Ni vita kati ya "Serikali" ya CCM na "nchi"

Ni vita kati ya "Serikali" ya CCM na "nchi"

Matendo mabaya humtafuna mhusika siku zote!
Matendo ya ccm ya SSH yameanza kumtafuna!
Alianza vyema kabisa huyu mama yetu, hapa kati kakutana na 'makuwadi' wa raslimali za Taifa ndio wamemuingiza chaka! Bora angefanya haraka kuachana nao.
Hili la bandari haliwezi kumuacha hadi akiamua kulirekebisha
Wanamdanganya ashinde kesi leo, aitumie kusema hata MAHAKAMA imeamua!

Hili haliishi kwa hila, litawarudia
 
Kwa hiyo unachochea uhaini? Wale jamaa wapima mkojo bado wapo.
Hapana ndugu! Sichochei...au tuendelee kutumia sanduku la kura tu? Maana naona uchaguzi wa 2020 watanzania walichagua mbunge mmoja tu waupinzani kutoka Nkasi.
 
Muvi ya kutisha na kuchosha.
Kama igizo lakini ni kweli.

Niwaambie kitu ambacho wengi hamkijui?!

Mlishajiuliza, ni kwa nini serikali ya Mh. Rais Samia iliamua kufuta vipande vya hotuba za Baba wa Taifa, katika Television na Radio zote?

Kachunguzeni, Mwinyi wala Mkapa hawakudiriki kuzuia, Kikwete wala JPM vilevile hawakuzuia hizo hotuba, ni kwa nini sasa, kwa Samia?!

Serikali ya CCM imeamua liwalo na liwe, inapambana na "nchi".

Haina tena simile wala soni,
Imeshamaliza kupambana karibia na kila mtu, sasa inapambana na nchi.

Sasa CCM imeamua kukodisha vikosi vya maangamizi ili kuishinda hii vita.
CCM imekodisha kombora la 'UDINI', UCHAWA, UKUNGUNI, UOGA, VITISHO, UJINGA, RUSHWA, UNAFIKI,, n.k ili kuimaliza kabisa nchi.

Ikifikia hatua sheria na kanuni za nchi zinabadilishwa ili kumgawia mtu rasilimali na maliasili mbalimbali, ujue serikali inapigana na nchi.

View attachment 2713238
Kwa kuwa wewe ni Mwanaccm Mwenzo basi naweza kuamini haya.
 
Hivi hamna kazi za kufanya nyie!?
Unapata vipi muda wa kukaa na kutunga insha ndefu ndefu hv!
Au ndio kazi yako inayokupatia mkate wa siku?
Tunaumia kuona kazi ya baba zetu kujikomboa nchi inaharibiwa na watu wachache waliopoka madaraka ya nchi
 
Back
Top Bottom