Ni vituko gani ulishawahi kufanyiwa na mwenye nyumba wako hadi ukatamani uhame uache Kodi?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,947
10,813
Nakumbuka miaka hiyo ndio nimepata kazi benki Fulani, nikapata nyumba Sinza ya mama mtu mzima kijana.

Akanikaribisha sana, hakuwa na noma, nilipokuja kununua flat TV enzi hizo plasma tv ndio zimetoka, hamna cha LCD na LED ni ndoto kabisa, yaani ndio kwanza watu wachache sana tumeamza kujikwamua kutoka kwenye machogo.

Basi yule mama akawa anataka muda wote aje ashinde ghetto kwangu, anavaa nguo very light.

Kuna siku jumamosi nimemaliza kufua, nikasema Leo nijilipie, nikachukua Konyagi kubwa, nikawa na Dodoma wine, kwenye oven kilo mbili za kitimoto zinaokwa taratibu. Mara ghafla mlango unagongwa huku mtu akiingia ndani bila kukaribishwa.

Nilikuwa Niko na boksa tu sikuwa natarajia mgeni, akaniudhi sana. Nikakimbilia taulo, akanifuata akanivua taulo. Nikasimama wima hasira Imenijaa.

Akaanza kujiliza ohh Mimi nakupenda siku zote, wewe unajidai huoni.

Nikamkaripia nikamwambia anikome. Baada ya hapo alianza chuki na visa, nilikaa miezi minne tu nikahama.
 
Mimi na wasela wenzangu enzi hizo tuko form six, katika kujiandaa tukaona ni vyema tupange chumba ili tuweke Kambi ya masomo.

Usiku mmoja nikashtuka usingizini, tukamuona baba mwenye nyumba na mkewe na watoto wako uchi wa mnyama wanaizunguka nyumba.

Nikawaamsha wenzangu. Chumbani kuna Giza hatujawasha taa hivyo tunawaona kwa uzuri sana.

Baada ya wiki tu tukahama. Walikuwa Wana roho nzuri sana utadhani watu kumbe ni mashetani
 
Alikunywa mataptap then akaweka balimi juu, akashikilia nyingine mbili akaja kunidai kodi kabla mda haujafika, na kwa bahati nzuri akatapika ndani kwangu, then bia moja ikaanguka ikapasuka... We we we siku hiyo nilimpiga bhn hatokaa asahau, nilimpiga kama mke wangu na kudeki akadeki usiku kucha.

Kesho yake wakaniita na mke wake wakasema nitafute chumba kingine nikaomba wanipe wiki ili nijipange, ndani ya hiyo wiki wakapata tatizo ñikawasaidia, wakaniita wakaomba msamaha na kunisihi nisihame, kwamba mi ni kijana mwema na kwa siku hiyo Mzee mwenye nyumba alikosea ndo maana nkachukua hatua hiyo. Nkasema poa, nkaendelea kuishi pale mpaka nilivyojipata.​
 
Nikiwa chuo mwaka wa tatu nilipangisha sehemu nzuri tu enzi hizo nyota imekubali vijisenti nnavyo, nkaanza kumla mtoto wa mama mwenye nyumba, shida nilikuwa napiga mzigo bila huruma. Mama mwenye nyumba akanipenda na kunipa pia kinapiga. Nlipokuja kugundua ni mtu na mwanae nilihama kimya jumapili usiku hata kodi ya miezi mitatu sikuitisha.
 
Nyumba nyingine nilihama sababu ya mtoto wa mwenye nyumba. Ni mdogo 13 years ananiambia uncle nakupenda nataka uwe my boyfriend. Si unajua hivi vitoto vya English Medium.

Nikaona hapa siku sio nyingi nitaitwa mbakaji. Katoto kuna siku kamekuja ghetto, kanajichekesha chekesha tu, nikakauliza Jacqueline how can I help you? Kakajibu nothing, just close the with a key, I want to sleep with you.

Aisee akili ikaniruka nikasema huyu Mzee wa Kichagga kamtuma mwanawe ili nitolewe kafara?

Kimbembe ikawa namna ya kukaondoa chumbani bila ya kukatimizia ndoto yake.

Nikakapa 10,000 nikakaambia kakalete soda baridi sana tuwe tunakunywa kabla hatujalala.

Kalipotoka, nikafunga mlango nikaondoka nikaanza kurudi usiku mkali,.Hadi nilipopata nyumba ya kuhamia
 
Chemba ya choo inajaa kila baada ya wiki 3 hadi 4, kuna siku nyoka akapanda na sink la choo tena nikiwa nataka kukata gogo 😂.
Dah sijui angenidunga ningefunga wapi.

Ukimwambia mwenye nyumba anasema kesho mafundi wanakuja, hawaji na miezi inakatika, nikaona hapa bora nihame. Nikaacha kodi ya miezi 4.
 
Chemba ya choo inajaa kila baada ya wiki 3 hadi 4, kuna siku nyoka akapanda na sink la choo tena nikiwa nataka kukata gogo 😂.
Dah sijui angenidunga ningefunga wapi.

Ukimwambia mwenye nyumba anasema kesho mafundi wanakuja, hawaji na miezi inakatika, nikaona hapa bora nihame. Nikaacha kodi ya miezi 4.
Ungefunga saba kavu
 
Dah sio powa mwanangu ile nyumba ni nzuri sana ila🙌.

Niliishi Kwa miaka miwili bila shida yoyote ghafla tu mwaka wa tatu nikiwa pale shida zikaanza. Kuna matukio matatu yanilitokea
1.Usiku nimezima taa nilale ghafla naona mtu anapita kwenye Kona ya kitanda anaelekea konani nikajua wenge la usingizi nikapotezea,night nipo kwenye usingizi nasikia sufuria zangu zinafunuliwa mezani ukiwasha tochi au taa hausikii kitu ukizima harakati zinaendelea.
2.Niliamka saa 10 usiku kuoga ili niwahi lindo ile natoka nje nakutana na watu wawili wamekaa katikati ya uwanja tunaangaliana mwili ulisisimka kinoma
3.Nilikuta vitu ambavyo sivielewi vimemwagwa mlangoni kwangu yani kitu kama damu/dawa za kienyeji.
Hili tukio la tatu ndio lilinifanya nisepe kabisa pale na hii ni baada ya kuongea vizuri na wazee wa mtaani na kunipa historia kamili ya ile nyumba Kwa undani.
Na kila mpangaji alikua alikutana na vituko vya aina tofauti tofauti Kuna dada mmoja alikua anakuta kinyesi Cha binadamu katikati ya kitanda.
Hali hii imenifundisha kutafuta taarifa muhimu ya sehemu unayotaka kuamia kabla ya kulipa kodi na kuanza kuishi.
Hiyo picha inaonesha kitu nilichokuta kimemwagwa mlangoni
 

Attachments

  • IMG_20240113_055134_279.jpg
    IMG_20240113_055134_279.jpg
    2.1 MB · Views: 5
Maji ya mgao, siku yakitoka wapangaji haturuhusiwi kuchota maji bombani. Mwenye nyumba anajaza tank then anatuuzia ndoo 200, nikaona hapa sipaswi kukaa hata miezi miwili
Hii nadhani ni njia napaswa kuifuata, kuna demu kapanga kwangu ila pesa analipiwa na sponsor, sasa huyu kwenye bill ya maji halipi kabisa, nikimforwadia msg unit tumitumia hizi mimi nalipa 80% wewe malizia basi hapo zitakuja hata bill 3 hajalipa, ni mtihani kwakweli.

Kwahiyo hapa msiwashitumu wenye nyumba hata wapangaji wengine ni vichomi tu.

Nadhani biashara sahihi ya nyumba wakae wapangaji tupu na mwenye nyumba ukae kwenye nyumba yako peke yako unakusanya kodi tu, asiyelipa maji wacha akatiwe tu na usiponunuwa luku utalala mwenyewe gizani.
 
Back
Top Bottom