Ni vema mshahara wake uwe mkubwa potelea mbali


mansakankanmusa

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Messages
4,193
Likes
662
Points
280
mansakankanmusa

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2010
4,193 662 280
mwalimu ananyanyaswa sana,

unyayasaji wake hauko kwenye chochote zaidi ya dharau anayofanyiwa, kebehi anazopewa, haki yake inavyopokwa

binafsi kwa ufahamu wangu, ni kwamba mshahara wa mwalimu unalingana au kuzidi chenchi kidogo za watumishi wengine, sometime sh12,000 range, 20000 nk

Tatizo ni ukweli kwamba, katika kada zingine wanatoa house allowance, transport nk

kwa upande wake mwalimu amechoshwa na adha ya nyumba za kupanga na gharama za nauli kila siku, na yeye kwa kawaida ndie anaesoma sana vitabu na majarida, je unajua kwamba ni mwalimu kila siku anaongea na waandishi, madokta, maprofesa waandishi mbalimbali hivyo yeye kuwa wa kwanza kuwa na upeo wakila kinachoendelea duniani?

Kama ambavyo enzi hizi za electronic kila kitu kimebadilika, haiwekani hata kama naenda kilometa moja watu wote wamepanda bodaboda mwalimu anashindwa kusimamisha pikipiki nae aonekane hana dhiki, ni afadhali basi awe amepaki bajaji yake nyu,bani hata akitembea anajipa moyo kuwa '"si ninayo nyumbani" walau anajipa kyo huo/

Kwa upeo mpana, Taifa lazima liangamie kwa kuwa misingi ya elimu ni mibaya, na wadau wengine wanatumia nafasi zao kuwakandamiza ama kwa kuwapa kisogo au kukebehi, hata kukaa kimya ni kebehi.

Mwalimu wa Tanzania anachangamoyo nyingi sana, bahati mbaya zaidi idadi kubwa ya raia milioni 40 ipo mikononi mwake. Ndie atatakiwa awaingize watoto katika electronic era, huyo huyo anatakiwa akae na watoto muda urefu kwa siku masaa yasiopungua nane ili watoto wasiende majiani/mtaani kulikojaa uhuni/matusi/uhalifu/facebook/nk kwani mwalimu akikaa muda mrefu na watoto wenu atampa mtoto huyo skills za maisha. Nionavy mm ni vema mshahara wake uwe mkubwa potelea mbali, na hakika wakiweka ile 50% au hata hiyo 30% mshahara utapaa, japo kidogo. Ona sasa mnashangaa, nini? hamjui watoto kutokaa na mwalimu muda wa kutosha ndio kosa kubwa? na unadhani akikaa na mwanao akiwa hana pesa, hana uhakika wa kodi, usafir mwanao atapona kweli?

naishauri serikali, ifanye hivyo hata kwa nguvu na mamlaka ya Mh Raisi afanye maamuzi na bila kujali kitu.
Wanasiasa wenye dira ya mbali na hasa matajiri, wanatumia nafasi hii uhakikisha hii population ya watu wasiopungua mil40 wanaangamia kwani ndiyo silaha ya kutetea watoto wao mika 20 ijayo katika nchi iliyojaa mambumbu, kwani hawatajua haki zao. wataishi maisha ya kubahatisha sana na itafanana na The barbaric invasions in Europe - Romanity

Mimi hata kama nitakufa leo, na kama mungu yupo amesikia, na atasema wewe mansakankanmusa umefanya sehemu yako, ingawa WW si mwalimu. Hawa watu wote hawa milion 40 wataishi maisha ya dhiki sana.


mwisho kwa leo.


source: JF mansakankanmusa mwenyewe, tarehe 13/6/2013
 

Forum statistics

Threads 1,273,879
Members 490,535
Posts 30,494,902