Tigo mnatuonea wateja wa zamani wa Postpaid, huu ni wizi

Mzalendo.mataro

New Member
Feb 9, 2012
2
0
Hello, wadau wa JF, kuna vitu nadhani sisi kama nchi hatuwi makini haswa kwa hawa Viongozi wetu tunachaguliwa, hili linakwenda moja kwa moja kwa Waziri Nape.

Kuna hizi huduma za Mitandao ya Simu Postpaid kwa safari hiii naizungumzia haswa ya Tigo. Tulielekezwa tukajiunga, Mr. Mm natumia ya 30K, kwa mwezi ambapo before ilikua wanatupatia 25GB baaadae wakabadilisha wakawa wanatupa (15-20) GB, na walitupunguzia kiwango bila kutushirikisha it was ok anyway tukakubali.

Sasa this time wameongeza kiwango cha GB now ukilipia 30K unatakiwa kupata 35GB, ila sisi ambao tumejiunga zamani still bado tunaendelea kupata (15-20) GB ila kwa wapya wanaojiunga wanapata 35GB.

Yaani hili kitendo kimeniuma mnoo, ni wizi wa wazi huu tunafanyiwa lakini tuna mamlaka tuna wataalam wa Serikari wanao deal na hizi issues waziri yupo amekaa pale ambaye hata kuna kipindi najiuliza jukumu lake kubwa ni lipi maana silioni.

Yaani what if kama asingekua pale waziri au cheo/ asingekua yeye nini kingeleta utofauti na uwepo wake? Yaani he’s there kwakuwa it’s just a position and someone should just feel it isikae wazi.

Yaani Tigo walipotaka kutupunguzia GB walifanya wenyewe ndani kwa ndani ila now wameongeza wanasema kwakuwa wewe ulisign mkataba wa zamani so utaendelea kukatwa kiwango cha zamani, seriously?

Ili hali wote mnalipa kiwango sawa, mbona wakati wanapunguza hawakutushirikisha? This is painful kwakweli, pale unakuwa Mwaminifu kulipia huduma lakini mtoa huduma ni JAMBAZI anakunyonya nakukuibia bila aibu.
 
Back
Top Bottom