Mheshimiwa Kikwete alihudhuria kwenye msiba wa Mandela na baadae kwenye mazishi. Nini maana yake Raisi kufanya safari mbili kwa tukio moja?. Obama na marais wa nchi zingine wameenda mara moja tu kule. Tanzania ni Nchi maskini kiasi kwamba haikustahili kabisa Raisi kufanya safari mara mbili kwa tukio moja. Tafsiri ndogo ya safari hizo ni ufujaji tu wa fedha za watanzania. Hata hivyo inaonyesaha washauri wa rais ni watu ambao hawako vizuri kabisa. Ikumbukwe kuwa kuna vijiji mpaka sasa havina hata kisima cha maji masafi wakati viongozi wanafanya safari za hasara. Simaanishi kuwa ni makosa kuhudhuria kwenye msiba ila kuhudhuria mara mbili nachukulia kuwa ni ufujaji wa fedha za uma. Mungu amlaze shujaa wetu wa Afrca pema peponi. Amen.