Ni wakati muafaka kuivunja TISS sasa!

Ni wakati muafaka kuivunja TISS sasa!

Kwani TISS ni nini ? Inajumuisha watu wa aina gani Mkuu ? Ina maana wale jamaa wa Military Intelligence hawawezi kubeba mikoba wakati hii TISS ya sasa inafanyiwa overhaul ?

Nakumbuka wakati fulani Jeshini kuna watoto wasiokuwa na adabu walikuwa kwenye kozi ya ukomando wakawa wanataka pesa fulani wakajifanya kuanzisha kimgomo na kuja hapo Upanga ... Kilichotokea ni kuondolewa kwenye hiyo kozi na kuvuliwa uanajeshi na kufungwa

Kuna mambo ya nchi hayataki uhuni uhuni hivi kuyaendesha sasa kama idara hii imefikia kwenye uhuni huu wa kutumia askari wa Raisi kuvamia media za watu kwanini isivunjwe ?
TISS 80% wako vizuri..ila Treni inafata injini
 
Kuvuja tiss ni kutengeneza tatizo jingine. La muhimu ni kutenganisha tiss na ccm na kuachakuajili tiss kwa mingi ya uccm au mtoto wa shangazi. Pa , tiss watumike kupambana vita ya kiychumi dhidi ya mataifa jirani na mengine na siyo kupambana na wakina Roma, Saa8 kwa kuwakosoa watawala.
 
tissivunjwe.png
Kuna namna nyingi za kushughulikia yanayoendelea nchini sasa hivi na hasa madai makali dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Mengi tumeshazungumza juu ya Idara hii na kwa muda mrefu. Bahati mbaya inaonekana hata wabunge wetu hawajaona njia rahisi na ya haraka ya kusafisha idara hii. Tayari inaonekana wapo wabunge wengi kutoka pande zote mbili ambao wanakubaliana kuwa kuna tatizo fulani katika Idara. Sasa kwanini wabunge wasitumie umoja wao huu wa misimamo kufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao?

Wabunge ndio watunga sheria wa nchi hi (law makers). Rais hatungi sheria hata moja; yeye kwake ni kuzipitisha tu. Siyo tu wabunge wanatunga lakini pia wanaweza kufanya marekebisho sheria na Katiba!

Sasa kuna pendekezo la Zitto kuchunguza matukio mbalimbali ambayo yanadaiwa kutokea hivi karibuni na Idara kuhusishwa. Njia hii ya Kamati Teule inaweza kutangulia – kama alivyodokeza – mabadiliko yoyote ya idara. Kamati Teule inaweza kuwaita watendaji na wakuu wote wa idara za usalama na kuwahoji chini ya kiapo – mbele ya camera au nje ya camera – na kutaka kujua nini kinaendelea. Na kwa vile Kamati ina nguvu za kibunge na mahakama inaweza kumlazimisha yeyote kati yao kufika mbele ya kamati hiyo au kuagizwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya kamati hiyo.

Hiyo inaweza kuwa ni njia sahihi ya kutaka kutafuta ukweli. Pamoja na kuwaita hawa wote inaweza kuwaita hata waathirika wa vitendo hivi. Bashe kwa mfano anaweza kuitwa mbele ya Kamati hiyo na kutoa ushahidi wa madai ya kuwa kuna “mawaziri” ambao wamempa taarifa kuwa yeye ni mlengwa wa kutekwa; Zitto mwenyewe vile vile n.k Lengo ni kutaka kujua ukweli zaidi ili watakapotaka kufanya mabadiliko wajue wapi pa kuanzia.

kipilimba-e1491927638963.jpg

Mkurugenzi wa TISS Dkt. Modestus Kipilimba
Hata hivyo, hilo linahitaji kuungwa mkono sana na wabunge wa CCM. Njia ya pili ambayo binafsi naipenda zaidi kama njia ya haraka ni kwa wabunge wenye kuona tatizo hasa – Bashe, Ridhiwani, Zitto, na wengine wakutane pamoja na kuandaa mswaada wa pamoja (bipartisan bill) ya kuivunja Idara ya Usalama wa Taifa na kuiunda upya ikiwa imetengenezwa kukidhi mahitaji ya kiusalama ya taifa hili na ikisimamiwa moja kwa moja na Bunge. Mswada huu uletetwe hata kwa hati ya dharura ili kabla ya Bunge hili kuisha usomwe unavyohitajika na upitishwe na Bunge na hatimaye upelekwe kwa rais kwa kuudhinisha.

Nina uhakika Rais Magufuli ataridhia kwani atakuwa amesaidiwa kazi ambayo labda ingemchukua muda yeye mwenyew ekuifanya. Na kama hatoridhia na kutishia Veto Bunge linaweza kuipiku veto hiyo kwa kura nyingi na kumlazimisha aisaini na kama haitowezekana basi Bunge litavunjwa na watu watarudishwa kwenye uchaguzi mkuu mpya ambapo wananchi watapata nafasi ya kwenda kuchagua wabunge na Rais mwingine kulingana na ajenda watakazosimama nazo.

Lakini kulalamika tu wakati nyenzo wanazo ni kupoteza muda wa watu. Ni wakati wa kufanya wanachoamini ni sahihi kufanya na wana uwezo wa kukifanya. Lakini pia utakuwa ni wakati wa watu kuhesabiwa. Kwa sisi wengine ambao tumekuwa tukilalamikia idara hii kwa muda mrefu tunaona labda hii ni nafasi ya pekee ya kuileta Idara hii kwenye karne ya 21. Inapofikia watu tena wazito wanadai kuwa Idara inajihusisha au watumishi wake wanajihusisha na vitendo ovya kighaidi hakuna namna namna nyingine ya kufanya isipokuwa kuivunja idara hiyo na kuiunda upya toka chini. Mkitaka mawazo tupo wengine tunaweza kuwasaidia.

KWA KUSOMA KWA KIREFU BONYEZA ZAMAMPYA.COM
Waambie huko uliko USA waivunje kwanza CIA na sisi Tutavunja TISS
 
Kuvuja tiss ni kutengeneza tatizo jingine. La muhimu ni kutenganisha tiss na ccm na kuachakuajili tiss kwa mingi ya uccm au mtoto wa shangazi. Pa , tiss watumike kupambana vita ya kiychumi dhidi ya mataifa jirani na mengine na siyo kupambana na wakina Roma, Saa8 kwa kuwakosoa watawala.
 
Mkuu TISS sio kama bodi ya korosho kule lindi useme unaweza kuivunja tu anytime...utatengeneza tatizo zaidi ya hili....solution Bunge limuwajibishe sizonje na vibaraka wake tu

Tiss lazima ivunjwe na Tiss mpya lazima ijitegemee sio kutegemea maagizo kutoka Ikulu.
 
Mwaka 2015 mleta mada pamoja na makada wenzako wa CCM mlikuwa unafurahia na kupiga makofi wakati TISS ilipogeuzwa kuwa idara maalum ndani ya CCM kupambana UKAWA kwenye uchaguzi mkuu ikitumia kila njia za hila kuumiza upinzani na kuiba kura.
Leo mmegundua hata nyinyi kumbe hamko salama na sasa mnaimba hiyo TISS ifute.

Taratibu tu tutaanza kuongea lugha moja, tutanyooka tu. Bila shaka ipo siku swahiba wako Dr.Slaa naye ataonja joto ya jiwe na kufunguka kama wewe. Ngoja posho aliyopewa iishe arejee bongo kuja kupigika....
Hawa CCM walifuga mamba ndani leo kawageuka ameanza kuwatafuna wao.
 
Mkuu unaamini kabisa mkulu atasaini sheria hiyo mpya?Siamini,kwakuwa yote yanayotokea yanaonekana kuwa na baraka kutoka ofisi kuu.
 
Nadhan ungesema... TISS itenganishwe na siasa.... eg.. wakuu wa mikoa wasiweze kuwatumia TISS bila kupata kibali maalumu.
Kundi flani la viongozi wa serikal wasiweze kuwa na mamlaka juu ya TISS
 
Tatizo siyo TISS bali Bashite........ Wao wanatii amri. Ukizungumza na baadhi yao wanasema tatizo ni amri toka kwa malaika mkuu.
 
Watanzania tufanye kazi. Tumezoa kuzusha mijadala kila kitu kinageuka kuw siasa. Hawa wanasiasa uchwara wanaturudisha nyuma. Bado nchi yetu ina fursa nyingi tuchangamkie fursa ili kujiletea maendeleo katika ngazi ya zote. Tuachwe kuendeshwa na wanasiasa uchwara kila Siku wanabadili mada baada ya kuona mirija Yao ya ulaji imekatwa sasa wanahaha kuichonganisha serikali na wananchi kwa mbinu za siri Na wazi. Tumeshawagundua
 
M

mkuu we ni kiongozi? Nina shida yangu
 
tissivunjwe.png
Kuna namna nyingi za kushughulikia yanayoendelea nchini sasa hivi na hasa madai makali dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Mengi tumeshazungumza juu ya Idara hii na kwa muda mrefu. Bahati mbaya inaonekana hata wabunge wetu hawajaona njia rahisi na ya haraka ya kusafisha idara hii. Tayari inaonekana wapo wabunge wengi kutoka pande zote mbili ambao wanakubaliana kuwa kuna tatizo fulani katika Idara. Sasa kwanini wabunge wasitumie umoja wao huu wa misimamo kufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao?

Wabunge ndio watunga sheria wa nchi hi (law makers). Rais hatungi sheria hata moja; yeye kwake ni kuzipitisha tu. Siyo tu wabunge wanatunga lakini pia wanaweza kufanya marekebisho sheria na Katiba!

Sasa kuna pendekezo la Zitto kuchunguza matukio mbalimbali ambayo yanadaiwa kutokea hivi karibuni na Idara kuhusishwa. Njia hii ya Kamati Teule inaweza kutangulia – kama alivyodokeza – mabadiliko yoyote ya idara. Kamati Teule inaweza kuwaita watendaji na wakuu wote wa idara za usalama na kuwahoji chini ya kiapo – mbele ya camera au nje ya camera – na kutaka kujua nini kinaendelea. Na kwa vile Kamati ina nguvu za kibunge na mahakama inaweza kumlazimisha yeyote kati yao kufika mbele ya kamati hiyo au kuagizwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya kamati hiyo.

Hiyo inaweza kuwa ni njia sahihi ya kutaka kutafuta ukweli. Pamoja na kuwaita hawa wote inaweza kuwaita hata waathirika wa vitendo hivi. Bashe kwa mfano anaweza kuitwa mbele ya Kamati hiyo na kutoa ushahidi wa madai ya kuwa kuna “mawaziri” ambao wamempa taarifa kuwa yeye ni mlengwa wa kutekwa; Zitto mwenyewe vile vile n.k Lengo ni kutaka kujua ukweli zaidi ili watakapotaka kufanya mabadiliko wajue wapi pa kuanzia.

kipilimba-e1491927638963.jpg

Mkurugenzi wa TISS Dkt. Modestus Kipilimba
Hata hivyo, hilo linahitaji kuungwa mkono sana na wabunge wa CCM. Njia ya pili ambayo binafsi naipenda zaidi kama njia ya haraka ni kwa wabunge wenye kuona tatizo hasa – Bashe, Ridhiwani, Zitto, na wengine wakutane pamoja na kuandaa mswaada wa pamoja (bipartisan bill) ya kuivunja Idara ya Usalama wa Taifa na kuiunda upya ikiwa imetengenezwa kukidhi mahitaji ya kiusalama ya taifa hili na ikisimamiwa moja kwa moja na Bunge. Mswada huu uletetwe hata kwa hati ya dharura ili kabla ya Bunge hili kuisha usomwe unavyohitajika na upitishwe na Bunge na hatimaye upelekwe kwa rais kwa kuudhinisha.

Nina uhakika Rais Magufuli ataridhia kwani atakuwa amesaidiwa kazi ambayo labda ingemchukua muda yeye mwenyew ekuifanya. Na kama hatoridhia na kutishia Veto Bunge linaweza kuipiku veto hiyo kwa kura nyingi na kumlazimisha aisaini na kama haitowezekana basi Bunge litavunjwa na watu watarudishwa kwenye uchaguzi mkuu mpya ambapo wananchi watapata nafasi ya kwenda kuchagua wabunge na Rais mwingine kulingana na ajenda watakazosimama nazo.

Lakini kulalamika tu wakati nyenzo wanazo ni kupoteza muda wa watu. Ni wakati wa kufanya wanachoamini ni sahihi kufanya na wana uwezo wa kukifanya. Lakini pia utakuwa ni wakati wa watu kuhesabiwa. Kwa sisi wengine ambao tumekuwa tukilalamikia idara hii kwa muda mrefu tunaona labda hii ni nafasi ya pekee ya kuileta Idara hii kwenye karne ya 21. Inapofikia watu tena wazito wanadai kuwa Idara inajihusisha au watumishi wake wanajihusisha na vitendo ovya kighaidi hakuna namna namna nyingine ya kufanya isipokuwa kuivunja idara hiyo na kuiunda upya toka chini. Mkitaka mawazo tupo wengine tunaweza kuwasaidia.

KWA KUSOMA KWA KIREFU BONYEZA ZAMAMPYA.COM

Mapendekezo yako mazuri sana na ya maana lakini unayatoa kwa taifa tofauti. Vitu kama hivyo havifanywi Afrika na wabunge wetu kama hawa na wananchi wenye maono kama ya Lizabon. Tanzania kama nchi ina muhimili mmoja tu wenye nguvu mingine ni ganga njaa. hakuna mahala popote pale penye bunge la kweli ambapo kiongozi wa serikali ama shirika la umma analigomea bunge. UK bunge lili muita tajiri mmiliki wa vyombo vya habari katika mabara matatu, Oceania, Europe na America na alienda bila kugoma. Bunge lilimuita waziri Mkuu na kumhoji na hakukataa Tanzania mkuu wa mkoa anambania pua spika wa bunge kiburi anapata wapi?

Lakini tusilaumu angalia wabunge wenyewe hawana adabu na wahuni hawakiheshimu kiti cha spika, wakati Spika ni kiongozi wa muhimili mmoja mkuu wa nchi. Hizi kelele ni bipartisan sababu zinawahusu wao ndiyo maana unazisikia kelele.
 
tulikwambia siku nyingi kuwa utachoka kumtetea bwana yule,ona unavyopata tabu kuongea,unafikiri tiss wa kibongo wanafanya mambo bila directions from up above!
 
Back
Top Bottom