Mbowe ni Genius wa Kisiasa. Mbobevu wa mikakati ya kisiasa

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
502
938
Nilipigwa na Butwaa tangu awali pale nilipo ona Slaa anakuwa Msemaji Mkubwa kwenye Suala la Bandari Kwa Jukwaa la Chadema kama kwamba , Chadema ina Mapungufu ya Wasemaji Vile.

Mbowe ninae MFAHAMU Mimi sikuamini kama asingeweza kuona Mtego wa Dr Slaa kupitia Upepo huu wa Bandari.

Katika Wanasiasa ambao ni Wanauwezo wa Kimkakati basi Mbowe ni Mmoja wapo kama watakuwa wawili , Kwa hivyo Mwanamkakati ni rahisi kutegua Mkakati anao wekewa.

Kwa Slaa hoja haikuwa Bandari Bali hoja ilikuwa ni Maumivu ya Kupoteza Ubalozi tu.

Anyway

Chadema ni Chama chenye Mikakati yake hakipaswi kuongezewa Mikakati na Watu wasiokuwa sehemu ya Uongozi.

Dr na wenzake Wasubiri kualikwa kwenye Mikutano ya Chadema ikiwa Viongozi wa Chadema itawapendeza kufanya hivyo au Waanzishe Chama ili wapate Jukwaa la kudai Bandari lakini si kuanzisha Program za Mikutano kupitia Chadema.

Nadhani Mbowe yupo Sahihi kwenye hili.


Andiko hili nimelinakiri kutoka katika ukurasa wa Facebook wa mwanasiasa Abdul Kambaya ambaye alikuwa mwanachama mwandamizi wa CUF, kisha akahamia Chadema na baada ya siku kadhaa, akaachana na Chadema
 
Back
Top Bottom