Kama kuna wakati tulipaswa kukemea Udini basi ni pale Askofu Gwajima na Shekhe Majini walipogombea Ubunge kwa tiketi ya CCM!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,024
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Duniani Dr Gwajima PhD ni Mbunge wa jimbo la Kawe CCM

Sheikh Majini yeye aligombea kule Handeni Tanga lakini alifeli Kwenye kura za Maoni

Kumbukumbu zangu zinanikumbusha Mbunge mh Mwamasika wa Iringa alijiuzulu Ubunge alipochaguliwa kuwa Askofu wa KKKT Dodoma Ili asichanganye Dini na Siasa

Wakati mchungaji Rwakatare alipoteuliwa kuwa mbunge wa vitu maalumu CCM aliyekuwa Askofu mkuu wa TAG Prof Rainwell Mwenisongole alimtaka kuacha mambo yote ya Uongozi wa Kanisa Ili asichanganye Dini na Siasa lakini Rwakatare alikataa na kusema Kanisa lake siyo Tanzania Assembly of God bali ni Mikocheni Assembly of God

Hivyo kumsemasema Askofu Mwamakula ilhali kuna mbunge Askofu siyo sahihi

Mungu wa mbinguni awabariki!
 
Viongozi wa dini wakiacha dini wakaenda kwenye siasa hakuna shida...
Shida wanapokuwa kotekote...na hawa maaskofu wa chadema kuvaa majoho Hadi majukwaani na press conferences...hii ni shida ...
Kama wanataka waache dini waingie moja Kwa moja Chadema wagombee nafasi za siasa
 
Askofu Gwajima kila Jumapili anaongoza Ibada Kanisani kwake Ubungo na mambo yanakwenda hakunaga mbambamba wala nini!
 
Viongozi wa dini wakiacha dini wakaenda kwenye siasa hakuna shida...
Shida wanapokuwa kotekote...na hawa maaskofu wa chadema kuvaa majoho Hadi majukwaani na press conferences...hii ni shida ...
Kama wanataka waache dini waingie moja Kwa moja Chadema wagombee nafasi za siasa
Kwa hiyo Masheikh wao wavae kanzu na baraghashia kwenye press zao, huku wakitekenya tasbihi ni sawa.

Ila kwa Wakristo, Maaskofu wakivaa unayoyaita joho (bila adabu)ni kosa, unafikiria kwa kutumia makalio?

Kuvaa tu ni ishara kwamba wao wanatimiza majukumu yao kama viongozi wa dini. Kusali kabla na baada ya mkutano, kuikumbusha jamii namna ya kuenenda katika njia impendezayo Mungu, nk.

Wala siyo siasa. Ila kwa kuwa mmejaa hofu na kugadhibika, basi mnatafisiri kama siasa.

Huo ni upunguani.
 
Askofu Mwamakula na Bagonza wavue majoho ya uaskofu na kuingia kwenye siasa mazima. Kuwa kotekote ni unafiki. Askofu Mwamakula ukimbana anakimbilia kusema yeye ni mtumishi wa Mungu badala ya kusema yeye ni mtumishi wa Mbowe.
 
Viongozi wa dini wakiacha dini wakaenda kwenye siasa hakuna shida...
Shida wanapokuwa kotekote...na hawa maaskofu wa chadema kuvaa majoho Hadi majukwaani na press conferences...hii ni shida ...
Kama wanataka waache dini waingie moja Kwa moja Chadema wagombee nafasi za siasa
Mbona sijaona ukimzungumzia mwenzenu Gwajima ambaye ni kiongozi mkuu wa kidini pia ni mbunge wa CCM?, yeye amechanganya nini?
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Duniani Dr Gwajima PhD ni Mbunge wa jimbo la Kawe CCM

Sheikh Majini yeye aligombea kule Handeni Tanga lakini alifeli Kwenye kura za Maoni

Kumbukumbu zangu zinanikumbusha Mbunge mh Mwamasika wa Iringa alijiuzulu Ubunge alipochaguliwa kuwa Askofu wa KKKT Dodoma Ili asichanganye Dini na Siasa

Wakati mchungaji Rwakatare alipoteuliwa kuwa mbunge wa vitu maalumu CCM aliyekuwa Askofu mkuu wa TAG Prof Rainwell Mwenisongole alimtaka kuacha mambo yote ya Uongozi wa Kanisa Ili asichanganye Dini na Siasa lakini Rwakatare alikataa na kusema Kanisa lake siyo Tanzania Assembly of God bali ni Mikocheni Assembly of God

Hivyo kumsemasema Askofu Mwamakula ilhali kuna mbunge Askofu siyo sahihi

Mungu wa mbinguni awabariki!
ccm ni chama cha kipuuzi sana. wanapozidiwa kwa hoja wao huingiza vihoja vya udini na ujinga mwingine. jibuni hoja acheni kuweweseka, kwani viongozi wa dini siyo watanzania?
nakumbuka hata mwaka 1994 ccm wallikuwa wakiweka picha za mauaji ya kimbari ya RWANDA na BURUNDI kila baada ya taarifa ya habari wakiwatisha watanzania kwamba wakiwachagua wapinzani ati pangetokea mauaji kama yale ya RANDA NA BURUNDI.
fikiria wangefanya wapinzani kingetokea ninini?
 
Kukataza mtu kugombea chochote sababu ya Imani zake ni Upuuzi na Ubaguzi..., Lakini mtu huyo kuleta Imani zake au kufanya kazi zake kulingana na Imani yake na sio Sheria na Katiba ya Nchi ni Upuuzi zaidi ambao unahitaji kukemewa...

Serikali haina Dini; wewe, wao na wenzenu Imani zenu ziacheni huko Mehakaluni, Makanisani na Misikitini; Tukikutana kitaa sihataji kujua Imani yako zaidi ya kuwa wewe ni Binadamu mwenzangu (hayo mengine yote ni ya kwako na kwa faida yako)
 
Viongozi wa dini wakiacha dini wakaenda kwenye siasa hakuna shida...
Shida wanapokuwa kotekote...na hawa maaskofu wa chadema kuvaa majoho Hadi majukwaani na press conferences...hii ni shida ...
Kama wanataka waache dini waingie moja Kwa moja Chadema wagombee nafasi za siasa
Dini na siasa unazitenga vipi? Viongozi wa dini kazi yao kukemea maovu, Yohana mbatizaji alimkemea mtawala kwa kupora mke wa ndugu yake, akakatwa kichwa, Yesu alimkemea maovu ya watawala akabambikiwa kesi iliyopelekea kusulubiwa msalabani. Maaskofu wanakemea uovu wa mkataba mnasema wanachanganya dini na siasa? Dini na siasa unazitenga vipi?
 
Askofu Mwamakula na Bagonza wavue majoho ya uaskofu na kuingia kwenye siasa mazima. Kuwa kotekote ni unafiki. Askofu Mwamakula ukimbana anakimbilia kusema yeye ni mtumishi wa Mungu badala ya kusema yeye ni mtumishi wa Mbowe.
Dini na siasa huwezi kuzitenga, viongozi wa dini kazi yao kukemea maovu, wameona ubovu wa mkataba waacheni wakemee.
 
Viongozi wa dini wakiacha dini wakaenda kwenye siasa hakuna shida...
Shida wanapokuwa kotekote...na hawa maaskofu wa chadema kuvaa majoho Hadi majukwaani na press conferences...hii ni shida ...
Kama wanataka waache dini waingie moja Kwa moja Chadema wagombee nafasi za siasa
Maaskofu wa Chadema ni wakina nani hao? Wataje utupe na namba za kadi zao.

Hao maaskofu wakati ule wakimponda Magufuli hukufungua mdomo wako, leo wanakemea uhuni wa kutolewa bure bandari zetu kwa waarabu ndio unawaona wa Chadema?

Unatembea kwenye hoja za kijinga muda mwingi mpaka unajizoea kwa ujinga wako, hivi hujihurumii wewe mzee?
 
Wakemee wakiwa makanisani sio kwenye majukwaa ya kisiasa.
Viongozi wa dini wakemee uovu hadharani ili viongozi mafisadi wajitambue. Yohana mbatizaji alimkemea mtawala kwa kupora mke wa ndugu yake akakatwa kichwa, Yesu alikemea maovu hadharani kweupe akabambikiwa kesi iliyopelekea kusulubiwa msalabani. Siasa na dini huwezi kuzitenga, viongozi wa dini wakemee uovu hadharani.
 
Back
Top Bottom