Ni tukio gani lilikupata ukikumbuka unacheka tu?

Mtuache

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
251
638
Nakumbuka miaka fulani maisha yalinipiga chenga mbaya mbovu, boksi langu lilikuwa gumu utasema ni vault za kuhifadhia dhahabu. Sasa siku moja mchumba akanicheki akadai amenimiss niende kwake tukaonane. Mzee nikajipiga search sina kitu, hapo naishi Segerea mchumba yupo Kawe.

Nikamfata mwanangu aliyekuwaga msaada wangu kinoma kipindi hicho kumuelezea shida yangu na kumuomba anipe hata nauli mwana akasema hana. Daah nilichoka!

Huku mtoto ananiuliza naenda saa ngapi, huku hata nauli sina. Nikapiga hesabu zangu wee, nikaona hata isiwe kinyonge chaaap nikajiandaa mosi mosi nikaanza kutembea. Nilipiga hamza kanuni kutokea Segerea mpaka Kawe hapo hata sikuwa nimekula.

Kufika Ubungo njaa ilikuwa inauma vibaya mno ila maji nishayavulia nguo. Mchumba nikamwambia foleni inazingua ila nafika siyo muda. Twaa twaa Mwenge hii hapa, nikanyoosha huku na huku nikaingia Kawe njaa inauma hadi inaumiza.

Kufika geto kwa mtoto nikavunga kama kitu kimenipata, story zikaanza "Ooh nimekumiss sana nikajua huji", mimi akili hata haisomi njaa inauma hata simuelewi anachozungumza. Naona anabweka tu wuu wuu wuuuu. Mtoto akaanza kunitomasa, touch za hapa na pale lakini waaapii mashine imelala yooo. Guswa kila kona mzigo unasoma 2G.

"Kheeeee kulikoni?" Akaniuliza

Ikabidi mamaa aulize vipi kulikoni? Sindo nikampa story, daah alisikitika sana kidogo alie. Akanilaumu mbona sikumwambia? Nikamwambia lawama zisiwe mingi kama unaweza nisadia sasa hivi fanya hivyo nile, hapo sura iko serious sicheki na nyani.. ah sorry sorry sorry sorry baby wangu siyo nyani. Hapo sura iko serious sicheki na baby.

Ndiyo akaingia jikoni akabandika uji halafu akaenda kufata chipsi. Kurudi uji ushaiva nikapewa ninywe, halafu nikazila na chips. Kipindi nakula kiepe yeye alikuwa anasonga ugali. Kwahiyo nilivyomaliza tu huku nikahamia kwenye nguna.

Ugali mkuuubwa na samaki piga wote mzee hakijabaki kitu. Sasa hapo nikawa tayari na show, sindo nikamvamia.

Akanambia "Wee sitaki kesi, umetoka kula chakula chote hicho halafu unataka mzigo? Ukipata kichomi? Unifie hapa? Pumzika kwanza kiasi babaa"

Nikaona isiwe kesi mwana nikaenda kuoga nikaja kulala. Nilivyoamka mali hii hapa imejilaza kando yangu weeee nilipeleka moto. Nilimchezesha segere mpaka akasema kweli we unaishi Segerea.



Nikiikumbuka hii siku huwa nacheka sana aisee.

FUNZO: Msichana ukiona mpenzi wako hafanyi vizuri usikimbilie kumlaumu, msongee ugali ale. Ukiona siku hiyo mashine haisimami, kila ukijaribu hivi hakuna kitu USILAUMU, SONGA UGALI ALE.

UGALI ULIOKOA MAISHA YANGU, SIJUI NINGEWEKA WAPI SURA YANGU. Muda mwengine ni njaa tu zinatusumbua tunaamua kujikaza!

Vipi wewe mdau siku gani huwezi kusahau?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom