Jindal Singh
JF-Expert Member
- Sep 9, 2015
- 1,857
- 1,543
Na Ahmad Ali
Aliyekuwa mwana CCM mkongwe, Edward Lowassa, ndieatakaepeperusha bendera ya UKAWA kupitia chama cha Chadema katika kinyang'anyiro cha urais mwezi wa Oktoba 2015.
Chama pinzani Chadema kimebariki mapokezi ya Edward Lowassa kutokea CCM na kumpatia fursa ya kugombea urais kupitia chama hicho, na hatimaye UKAWA kutia saini ya makubaliano hayo. Kejeli na kashfa za ufisadi ambazo upinzani walikuwa wakizitoa dhidi ya Lowasa kumbe ilikuwa ni debe tupu bila ya kuwa na ukweli wowote. Na huu ndio uhalisia wa demokrasia.
Baada ya uteuzi wa CCM uliofuatiliziwa na kumpata mgombea urais kupitia chama hicho, ambapo matokeo yake yaliwastaajabisha wengi katika chama tawala pamoja na upinzani, kufuatia John Magufuli kuibuka mshindi wakupeperusha bendera ya CCM katika kinyang'anyiro cha urais mwezioktoba Huku matarajio ya wengi yakidharauliwa na kupuuzwa kwa kiasi kikubwakatika uteuzi huo mpaka kupelekea baadhi ya wanachama wa CCM kurudisha kadi na kujitoa moja kwa moja ndani ya chama. Lowassa na Benard Membe ndio yaliyokuwa matarajio ya wengi katikamchuano wa kinyang'anyiro cha urais kwa kupitia tiketi ya CCM.
Matarajio haya ya wengi chini ya kisingizio cha demokrasia yalimalizwa na kusambaratishwa bila huruma kwa nguvu na mabavu. Wengiwalishindwa kuelewa kwamba ubepari au maslahi ya kiuchumi ndio yanayo kuwa mbele kuliko maslahi ya kisiasa au kidemokrasia. Kipimo cha maamuzi ya kufanya jambo au kuachakufanya ni faida na hasara , hii ni kwa mujibu wa mfumo huu mchafu wa kidemokrasia. Hivyo ni ngumu kusikilizwa maamuzi ya wengi ikiwaitasababisha kupotea kwa maslahi ya mabwana wakubwa wakoloni pamoja na vibaraka wao.
Mtikisiko wa uteuzindani ya CCM ulikuwa ni wa kukata na shoka baina ya kambi mbili. Kambi ya Marekani na kambi ya Mwingireza. Na hizi ndio kambi mbili kuu zinazoikondesha CCM, na huu ndio mpasuko wa kikweli ndani ya CCM.
Na mpaka sasa kambi ya Mwamerika ndio kambi yenyemakali na ndio iliyoibuka na ushindi ndani ya uteuzihuo na kumuacha Mwingereza kwenye mataa na mipango yake mbadala.
Kambi ya Mwamerika imefanikiwa kushinda katika chaguzi hizo licha ya kuwa makusudio yake hayakuwa kwa John Magufuli , lakini imekuwa hivyo kutokana na mipango na mashambulizi makali kutoka kambi ya Mwingereza ambayo ilijipanga kisawasawa kuhakikisha koloni linarudi kwa bwana mkubwa wa asili Mwingereza, kwani hapo mwanzo lilikuwa mikononi mwake lakini Mwamerikaakamfanyia mapinduzi ya kisiasa na kulitia mikononi mwake.
Mwingereza ameshindwa kulirudisha koloni lake la asili kwa kumtumia Lowasa ndani ya CCM. Lakini bado hajakata tamaa anajaribu kuitupa tena karata yake hii ndani ya Chadema kwa jahazi la UKAWA kwa kumtumia mtuwake yuleyule Edward Lowassa. Na hii ni kutokana na kuelewa Mwingereza kwambamtuwake huyu anavyokubalika katika jamii, na kuona matarajio ya karibu katika kurejesha koloni lake.
Chadema ambacho ni chama chaMwingereza kimempokea mwanakambi mwenzao Edward Lowassa na kumvisha joho la kugombea urais bila hata ya kuona haya kwa kejeli na kashafa za ufisadi walizokuwa wakimshutumu nazoawali kwa siri na kwa dhahiri. Vinywa vyao vimefyata kabisa ,haya na fedheha zimewafika kwa sababu ya maslahi ya urais 10/2015. Hiki kipimo cha kimaslahi ndicho watakachoendeleanacho mpaka hata itakapo hakikishika ndoto yao ya Urais.
Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza ya Rais Kikwete , mnamo mwezi februari/2008 alijiuzulu rasmi kwa kulazimishwa kuachia ngazi ya kiti cha uwaziri mkuu kuinusuru serikali ya Kikwete kufuatia kashfa ya sakata la Richmond.
Hakika ya mambo ni kwamba huu ulikuwa usaliti wa wazi dhidi ya Lowasa. Nakuanzia hapo karata hii ya mwingereza ilielewa rasmi kwamba imeshasalitiwa dhidi ya mipango ya kuwa raisi katika awamu ijayo. Kutokea hapo na kuendelea mpaka sasa takriban miaka sita Lowasa alikuwa katika maandalizi mazito ya ndani ya chama na nje ya chama kwaajili ya kampeni ya uraisi mwaka wa2015.
Sio hali ya kushangaza hata kidogo kuonekana mtu huyu akipendwa na wengi, kwa kuwa ametumia miaka mingi kufanya kampeni tena huku akishirikiana nabaadhiya wakongwe wa chama cha CCM kama vile akina Kingunge nk. Hivyo kama sio kutumika mabavu katika uteuzi uliofanyika ndani ya CCM basi Lowasa leo angekuwa mpeperushaji wa bendera ya CCM katika kuwania uraisi mwezi oktoba2015.
Zimetumika nguvu nyingi mno zilizofuatiliziwa na mikakati ya hali ya juu katika kumtengeneza na kumnadi Lowassa kwa urais mwaka 2015 kupitia teketi ya CCM. Lakini kwa bahati mbaya matarajio hayakuwa.
Hata hivyo, Mwingereza hayuko tayari kuona nguvu zake hizi zikipotea bure bila mafanikio yoyote, na badala yake ameamua kuitupa tena uwanjani karata yake hii kupitia chama chake cha kikoloni cha Chadema na hatimae kupeperusha bendera ya UKAWA.
CUF ndani ya ndoa ya UKAWA ni chama kilichosimama kwa ajili ya kuchunga maslahi ya Mwamerika, chama hichi kamakilivy CCM kipo nyuma ya Mwamerika , kikifanya kazi na Chadema bega kwa bega ili kuchunguza mikakati yote ya Mwingereza inayopangwa kupitia Chadema.
Mwamerika anapanga namna ya kulidhibiti koloni lake na huku Mwingereza anapanga namna ya kulirudisha koloni lakelaasili mikononi mwake. Hakika ya mambo ni kwamba huu ni mpambano mkali wa wa kisiasa wa kukatana shoka kati ya Marekani Uingereza.