadiliano.ungamo la kweli ni la rohoni si kwa ajili ya watu.
pia inakera zaidi kwa pande zote kuchukulia misiba km sehem za kutoa dukuduku lao,wafiwa wanataka faraja sio kuwafikirisha mambo mengine
 
Je anao uwezo wa kumsema Kiongozi wakiwa wanaonana USO KWA USO?

Hapo ndipo hoja yangu imejikita.
Unateswa na mahaba - fuatilia vizuri yupo Askofu wa Jimbo la Ngara NIWEMUGIZI (Mzaliwa wa Rukoto Biharamulo - karibu kidogo na Seminari ya Katoke)
 
Huyo askofu roho ilimuuma toka aone vijna wake wa kaskazini wamekosa utawala wa nchi nae kaamua kuwa mpinzani mazima
 
Na hiyo complexity ndiyo inalifanya liwe taasisi imara.

Mfano, watu wengi hawajui nafasi Askofu Ruwaichi wa Jimbo Kuu la DSM. Ruwaichi ni Askofu Mwandamizi, Pengo ni Askofu, Nzigirwa ni Askofu Msaidizi.

Ila kimamlaka, Ruwaichi ndiye Mkubwa, maana yeye yupo pale kuchukua madaraka baada ya Pengo kustaafu. Nzigirwa anabakia kuwa msaidizi.

Maaskofu wote wanateuliwa na Papa wawe Jimbo Kuu au Jimbo. Na hawapigiwi kura!

Pengo ndio Mkuu wa Jimbo kuu la DSM mpaka pale atakapo staafu ama kwa hiari (Miaka 75) au kwa shuruti (Miaka 80) au akifa!
Nzigilwa ndio the second in command sio kwa sababu ya kuwa Askofu Msaidizi ila kwa sbb pia ni Vicar General(Makamu Askofu) Kuna tofauti kubwa sana kati ya Askofu Msaidizi na Makamu Askofu! Makamu Askofu sio lazima awe Askofu Msaidizi. Jimboni DSM Mwadhama Rugambwa hakuwa na Askofu Msaidizi ila alikuwa na Makamu Askofu. Angalia vema sio Makamu wa Askofu….Ni Makamu Askofu kwa lugha yao ni Vicar Generalis.

Ruwaichi ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki. Katika jimbo Kuu la DSM mpaka sasa hana mamlaka yoyote. Hadhi yake ndio hiyo Askofu Mkuu Mwandamizi…….Hadhi yake ni kusubiri tu siku Pengo ana staafu au anaondolewa au anakufa! Likitokea mojawapo kati ya hayo dakika hiyo hiyo anachukua mamlaka yote aliyokuwa nayoPengo ndani ya DSM.....hatosubiri tena kupewa au kuambiwa na mtu…….. Huyu ni mtu anayesubiri! Ruwaichi akichukua madaraka ni juu yake abaki na Askofu Msaidizi au la? Na abaki nae vipi kama askofu msaidizi au kama askofu msaidizi na makamu askofu!!!!!

Kumbuka Pengo alimwondoa Kilaini kama Askofu Msaidizi na Makamu Askofu!

Pengo naye aliletwa DSM 1990 kwa hadhi kamaya Ruwaichi akasubiri mpaka Rugambwa alipostafu 1992 akajitwika madaraka.
 
Kwanza ndugu zangu wa JF naomba niwasalimu wote.

Pili naomba niseme ukweli wangu kutoka moyoni ya kuwa Leo katika Ibada ya Mazishi ya DR. MENGI, nimefurahishwa sana na kile alichosema ASKOFU DR. SHOO. Sababu kubwa ni hizi;

i.Amesema ukweli bila kuogopa kama muhusika yupo au la.

ii.Amewasemea wanyonge na wenye hofu ya kusema ukweli.

iii.Ametoa ushauri bila kuogopa wenye mamlaka kama wapo au la.

iv.n.k

Binafsi nimejiuliza, "JE KUNA KARDINALI, ASKOFU au PADRI MWENYE UWEZO WA KUVAA JAPO SOKSI TU NA SIYO VIATU VYA ASKOFU DK.SHOO AKIPEWA NAFASI YA KUSEMA NENO MBELE YA VIONGOZI WA SERIKALI?"
kwamba ulitaka iseme RC na siyo KKT?
 
Back
Top Bottom