Ni vizuri kwenda kwenye msiba. Je ni busara kufanya safari mbili kwa tukio moja?.

Sengeon

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
529
0
Mheshimiwa Kikwete alihudhuria kwenye msiba wa Mandela na baadae kwenye mazishi. Nini maana yake Raisi kufanya safari mbili kwa tukio moja?. Obama na marais wa nchi zingine wameenda mara moja tu kule. Tanzania ni Nchi maskini kiasi kwamba haikustahili kabisa Raisi kufanya safari mara mbili kwa tukio moja. Tafsiri ndogo ya safari hizo ni ufujaji tu wa fedha za watanzania. Hata hivyo inaonyesaha washauri wa rais ni watu ambao hawako vizuri kabisa. Ikumbukwe kuwa kuna vijiji mpaka sasa havina hata kisima cha maji masafi wakati viongozi wanafanya safari za hasara. Simaanishi kuwa ni makosa kuhudhuria kwenye msiba ila kuhudhuria mara mbili nachukulia kuwa ni ufujaji wa fedha za uma. Mungu amlaze shujaa wetu wa Afrca pema peponi. Amen.
 
Moony

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,595
1,195
mtu kukujibu ni kuwa sawa nawe na kupoteza muda, tukuache ulivyo...
 
believer

JF-Expert Member
Dec 22, 2012
615
250
Msiba huu msilete siasa,we have a lot in common kati ya TZ na RSA,sioni tatizo Raisi kuhudhuria kikamilifu,nothing binds USA & RSA as much as we are,ni kwel una hasira na uchungu juu ya hii nchi,lkn ktk ili let the president on behalf of us(a nation)send tata madiba on his last journey.
 
masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
14,970
2,000
Mheshimiwa Kikwete alihudhuria kwenye msiba wa Mandela na baadae kwenye mazishi. Nini maana yake Raisi kufanya safari mbili kwa tukio moja?. Obama na marais wa nchi zingine wameenda mara moja tu kule. Tanzania ni Nchi maskini kiasi kwamba haikustahili kabisa Raisi kufanya safari mara mbili kwa tukio moja. Tafsiri ndogo ya safari hizo ni ufujaji tu wa fedha za watanzania. Hata hivyo inaonyesaha washauri wa rais ni watu ambao hawako vizuri kabisa. Ikumbukwe kuwa kuna vijiji mpaka sasa havina hata kisima cha maji masafi wakati viongozi wanafanya safari za hasara. Simaanishi kuwa ni makosa kuhudhuria kwenye msiba ila kuhudhuria mara mbili nachukulia kuwa ni ufujaji wa fedha za uma. Mungu amlaze shujaa wetu wa Afrca pema peponi. Amen.
Tatizo kubwa la nyie vijana wa jana ni kutojua uhusiana wa Tanzania na nchi nyingi kudini mwa Afrika.
Jisomeeni juhudi za Mwalimu na jinsi viongoxi kama Mandela, Tanzania ilikuwa kama ndugu wa damu.

Kwa mfano tu ikaja mtoa mada ukafiwa na mzazi wako, anza kujishaua shaua kwa kuingia mitini na uone wana ukoo watakapo kumaliza.
Rais wa Marekani mwenyewe kawabeba marais wastaafu lukuki kwenda karibu km 17000 kwenda na kurudi, itakuwa JK?
 
Ze mimi

Senior Member
Oct 13, 2013
128
195
We si mwafrika,maana ya kwenda msibani hujui?
Swala sio kwenda msibani ila kama alijua atahitajika awepo siku ya mazishi alikua na sababu gani ya msingi kwenda ile safari ya kwanza?Miongoni mwa nchi ambazo hazikuhudhulia mazishi ya Madiba ni Israel kwa kukosa fedha kwa ajiri ya safari,hii haimaanishi kwamba Israel ni nchi maskini lahasha ila hawakua na fedha zisizokua na malengo maalumu sasa iweje nchi kama Tz kufanya safari mbilimbili kwa tukio moja?Hii ni aibu sana kwa viongozi wanaojua hasa nini naana ya fedha za umma,hii inaashiria kwa kiwango kikubwa kabisa ni namna gani viongozi wetu wasivyojali umaskini wa walipa kodi ambao ni sisi wananchi kwa kuchezea fedha zetu bila hata huruma wakituacha kukifa na umaskini kwa ajiri ya kunyonywa jasho letu.Hivi hawa wanaoitwa washauri wa Rais wanauchungu na nchi hii?Maana hawa ndio wamekua wakimpotosha Rais mara zote kwa maslahi yao binafsi huku wakimuacha Rais akionekana ndiye mwenye makosa.
Mungu ibariki Afrika,Mungu ibariki Tanzania.
 
Ahsante kwa ufafanuzi mkuu.
 
Rover Rider

Member
Nov 18, 2013
67
95
mtu kukujibu ni kuwa sawa nawe na kupoteza muda, tukuache ulivyo...

Jibu swal ww mbulula. au kisa unalishwa na kuvishwa na baba'ako aliye CCM ndo unaona kila kitu poa poa.? Kuna watu wana shida ya maji, umeme na ata chakula. ww huwez kuona uchungu sabab hujapitia uko. Ubongo wako una carbon mpaka uende India ukausugue na msasa ndo uta-thnk straight.
 
Gwangambo

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
3,641
1,225
Tatizo kubwa la nyie vijana wa jana ni kutojua uhusiana wa Tanzania na nchi nyingi kudini mwa Afrika.
Jisomeeni juhudi za Mwalimu na jinsi viongoxi kama Mandela, Tanzania ilikuwa kama ndugu wa damu.

Kwa mfano tu ikaja mtoa mada ukafiwa na mzazi wako, anza kujishaua shaua kwa kuingia mitini na uone wana ukoo watakapo kumaliza.
Rais wa Marekani mwenyewe kawabeba marais wastaafu lukuki kwenda karibu km 17000 kwenda na kurudi, itakuwa JK?

Duuh!Mkuu una mafua? au viloba jogoo mixer na K-Vant na miraa? Ulinkafu ughwe?
 
Gwangambo

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
3,641
1,225
Mheshimiwa Kikwete alihudhuria kwenye msiba wa Mandela na baadae kwenye mazishi. Nini maana yake Raisi kufanya safari mbili kwa tukio moja?. Obama na marais wa nchi zingine wameenda mara moja tu kule. Tanzania ni Nchi maskini kiasi kwamba haikustahili kabisa Raisi kufanya safari mara mbili kwa tukio moja. Tafsiri ndogo ya safari hizo ni ufujaji tu wa fedha za watanzania. Hata hivyo inaonyesaha washauri wa rais ni watu ambao hawako vizuri kabisa. Ikumbukwe kuwa kuna vijiji mpaka sasa havina hata kisima cha maji masafi wakati viongozi wanafanya safari za hasara. Simaanishi kuwa ni makosa kuhudhuria kwenye msiba ila kuhudhuria mara mbili nachukulia kuwa ni ufujaji wa fedha za uma. Mungu amlaze shujaa wetu wa Afrca pema peponi. Amen.
Kweli wewe ni Senge-on kama ID yako, you better be Senge-off kama huna hoja.
 
mzaramo

JF-Expert Member
Sep 4, 2006
6,340
2,000
uhusiano wa tanzania na south africa ni tofauti na uhusiano wa south africa na israel au south africa na marekani....kama raisi ratiba inamruhusu hakuna tatizo katika hilo kwetu waafrica kushiriki msiba wa jirani yako ni zaidi ya utu na wema...usilete siasa msibani
 
Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,372
2,000
Hoja yako si ya msingi sana..

Kuna mambo huwa utu unatangulizwa kwanza halafu gharama zinafuata...

Labda kama ungejenga hoja kwa kuleta mchanganuo ni kiasi gani cha fedha kimetumika katika safari hizo na ni shilingi ngapi zingeokolewa kwa kukatisha safari moja..

Otherwise pesa isiwe kipimo cha utu
 
Jino Kwajino

Senior Member
Dec 22, 2012
191
0
Ni ufujaji wa mali za umma huo asiependa anyamaze tu ila asitetee upuuzi kama huu. Laiti Mandela angefufuka angemrudisha kikwete na angemuonya juu ya safari hizo kama alivyowahi kukataa kufungua hoteli ya kifisadi ya akina BWM.
 
Sengeon

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
529
0
Hoja yako si ya msingi sana..

Kuna mambo huwa utu unatangulizwa kwanza halafu gharama zinafuata...

Labda kama ungejenga hoja kwa kuleta mchanganuo ni kiasi gani cha fedha kimetumika katika safari hizo na ni shilingi ngapi zingeokolewa kwa kukatisha safari moja..

Otherwise pesa isiwe kipimo cha utu

Kwa sababu wewe ndie uko karibu na wafujaji wa fedha za serikali, Tunaomba utupe bei ya safari moja kwenda S. Africa kwa private Jet.
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,070
2,000
nyie watoto kasomeni historia. naunga mkono jk kwenda kwenye msiba wa mandela.

msiangalia kwa nini obama au cameron hawajarud tena. mandela alikuwa kwenye list yao ya magaidi adi mwaka 2008 walipolitoa.

uyo cameron mwaka 1985 akiwa kiongoz wa chama kijana wakat huo aliongoza maandamano mandela anyongwe na alivaa tshirt imeandikwa mandela anyongwe.

msishabikie ujinga
 
vegas

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,043
2,000
Jibu swali je ni busara kufanya safari mbili kwa tukio moja.

siyo busara kabisa, kama ikulu ilipanga rais atahudhuria mazishi ile safari ya kwanza isinge kwepo, ndiyo maana wenzake wanaojali muda na kodi za wananchi wao walienda mara mmoja tu
 
Kashi

JF-Expert Member
Jan 6, 2013
812
1,000
uhusiano wa tanzania na south africa ni tofauti na uhusiano wa south africa na israel au south africa na marekani....kama raisi ratiba inamruhusu hakuna tatizo katika hilo kwetu waafrica kushiriki msiba wa jirani yako ni zaidi ya utu na wema...usilete siasa msibani

Kumbuka kuwa bajeti ya safari za viongozi wa nchi ilishamalizika miezi miwili tu baada ya kuanza kutumika kwa mwaka 2013/2014.
 
Ntakasi

JF-Expert Member
Oct 21, 2013
1,427
1,195
Mweeeeh....hakuna ulazima wa maswali mengine ila ndio hivyo....Mdomo haulipiwi kodi atiiiii....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom