Ni Wakati Sasa wa Kushughulikia "Majipu Halisi!"

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,192
1,971
Wakati Dr Magufuli akifanya kazi muhimu sana ya "utumbuaji majipu" ni maoni yangu kwamba akajikita kwenye "Majipu Halisi" kwa sasa!

"Majipu Halisi" ni Wanasiasa ambao wametufikisha hapa tulipo! Wanasiasa ndio hasa wanaopanga mikakati na utekelezaji wake!

Nchi kunuka rushwa, ukwepaji kodi, umaskini, nk ni mazao ya Wanasiasa! Watendaji ni watu wa kufuata upepo wa Wanasiasa!

Haya Dr Magu mulika ndani ya Chama chako kuna "majipu" ya kufa mtu huko!
 
Huyo hana lolote ameishia kuonea vidagaa tu huku akiacha mapapa nani hajui chanzo cha hayo ni wanasiasa anaogopa kuwagusa. sifa tu hana lolote.
 
Wakati Dr Magufuli akifanya kazi muhimu sana ya "utumbuaji majipu" ni maoni yangu kwamba akajikita kwenye "Majipu Halisi" kwa sasa!

"Majipu Halisi" ni Wanasiasa ambao wametufikisha hapa tulipo! Wanasiasa ndio hasa wanaopanga mikakati na utekelezaji wake!

Nchi kunuka rushwa, ukwepaji kodi, umaskini, nk ni mazao ya Wanasiasa! Watendaji ni watu wa kufuata upepo wa Wanasiasa!

Haya Dr Magu mulika ndani ya Chama chako kuna "majipu" ya kufa mtu huko!

Ngoja nikuulize ungekuwa wewe mtu akikuambia vaa chupi kichwani utavaa? maana wakati mwingine tunawaonea wanasiasa. kama mtu amekuambia pitisha contena bila kupokea ushuru yaani kodi ya serikali ukakubali wewe ndio mjinga.Hata kama kuna wanasias walio husika unadhani huu ndio ideal time?saikolojia inakataa.
 
ccm ni ile ile ooo ni ile ileeee x2

rudia mara nyingi kadri uwezavyo ili usiumize kichwa kuwaza majipu
 
Ngoja nikuulize ungekuwa wewe mtu akikuambia vaa chupi kichwani utavaa? maana wakati mwingine tunawaonea wanasiasa. kama mtu amekuambia pitisha contena bila kupokea ushuru yaani kodi ya serikali ukakubali wewe ndio mjinga.Hata kama kuna wanasias walio husika unadhani huu ndio ideal time?saikolojia inakataa.

Kwa mfano wewe umeniteua nikae pale Bandari na wewe ndo boss ukanipa maelekezo kwanini nisiyafuate.
 
Naona kwenye chama chake betri za tochi anayotumiaga kumulika wizara zingine na taasisi zingine zimefifia nwanga hauonekani
 
Just the matter of time. Watu watafungwa na kufilisiwa sana wakti huu kuliko wakati wowote ule.
 
ANBEN, TEMBO DENTIST, SIMBA TRUST, EPA, ESCROW, NET GROUP, DEEP GREEN, TANGOLAD, MEREMETA, RICHMOND, UDA, TICKS, TRL, TPA, TPDC, TRA, ATC, TANAPA, DISTRICT & MUNICIPAL COUNCILS, Yoote hayo majipu. Yameiva kwa viwango mbalimbali.
 
Back
Top Bottom