kelao
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 8,132
- 5,785
Naunga mkono hojaNi wakati mwingine tena kauli ya Kiongozi Mmoja mkubwa wa kanisa la Tanzania imetikisa nchi.Hii ni sauti ambayo ilisubiriwa kwa muda mrefu toka kwa moja wa viongozi wa dini wanaoheshimika Tanzania.Hii ni kwa sababu,licha ya viongozi wa kisiasa kuwa na mamlaka na nguvu za kidola,bado viongozi wa kidini huwa na heshima na uaminifu wa kauli zao toka kwa waumini wao.
Ni bahati mbaya kuwa,tupo katika zama ambazo watawala tulionao wanajiona miungu watu,wanapenda kusifiwa,kutukuzwa na kuabudiwa.Wamejivika umalaika na ukuu usiohojika.Wanapenda kukemea pasipo wao kukemewa,wanapenda kuonya pasipo kuonywa na wanapenda kuwakosoa wenzao mbele kadamnasi ila wao wanapenda wasifiwe hadharani na kutukuzwa wakiwa faragha.
Imekuwa hivyo sehemu nyingi duniani,viongozi waliopo madarakani kuhakikisha kuwa "wanawateka" viongozi wa kidini ili wasikosolewe,wasionywe wala wasikemewe.Hii imeota mizizi pia hapa Tanzania.Watu hawataki kukosolewa,wanataka kusifiwa,hawataki kuonywa wanataka kuabudiwa,hawataki kukemewa wanataka kutukuzwa.
Juzi walipokaribishwa kumsimika kiongozi mkubwa wa dini kule nyanda za juu kusini,waliposifiwa na kuabudiwa,hawakusema kuwa "siasa imeingia kwenye dini",ila wakikosolewa wanasema dini imeingilia siasa.Juzi walikaribishwa pale Mwenge,kwenye kanisa binafsi la mtu,na walipewa nafasi ya kuhubiri kama wachungaji na kutafsiri vifungu vya biblia,hawakusema kuwa wanasiasa wameingilia dini.Askofu mwenye kanisa lake akawasifia na kuwatukuza,hawakusema dini imeingilia siasa.Ila wanapoonywa na kukosolewa,wanang'aka na kupayuka kuwa dini imeingilia siasa.
Siku chache zilizopita,waliamua kutoa ahadi ya kutoa zawadi ya jina la mtaa uitwe kwa heshima ya Kiongozi mmoja wa dini,na hilo kwao haikuwa siasa imeingilia dini.Kiongozi yule kupewa mtaa kwa heshima yake,wengine waliguna,maana walijua ndio mwanzo wa kiongozi mzawadiwa kupoteza uhalali wa kuikosoa serikali na maovu yake,na pia ndio mwisho wa kiongozi kuwatetea waumini wake wanyonge kwa gharama ya zawadi ya jina la mtaa.
Hii inaturudisha nyuma katika maandishi ya kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed".
Wakati wa utawala wa Kifashisti kule Italia,Mussolini aliona tishio la Kanisa Katoliki ktk kufikia malengo yake.Maana kwa wakati ule,kanisa lilikuwa na "kontroo "ya maisha ya kiroho na serikali ilikuwa na "kontroo" ya maisha ya kisiasa.
Alichokifanya Mussolin ni kujipendekeza kwa kanisa na kutoa "rushwa" ili yote atakayoyafanya kanisa katoliki lililokuwa na nguvu sana Italia libaki kimyaa.Alifanikiwa.
Kwanza aliamua kumbatiza mwanae wa kiume,ambaye hapo awali hakuwa amebatizwa.Hapa akaliteka kanisa kwa karata ya kwanza.
Pili aliamua kufunga ndoa ya kikanisa,baada ya kuwa amekaa miaka 11 na ndoa ya "bomani" na mkewe Rachele.Hii ikawa karata ya pili ya kujisogeza na kujiweka karibu na kanisa ili kutimiza malengo yake ya ufashisti.
Karata nyingine;aliamuru kufungwa kwa maduka yote ya vileo(wine shops) na kufuta leseni za sehemu za starehe zote za usiku ili kuendana na kauli ya kanisa ya kupunguza uovu mitaani kwa ulevi na anasa za usiku.Hapa kanisa katoliki likanasa mtegoni.
Alienda mbali mpaka akatangaza kuwa "Public Swearing" kama "Public Crime"...Yaani mwananchi ukiwa mtaani mnabishana,mtu akikwambia sema haki ya Mungu...Ukisema tu "Haki ya Mungu ntayafunga majizi yote,msema kweli ni mpenzi wa Mungu".Basi ujue wewe una kesi ya jinai ya kujibu.Hapa alitaka kulifurahisha kanisa kwa amri ile ya "Usitaje bure jina la bwana Mungu wako"(Kwa hiyo amri hiyo ingekuwa enzi hizi,kuna mtu angekuwa jela zamaniii,maana huwa anajiapiza sana mikutanoni)
Mussolini akaamuru kupigwa marufuku vidonge vya majira na kampeni zote za matumizi ya uzazi wa mpango kama ulivyo msimamo wa kanisa.Wakati huo wa 1920's kanisa lilitaka wanawake wabaki nyumbani ili kulea watoto na kukuza familia vyema.Mussolini akalipigia chapuo hili na kulitungia sheria ili kuwafurahisha wazee wa kanisa.
Akatunga sheria ambayo ilifutilia mbali talaka kwa ndoa hata za bomani.Hii ilikuwa ni njia ya kuungana na kanisa ktk ndoa ya mke mmoja na isiyo na talaka mpaka Mungu awatenganishe.
Ndoano hii ikanasa vizuri kwa kanisa.
Hawakupepesuka wala kutikisika.Mambo yote ya ndoa yakaondolewa serikalini na kubaki kuwa "Full Control of the Catholic Church".Wale wapenda mteremko wa ndoa za bomani wakakosa pa kwenda.
Akatoa 109 acres ktk mji wa Roma ili yajengwe makao makuu ya Papa(Vatican) baada ya kuwa yalipokonywa wakati wa "Unification of Italy" ya miaka ya 1870's,na akaamuru kanisa lilipwe zaidi ya £130 milioni kwa wakati ule.Hii ilikuwa ni ndoano iliyoingia sawasawa kwa kanisa,na kanisa halikusema lolote juu ya "ufashisti" wa Mussolini hadharani;japo liliouona na kuuhisi kwake na kwa waumini wake.
Vatican ikawa nchi ndani ya mji,wakapewa mamlaka juu ya Post Office,jeshi dogo,polisi na "Rail station".Baada ya hapo,ugomvi ukawa ni nani anatakiwa "kukontrol" Elimu?Mussolini alihitaji elimu ili apandikize "ufashist" kwa watoto,na kanisa lilitaka elimu ili kupandikiza "dini" kwa watoto.
Mambo haya yote ambayo baadae,waumini wasio rasharasha waliona ni kama "rushwa" kwa kanisa ili liweze kusifia na kukaa kimya juu ya serikali ya kifashisti ya Mussolin yalifanikiwa.Si ajabu Papa John Paul II alikuja kuiomba jumuiya ya waumini na wasio waumini ktk jubilei ya miaka 2000 ya Ukristo kwa yale yote kanisa iliyoyakosea ktk kukuwa kwake.
Hakukuwa na Kardinali,askofu wala kasisi(padre) aliyeikemea serikali isiyo ya kidemokarasia ya Utawala wa Mussolini.Mengi yalitokea na kanisa lilikaa kimyaaa.Waumini waliteseka,waliumia na walipata machungu ya maisha...Lakini kanisa lilisema hewala,huu ni utawala mzuri tu,maana umerudisha heshima ya Papa katika nchi ya Vatican.
Kama kanisa la wakati huo lilibaki kimya juu ya ufashisti wa Benitho Mussolini,hili la kwetu la Tanzania,lisibaki kimya juu ya malalamiko ya wananchi,kutekwa kwa watu,kupigwa risasi kwa watu na kuongezeka kwa kasi uvunjifu wa haki za binadamu kwa mgongo wa hao wanaoitwa "Watu wasiojulikana".Kanisa la Tanzania lisikae kimya juu ya kauli za kibaguzi na zinazoligawa Taifa.
Hatumaanishi kuwa sasa Tanzania tuna "ufashisti",lakini tunakubaliana kuwa kwa sasa Tanzania maisha ni magumu,pesa imepotea na uchumi umenyambulika na kutikisika.Hii inaweza kuwa ni matokeo ya kipindi cha mpito kuelekea uchumi wa viwanda,lakini haiwezi kuwa sababu ya kutokusema ukweli kuwa "HALI NI NGUMU"
Tuwakumbushe viongozi wa dini wajibu wao,hata wale wanaoamua kunyamazia utekwaji wa watu,pengine ni kwa sababu wamezawadiwa majina ya mitaa.
Tuwakumbushe tu heri shari inayojengeka kutokana na kuali thabiti zinazoonyesha kuwatumikia watu na kuitumikia roho,kuliko kuendekeza uwoga na unafiki kwa manufaa ya zawadi za kimwili na sifa za kuwa karibu na wenye mamlaka.Ndio maana Lugha Mama ya Kanisa ya Kilatini ikasema "Nemo Liber Est Qui Corpori Servit" yaani "No One is Free who is a slave of his body"
Tuitumikie Roho inayodumu milele,kuliko mwili unaooza na kuliwa na nyenyere.
barafu wa JF
Machame,Kilimanjaro.