Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,996
Mh Mnyika,
Nashukuru kwa majibu yako mazuri lakini nasikitika baadhi ya ahadi zako unazikana...anyway kama ujasema wakati wa kampeni zako za ubunge kuwa utaleta maji pamoja na kujenga barabara ndio tabia za wana siasa kuyakana maneno yao!
Sikukuu njema Mh Mnyika
Mh.Ruge ni Al shaabab nasikia, wana jf mnijuze vizuri katika hili.....!
Sijui kwa nini ukiwa Chadema na akili zinahama!Kama kawaida yako, ulikurupuka kuandika kwa akili yenu magamba kuahidi vitu msivyovijua! Sasa umejibiwa na kuelekezwa unaanza kujing'atang'ata kama demu wa kijijini anayetongozwa.
Nenda kamkumbushe kikwete zile ahadi zaidi ya sabini ataanza lini kuzitekeleza, maana mwaka ndo umekwisha na hatuoni kinachoendelea!
Wapinzani wao kazi yao kubwa ni kupinga kila kitu.
Sijui kwa nini ukiwa Chadema na akili zinahama!
Wewe unamuona Mnyika ni Mtume kila anachosema ni kweli, tumia akili yako wakati mwingine hata kama una ubongo mdogo kama wa sisimizi.
Mbona kashindwa kusema ahadi alizohaidi na kuishia kusema ahadi zingine sikusema zipi sasa alizosema kazifanyia kazi?
Nimemwambia ni kawaida yao wana siasa kuyakana maneno yao!
Tumeona hata Lema kule Arusha kakana kuwa akusema kama atajenga Machinga Complex mbili na barabara za juu..
Dr Slaa, nae alisema Chadema wakichukuwa nchi saruji itauzwa mfuko mmoja Sh5000, saizi ukimuliza atakana.
Ilo la mwanake wa kijijini siwezi kulitolea ufafanuzi sababu mimi sijazaliwa kijijini nimezaliwa mjini.
Pale karibia na Ikulu
Wana jf nisidieni huenda mm siijui vizuri sheria niliwahi kusikia ukishitakiwa huruhusiwi kugombea uongozi huyu Rage si alishatumikia kifungo ukonga alipataje nafasi ikiwa alishawahi kufungwa?Wananchi wazalendo ni lazima watumie muda mwingi kuhakikisha kuwa mchakato wa kupata katiba mpya ya nchi yetu hauchakachuliwi, kuepuka kupata katiba ambayo haitakidhi matakwa ya wengi!! Katiba mpya ikipatikana kero nyingi za wananchi zitatatuliwa kirahisi; kwa mfano mamlaka ya Rais kuteua watu kwenye nafasi nyeti kumbe ni mafisadi ambao vitendo vyao vinaongeza umasikin kwa wananchi, mamlaka hayo ya uteuzi yakithibitiwa na bunge upuuzi wa kuwapa vyeo maswahiba wa rais wasiowaadilifu utakwisha na hivyo kuwapunguzia machungu wananchi.
Asante sana mheshimia maana huyu Ritz huwa anamatatizo ya kufikiri. Asante kwa kumjibuRitz,
Asante kwa maoni yako. Hata hivyo umetaja ahadi nyingine ambazo zijawahi kuzitoa wakati wowote kwenye kampeni zangu popote. Sijawahi kuahidi machinga complex mbili, kwa sababu naamini kwenye uzalishaji na huduma zaidi ya uchuuji. Tandale haipo katika jimbo la Ubungo, ipo Jimbo la Kinondoni; hivyo ahadi uliyoitaja sijawahi kuitoa. Kuhusu maji, barabara na ajira; ahadi zangu zilikuwa tofauti na ulivyozieleza; kwa kuwa naelewa vizuri kuwa kazi ya mbunge ni kuwakilisha, kuisimamia serikali na kutunga sheria. Ahadi zangu wakati wa kampeni niliziandika kwa ajili ya rejea kwa sababu niliamini ni mkataba baina yangu na wapiga kura. Mara baada ya kuchaguliwa nilizirudia hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/91961-ujumbe-wa-mbunge-shukrani-twende-kazi.html wakati wa kuwashukuru ili kuunganisha nguvu ya umma katika utekelezaji na pia upatikane msingi wa kupima utekelezaji wa ahadi husika katika kipindi cha miaka mitano. Kwa mwaka huu wa kwanza nimekuwa na utaratibu wa mara kwa mara kutoa mrejesho wa masuala mahususi, unaweza kufanya rejea tu humu. Lakini kwa kuwa tunaelekea mwisho wa mwaka nitatoa pia taarifa nyingine ya ujumla; na pia nitaelekeza zitolewe taarifa za kata kwa kata. Nakutakia heri ya Xmas na mwaka mpya na tuendelee kushirikiana katika utumishi wa umma.
JJ
Ritz una akili kweli, mbona unalazimisha vitu ambavyo havipo, umepewa sehemu ya kufuatilia ahadi na jinsi zinavyotekelezwa bado unabishana, hivi ninyi pro-CCM mtaacha lini ushabiki maandazi, kazi kushabikia lichama zee linalokaribia kujifia, shame on you.Mh Mnyika,
Nashukuru kwa majibu yako mazuri lakini nasikitika baadhi ya ahadi zako unazikana...anyway kama ujasema wakati wa kampeni zako za ubunge kuwa utaleta maji pamoja na kujenga barabara ndio tabia za wana siasa kuyakana maneno yao!
Sikukuu njema Mh Mnyika
ritz naomba unitajie ahadi alizotekeleza Rage na Kikwete wake. Nakushauri uendekumsaidia mzee Mohamed Saidi kuhubiri chuki dhidi ya Nyerere hilo nimuafaka kwa ubongo wakoNaomba mwana Chadma yoyote humu JF anitajie ahadi alizotekeleza John Mnyika, tunakumbuka sana wakati wa kampeni maneno yake!