Ni wakati sahihi CHADEMA Kujitafakari!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Ninasema hivyo kutokana na mtazamo wangu binafsi.siwakilishi chama chochote cha kisiasa nchini.

Mbinu za ufanyaji siasa za chadema kwa sasa zimepitwa na wakati au zimechokwa!

Ninaposema hivyo nina maanisha kwamba ...wananchi wanahitaji tofauti.
Wakati Chadema pia mnalo hitaji lenu tofauti.

Jaribuni kukaa na kupata watunga sera mahiri ili wawasaidie kutunga sera zinazowagusa wananchi kwa 100%.

Badala ya Sera hizi za matukio na kutafuta Sympathy kwa watanzania.
Maana hata watanzania pia wanaihitaji hiyo hiyo Sympathy toka kwenu wanasiasa.Badala yake nyinyi mnawatumia wananvhi kama ngao ya kujikingia ili mjinufaishe binafsi

Kwa Dunia hii yenye utandawazi uliokithiri,kuwa mpinzani kunahitaji uwe mkweli na muwazi.uwe kweli unaakisi uhalisia na wananchi waweze kuweka imani kwako

Maana uelewa wa wananchi ni mkubwa kwa sasa tofauti na hapo awali.Pia mawasiliano na mifumo yake imebadilika kwa kiasi kwamba wananchi kwa asilimia kubwa wanapata na kuelewa habari nyingi nchini kwa wakati husika na kusha kuzifanyia upembuzi makini.

Ila wanasiasa mmeeendelea kuwachukulia wananchi kama watu wasiojielewa elewa ki- viile!

Lakini kumbe unakuta wananchi ndio wamewapuuza wanasiasa baada ya kuchoka na ngonjera zao zisizo na ukomo wala ukweli.

Sasa siasa imegeka kuwa sehemu ya ajira na kipato cha utajiri, na sio kipawa cha uongozi na maadili mema!

Hili ni tatizo kubwa kwa wanasiasa wa Tanzania..kote kabisaa!
Sio CCM wala Chadema pekee,bali vyama vyote!

Tukisema Chadema mnapenda kick za matukio kupata Political Mileage mnasema tunakosea?
Mfano wa hili ni juzi huko Katesh.

Chadema jipimeni kwa kina maana kwa uhalisia ni kwamba mnahitaji uongozi mpya wenye kuweza kufanya mabadiliko makubwa na ubunifu wa sera na mbinu za ufanyaji siasa kuendana na wakati uliopo ili muweze kwenda sambamba na upepo halisi wa kisiasa nchini.

Viongozi waliopo kwa sasa pumzi yao inaonekana rasmi, ndio inaelekea imefikia ukomo kisiasa.
Hawana mbinu mpya za kukabiliana na CCM wanaobadilishana vijiti kila baada ya miaka kumi(10).

Kama ni riadha ya kisiasa!
Mbowe ameishazunguka uwanja mpaka amepitiliza na vijiti nje ya uwanja. na sasa anakimbia peku kwenye lami.
Msaidieni......

Kwa kuwa matusi ni sehemu ya seraza baadhi yenu!sintawashangaa mkianza kuyaporomosha hapa
Ila mimi nimemaliza kutoa langu la Moyoni.

Niwatakie SABHATHO njema!
 
Mtoa hoja unasemea watanzania gani waliokupa uwezo wa kuwasemea?pambana mwenyewe na usitegemee watu wengine wakupiganie, uoga wako wa kizuzu, ndio kila wakati unakufanya uje kulalama humu, push back yako ipo wapi? Unalalama humu then usiku ukifika unanyatia kitanda chako!

Miaka 60 sasa Tanzania imetawaliwa na ccm,bado wale maadui wapo na wametamalaki, ujinga, umasikini, maradhi na sasa rushwa!

Mkuu mtoa hoja Shuka huko juu na uje kwenye hawa poor of the poorest ujionee uhalisi wa maisha yao, mvua za jana nimetembelea Temeke, ni shida mkuu, kila nyumba imepata swimming pool chafu ,inayonuka mbele ya nyumba zao, ukiuliza mhusika yupo wapi ,yeye anaishi Masaki!!
 
Mwaka gani ambapo walikua na pumzi na CCM wakawasifu kua CHADEMA sasa ina viongozi wenye pumzi au wanaonekana tu wakiwa hawana pumzi?
Siku zote usifanye suasa kwa kutegemea sifa toka kwa mpinzani wako!
Ndio maana akaitwa mpinzani!
Ukiona mpinzani wako anakusifia ujuwe ananeemeka na sehemu ya uongozi wako!

Ma ukiona malalamiko yamezidi ujuwe umembana mahali fulani!

Chama mahiri na makini hujitahidi kuwekeza kwa wananchi ambao ndio desicion makers!
Unajiandaa kuanzia grass root kisha ndio unaenda huko juu kwenye matawi.

Lakini kwa Tanzania wapinzani wanaanzia kushambulia juu badala ya shina la mti.
 
Ninasemacl hivyo kutokana na mtazamo wangu binafsi.siwakilishi chama chochote cha kisiasa nchini.

Mbinu za ufanyaji siasa za chadema kwa sasa zimepitwa na wakati.tunaposema hivyo tuna maanisha kwamba ...wananchi wanahitaji tofauti.
Wakati Chadema mnalo hitaji lenu tofauti.

Jaribuni kukaa na kupata watunga sera mahiri ili wawasaidie kutunga sera zinazoeagusa wananchi kwa 100%.

Badala ya Sera za matukio na kutafuta Sympathy kwa watanzania.
Maana hata watanzania pia wanaihitaji hiyo hiyo Sympathy toka kwenu wanasiasa badala yake nyinyi mnawatumia wananvhi kama ngao ya kujikingia ili mjinufaishe binafsi

Kwa Dunia hii yenye utandawazi uliokithiri,kuwa mpinzani kunahitaji uwe mkweli na muwazi.uwe kweli unaakisi uhalisia na wananchi waweze kuweka imani kwako.

Hili ni tatizo kubwa kwa wanasiasa wa Tanzania..kote kabisaa!
Sio CCM wala Chadema pekee,bali vyama vyote!

Tukisema Chadema mnapenda kick za matukio kupata Political Mileage mnasema tunakosea?

Chadema jipimeni kwa kina maana kwa uhalisia ni kwamba mnahitaji uongozi mpya wenye kuweza kufanya mabadiliko makubwa na ubunifu wa sera na mbinu za ufanyaji siasa kuendana na wakati uliopo ili muweze kwenda sambamba na upepo halisi wa kisiasa nchini.

Viongozi waliopo kwa sasa pumzi yao inaonekana rasmi, ndio inaelekea imefikia ukomo kisiasa.
Hawana mbinu mpya za kukabiliana na CCM wanaobadilishana vijiti kila baada ya miaka kumi(10).

Kama ni riadha ya kisiasa!
Mbowe ameishazunguka uwanja mpaka amepitiliza na vijiti nje ya uwanja. na sasa anakimbia peku kwenye lami.
Msaidieni......

Kwa kuwa matusi ni sehemu ya sera zenu,sintawashangaa mkianza kuyaporom9sha hapa!
Ccm bana mmebaki na story za kijinga, mmepotezea siasa mvuto, saa hii mmebaki kuleta ushauri na vitisho vya kijinga. Kwa taarifa yako kabla ya kufika kuwapa cdm ushauri, ni vyema ungewashauri ccm kuwa kizazi kimebadilika, Yale mambo ya kutawala kwa shuruti na kuhujumu Kila chama pinzani, kitaacha siasa za nchi hii zikiwa hazina mvuto, huku ccm ikilazimisha kutawala kizazi kilichoichoka.

Hata muhujumu Kila chama Cha upinzani kwa sababu za kweli na kutunga, Bado hakutaifanya ccm ipate mvuto, sana sana mtaishia kufanya siasa na chaguzi kupuuzwa. Yaani kama kweli unataka kutoa ushauri, washauri ccm zaidi maana wao ndio tatizo la msingi wa siasa za nchi hii. Kutawala muda mrefu kwa mabavu wakati kizazi kimeshabadilika ni kujipotezea muda Bure, na kufanya siasa zipuuzwe.
 
Mtoa hoja unasemea watanzania gani waliokupa uwezo wa kuwasemea?pambana mwenyewe na usitegemee watu wengine wakupiganie, uoga wako wa kizuzu, ndio kila wakati unakufanya uje kulalama humu, push back yako ipo wapi?,unalalama humu then usiku ukifika unanyatia kitanda chako!,miaka 60 sasa Tanzania imetawaliwa na ccm,bado wale maadui wapo na wametamalaki, ujinga, umasikini, maradhi na sasa rushwa!,mkuu mtoa hoja Shuka huko juu na uje kwenye hawa poor of the poorest ujionee uhalisi wa maisha yao, mvua za jana nimetembelea Temeke, ni shida mkuu, kila nyumba imepata swimming pool chafu ,inayonuka mbele ya nyumba zao, ukiuliza mhusika yupo wapi ,yeye anaishi Masaki!!
Nimekwisha tamka kabla kwamba siwakilishivchama wala mtu yeyote!
Haya ni maoni yangu binafsi na kwa izoefu wangu wa mambo ninavyoyadhuhudia kila uchao nchini.

Hayo mambo ya luwasemea wananchi mimi sijatamka humu.
Bali nimejisemea mimi kama mwananchi.
Na ushauri wa kushuka chini huku grass roots ndio hasa ungewapatia viongozi wako huko Chadema.

Tena mfano mdogo umenikilumbusha kwamba viongozi hawa waandamizi Chadema familia zao ziko ughaibuni huko.
1- Tundu lissu.
2-Godbless Lema.
3-Freeman Mbowe.

Kwa kauli zao wenyewe wamewahi kukiri hilo.tena wengine hata uraia wa Tanzania walikwisha ukana.
Sasa hao ndio wanaohimiza mabadiliko huku akaunti zikiwa nono huko majuu.
 
Siku zote usifanye suasa kwa kutegemea sifa toka kwa mpinzani wako!
Ndio maana akaitwa mpinzani!
Ukiona mpinzani wako anakusifia ujuwe ananeemeka na sehemu ya uongozi wako!

Ma ukiona malalamiko yamezidi ujuwe umembana mahali fulani!

Chama mahiri na makini hujitahidi kuwekeza kwa wananchi ambao ndio desicion makers!
Unajiandaa kuanzia grass root kisha ndio unaenda huko juu kwenye matawi.

Lakini kwa Tanzania wapinzani wanaanzia kushambulia juu badala ya shina la mti.
Anzisha chama uanzie kwenye hizo grass roots. Kwa taarifa yako kwa aina ya katiba ya nchi hii, ni Wenda wazimu kuamini wananchi ndio wafanya maamuzi. Tulivyo na chaguzi za kishenzi ni nadra hiyo nguvu ya wananchi kuonekana. Tungekuwa na chaguzi zinazoheshimiwa ushauri wako ungekuwa na maana.
 
Tunajua wewe una cheo zaidi ya kamanda mwashambwa, kama chawa mwandamizi...
Ni muda unasubiri ili uwe activated....
 
Nimekwisha tamka kabla kwamba siwakilishivchama wala mtu yeyote!
Haya ni maoni yangu binafsi na kwa izoefu wangu wa mambo ninavyoyadhuhudia kila uchao nchini.

Hayo mambo ya luwasemea wananchi mimi sijatamka humu.
Bali nimejisemea mimi kama mwananchi.
Na ushauri wa kushuka chini huku grass roots ndio hasa ungewapatia viongozi wako huko Chadema.

Tena mfano mdogo umenikilumbusha kwamba viongozi hawa waandamizi Chadema familia zao ziko ughaibuni huko.
1- Tundu lissu.
2-Godbless Lema.
3-Freeman Mbowe.

Kwa kauli zao wenyewe wamewahi kukiri hilo.tena wengine hata uraia wa Tanzania walikwisha ukana.
Sasa hao ndio wanaohimiza mabadiliko huku akaunti zikiwa nono huko majuu.
Bado una siasa za kishamba za kuangalia maisha binafsi ya viongozi. Wananchi wameshapuuza uchaguzi maana hakuna heshima tena kwenye maamuzi Yao. Ww unatuletea habari za grassroots wakati tunaona hata chaguzi za serekali za mitaa zinapuuzwa. Amka ww, hiki sio kizazi Cha ccm, sana sana mmefanikiwa kufanya watu wakinai siasa kwa kulazimisha kutawala kizazi kilichowachoka.
 
Anzisha chama uanzie kwenye hizo grass roots. Kwa taarifa yako kwa aina ya katiba ya nchi hii, ni Wenda wazimu kuamini wananchi ndio wafanya maamuzi. Tulivyo na chaguzi za kishenzi ni nadra hiyo nguvu ya wananchi kuonekana. Tungekuwa na chaguzi zinazoheshimiwa ushauri wako ungekuwa na maana.
Ninaposena grassroots nina maana ya kuwekeza kwa wananchi ambao mwisho wa siku wakikuelewa na kukuamini.
Kwa wingi wao lolote linawezekana!
Iwe ni kujitokeza kuandamana au iwe ni kulinda kura nk.

Lakini hii haiwezi kutokea endapo kwanza hutashuka na kuwajengea imani ya uaminifu wananchi hao ili wakuamini kweli uko nao.
Na kwamba kile unachowaambia mkipiganie ni kwa maslahi yenu wote.
CCM wanatumia aina hiyo ya mbinu na kutokana na uelewa mdogo wa watanzania hususan wa vijijini.
Wanafanikiwa ukiongezea na nguvu ya Rushwa inayosaiduwa na. Njaa ya wananchi.
Hivyo upinzani nchini hauwezi kufanikiwa kuiamgusha CCM kama hautafanikiwa kujisimika mashinani badala ya kuanzia Dodoma.l na kusubiri uchaguzi.
 
Bado una siasa za kishamba za kuangalia maisha binafsi ya viongozi. Wananchi wameshapuuza uchaguzi maana hakuna heshima tena kwenye maamuzi Yao. Ww unatuletea habari za grassroots wakati tunaona hata chaguzi za serekali za mitaa zinapuuzwa. Amka ww, hiki sio kizazi Cha ccm, sana sana mmefanikiwa kufanya watu wakinai siasa kwa kulazimisha kutawala kizazi kilichowachoka.
Kabla hujaniambia mimi kuamka,ulipaswa kumwambia mwenyekiti Mbowe aamke na kufanya upinzani unaoendana na karne ya kisasa!
Kuyaangalia maisha binafsi ya kiongozi wa kisiasa ndio wajibu namba moja kwa mwananchi.
Ndio maana hao tunaowauga siasa zao huko ughaibuni....
Maisha binafsi yako screened kwa 100%.
Hususan Uingereza kwenyewe nyumbani mwa "Commonwealth"
Unapotafuta kuongoza watu wakati wewe sio msafi hilo ni kufuli kubwa mguuni.
Ndio maana unawaona kina Chongolo wakilazimika kujiuzuru.
 
Ninaposena grassroots nina maana ya kuwekeza kwa wananchi ambao mwisho wa siku wakikuelewa na kukuamini.
Kwa wingi wao lolote linawezekana!
Iwe ni kujitokeza kuandamana au iwe ni kulinda kura nk.

Lakini hii haiwezi kutokea endapo kwanza hutashuka na kuwajengea imani ya uaminifu wananchi hao ili wakuamini kweli uko nao.
Na kwamba kile unachowaambia mkipiganie ni kwa maslahi yenu wote.
CCM wanatumia aina hiyo ya mbinu na kutokana na uelewa mdogo wa watanzania hususan wa vijijini.
Wanafanikiwa ukiongezea na nguvu ya Rushwa inayosaiduwa na. Njaa ya wananchi.
Hivyo upinzani nchini hauwezi kufanikiwa kuiamgusha CCM kama hautafanikiwa kujisimika mashinani badala ya kuanzia Dodoma.l na kusubiri uchaguzi.
Kama hao wananchi wanapatikana kwa uelewa wao mdogo na rushwa, ni kipi utafanya kwa watu wa aina hiyo? Au huko kwenye grass root utatengeneza watu wako tofauti na hao wajinga na waabudu rushwa?

Nimekushauri anzisha chama ufanyie huu ushauri wako, ni lazima utachukua nchi. Au ni mambo ya motivational speaker?
 
Ninasemacl hivyo kutokana na mtazamo wangu binafsi.siwakilishi chama chochote cha kisiasa nchini.

Mbinu za ufanyaji siasa za chadema kwa sasa zimepitwa na wakati.tunaposema hivyo tuna maanisha kwamba ...wananchi wanahitaji tofauti.
Wakati Chadema pia mnalo hitaji lenu tofauti.

Jaribuni kukaa na kupata watunga sera mahiri ili wawasaidie kutunga sera zinazoeagusa wananchi kwa 100%.

Badala ya Sera hizi za matukio na kutafuta Sympathy kwa watanzania.
Maana hata watanzania pia wanaihitaji hiyo hiyo Sympathy toka kwenu wanasiasa.Badala yake nyinyi mnawatumia wananvhi kama ngao ya kujikingia ili mjinufaishe binafsi

Kwa Dunia hii yenye utandawazi uliokithiri,kuwa mpinzani kunahitaji uwe mkweli na muwazi.uwe kweli unaakisi uhalisia na wananchi waweze kuweka imani kwako.
Maana uelewa wa wananchi ni mkubwa kwa sasa tofauti na hapo awali.Pia mawasiliano na mifumo yake imebadilika kwa kiasi kwamba wananchi kwa asilimia kubwa wanapata na kuelewa habari nyingi nchini kwa wakati husika.

Ila wanasiasa mmeeendelea kuwachukulia wananchi kama watu wasiojielewa elewa ki viile!
Lakini kumbe unakuta wananchi ndio wamewapuuza wanasiasa baada ya kuchoka na ngonjera zao zisizo na ukomo wala ukweli.

Sasa siasa imegeka kuwa sehemu ya ajira na kipato cha utajiri, na sio kipawa cha uongozi na maadili mema!

Hili ni tatizo kubwa kwa wanasiasa wa Tanzania..kote kabisaa!
Sio CCM wala Chadema pekee,bali vyama vyote!

Tukisema Chadema mnapenda kick za matukio kupata Political Mileage mnasema tunakosea?

Chadema jipimeni kwa kina maana kwa uhalisia ni kwamba mnahitaji uongozi mpya wenye kuweza kufanya mabadiliko makubwa na ubunifu wa sera na mbinu za ufanyaji siasa kuendana na wakati uliopo ili muweze kwenda sambamba na upepo halisi wa kisiasa nchini.

Viongozi waliopo kwa sasa pumzi yao inaonekana rasmi, ndio inaelekea imefikia ukomo kisiasa.
Hawana mbinu mpya za kukabiliana na CCM wanaobadilishana vijiti kila baada ya miaka kumi(10).

Kama ni riadha ya kisiasa!
Mbowe ameishazunguka uwanja mpaka amepitiliza na vijiti nje ya uwanja. na sasa anakimbia peku kwenye lami.
Msaidieni......

Kwa kuwa matusi ni sehemu ya sera zenu,sintawashangaa mkianza kuyaporom9sha hapa!

Niwatakie SABHATHO njema!
Ngonjera ndeeeefu sijapata mantiki yako,vp ndugu au ndo sukuma gang nn msioamini mpaka leo kua mwendazake hatunae,km kufiwa tulifiwa wote ila kuna mliofiwa zaidi .Km ccm inadeliver kile watz wanastahili wateseka nn na hao "watoa taarifa"!?.
 
Chadema nayo ni yakushauriwa na manyangarakasha! Haka kanyangarakasha kanawashauri viongozi wa Chadema wakati kenyewe kameshindwa kuyanyoosha maisha yake! Tanzania kila mtu mjuaji.
 
Kabla hujaniambia mimi kuamka,ulipaswa kumwambia mwenyekiti Mbowe aamke na kufanya upinzani unaoendana na karne ya kisasa!
Kuyaangalia maisha binafsi ya kiongozi wa kisiasa ndio wajibu namba moja kwa mwananchi.
Ndio maana hao tunaowauga siasa zao huko ughaibuni....
Maisha binafsi yako screened kwa 100%.
Hususan Uingereza kwenyewe nyumbani mwa "Commonwealth"
Unapotafuta kuongoza watu wakati wewe sio msafi hilo ni kufuli kubwa mguuni.
Ndio maana unawaona kina Chongolo wakilazimika kujiuzuru.
Unasema huko kwenye grass root watu ni wajinga na wanapatikana kwa rushwa, huyo mwenyekiti atafanya nini kwenye kizazi cha aina hiyo? Hiyo Karne ya kisasa iliyojaa wajinga huko kwenye grass roots na wanaopatina kwa rushwa ni siasa zipi za kisiasa utawapelekea wakati tayari wao ni wajinga?

Badala ya kuleta ushauri wa kinadharia, anzisha chama ukafanyie kazi maana tayari mwenyekiti wa cdm ameshindwa.
 
Kama hao wananchi wanapatikana kwa uelewa wao mdogo na rushwa, ni kipi utafanya kwa watu wa aina hiyo? Au huko kwenye grass root utatengeneza watu wako tofauti na hao wajinga na waabudu rushwa?

Nimekushauri anzisha chama ufanyie huu ushauri wako, ni lazima utachukua nchi. Au ni mambo ya motivational speaker?
Watapatikana kwa kutumia utoaji elimu mashinani kupitia vijana wapya wenye elimu kubwa ya uelewa waliojazana huko mitaani na vijijini wakiwa bila fursa!

Hao watatumika sambamba na kusimika uongozi wa vyama vya upinzani madhinani ili kwenda sambamba na wenzao wa CCM.
Ruzuku itumike zaidi vijijini badala ya kukodi helkopta angani.
Wapinzani wawekeze ardhini kwa wananchi ili kuwabana mabalozi na watendaji wa CCM mashinani,ambako rasmi ndiko wizi huratibiwa rasmi.
 
Anzisha chama mkuu ufanye haya yote lazima utachukua nchi. Au ww huna uthubutu wa kuanzisha chama, lakini una ushauri tu?
 
Ngonjera ndeeeefu sijapata mantiki yako,vp ndugu au ndo sukuma gang nn msioamini mpaka leo kua mwendazake hatunae,km kufiwa tulifiwa wote ila kuna mliofiwa zaidi .Km ccm inadeliver kile watz wanastahili wateseka nn na hao "watoa taarifa"!?.
Magufuli kufariki sio mpango wako wewe au mimi.
Kamwe jaribu kuheshimu baadhi ya mambo kama vile maamuzi ya Mungu.
Maana Magufuli sio wa kwanza kufa na pia sio wa mwisho kufa.
Bali wote tutaendelea kufa.

Sasa naanza kupata picha kwa nini Chadema mliumia na mbaendelea kuumia na ujio wa Makonda na Sabaya Senior kwenye siasa za CCM ilhali sio chama chenu.
 
Kama hao wananchi wanapatikana kwa uelewa wao mdogo na rushwa, ni kipi utafanya kwa watu wa aina hiyo? Au huko kwenye grass root utatengeneza watu wako tofauti na hao wajinga na waabudu rushwa?

Nimekushauri anzisha chama ufanyie huu ushauri wako, ni lazima utachukua nchi. Au ni mambo ya motivational speaker?
Huyo achana nae mkuu,bado yupo kwenye mambolezo ya mwendazake,anamiliki ujinga wa kihalaiki.Kazi wanayoifanya hao"watoa taarifa" kwa aina ya wananchi wa tz ni ngumu haswa,nimewahi shiriki hizi siasa za tz back 2010 nilijifunza mengi sana jinsi chama cha mambuzi kilivyocorrupt mind set za wadanganyika.Tulifanya siasa ngumu kweli na jimbo tulichukua ila baada ya hapo niliona wadanganyika sio watu wa kuwapigania.
 
Watapatikana kwa kutumia utoaji elimu mashinani kupitia vijana wapya wenye elimu kubwa ya uelewa waliojazana huko mitaani na vijijini wakiwa bila fursa!

Hao watatumika sambamba na kusimika uongozi wa vyama vya upinzani madhinani ili kwenda sambamba na wenzao wa CCM.
Ruzuku itumike zaidi vijijini badala ya kukodi helkopta angani.
Wapinzani wawekeze ardhini kwa wananchi ili kuwabana mabalozi na watendaji wa CCM mashinani,ambako rasmi ndiko wizi huratibiwa rasmi.
Kutumia helikopta ni rahisi sana kuliko kutumia mav8 kumi na tano yanazurula nchi nzima yakiwashwa asubuhi hayazimwi mpaka kwenda kulala, tumia akili kabla ya kuandika.
 
Back
Top Bottom