Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,895
- 2,778
Sijui kama hili limeshawaingia kwenye milango yenu ya fahamu. Jina la kampuni yenu linatumika VIBAYA mno! Imekuwa ni kawaida watu kuzungumzia tigo kama njia ya haja kubwa. Neno tigo pia linatumika kuhamasisha ngono kinyume na maumbile (ulawiti). Ni rahisi sana mtu kusema 'naomba tigo' akimaanisha kulawiti. Tatizo hili limechangiwa na namna mnavyotangaza huduma zenu. Kiukweli neno tigo linakuwa gumu kutamkika kadri siku zinavyoenda. Labda tigo mtuambie mnafarijika mnavyohusishwa na njia ya haja kubwa.
Kweli jina ni lenu lakini mmechangia sana kuliletea sifa mbaya. Mnakumbuka yeboyebo? Kubazi zilipendwa sana ila tatizo sabasaba moja tu iliharibu kabisa jina na biashara ya kubazi zile. Sasa na nyie heshima yenu inashuka.
Nalisema hili kutokana na jinsi watu katika jamii wanavyolitumia kuelezea njia ya haja kubwa. Balaa zaidi ni katika mitandao ya kijamii mfano jf. Watu wameshalitohoa na kulitumia watakavyo.
Ni wakati wa kampuni hii ya simu kubadili jina sasa na kupiga marufuku matumizi yake popote. JF pia natoa wito kwenu kukataza matumizi yasio sahihi kwa jina hili katika mijadala ya humu.