Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Tofauti na mwaka 2025 wakati kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu imeanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na baadaye Mahakama Kuu jijini humo, mwaka 2026 kesi hiyo imeanza bila vitendo vya ukatili wa polisi kwa wafuasi wa chama hicho wanaohudhuria.
Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma na kusafirishwa hadi Dar es Salaam, ambapo Aprili 10, 2025 alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kufunguliwa mashitaka ya uhaini.
Awali mwaka 2025, ulinzi mkali ulishuhudiwa Mahakamani, watu kupigwa, wengine wakikamatwa kwa sababu tu ya kuhudhuria kesi ya kiongozi wao.
Tunakumbuka tukio la Aprili 25, 2025 ambapo wanachama na viongozi wa chama hicho walikamatwa na kupigwa kisha wakaenda kutupwa Mabwepande nje kidogo ya Dar es Salaam na wengine wakatupwa wilayani Bagamoto mkoa wa Pwani.
Tukio lingine ni la kukamatwa kwa wanasiasa na wanaharakati walioka nchini Kenya na Uganda kuja kushuhudia kesi hiyo, Mei 18, 2025.
Baadhi yao akiwamo mwanasiasa Martha Karua na Jaji Mkuu wa zamani wa Kenya, Dkt. Willy Mutunga walirudishiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JKIA) mara baada ya kutua jijini Dar es Salaam.
Wanaharakati wengine akiwamo Agatha Atuahire kutoka Uganda na Francis Mwangi kutoka Kenya waliokuwa wameingia nchini walikamatwa wakiwa hotelini na watu wanaodaiwa kuwa ni polisi na baada ya siku mbili walisafirishwa hadi mipaka ya nchi zao, ambapo baadaye walisimulia ukatili mkali waliofanyiwa.
Manyanyaso yaliendelea hata kesi ilipofikishwa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, ambapo wafuasi wa CHADEMA walipigwa, walitwezwa na wengine kukamatwa. Tukio moja wapo ni lile la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa BAVICHA na wakili Deogratius Mahinyila, huku wafuasi wengine wakipokea kipigo kikali mbele ya mahakama hiyo.
Lakini tangu kesi hiyo ianze tena Februari 9, 2026 utendaji wa polisi umebadilika, kwani ule ulinzi mkali uliokuwepo awali sasa umepunguzwa. Yale manyanyaso kwa wafuasi wa CHADEMA hayapo tena.
Mahudhurio ni makubwa yakihusisha wafuasi wa chama hicho, wafuasi wa vyama vingine, wanasheria, wanandugu na wapenzi wa chama hicho. Hakuna bugdha yoyote iliyoshuhudiwa tena.
Kwa hali hiyo, Je, Jeshi la Polisi lina hofu ya kutokea matukio kama ya Oktoba 29, 2025, ambapo watu walishambuliwa, wengine kuuawa na wengine kujeruhiwa? Je, jeshi hilo limeamua kubadilika kabisa, au wamejifunza kwamba inawezekana kuepuka ukatili na bado mambo yaende vizuri?