Ni tukio gani lilikutokea ukikumbuka unacheka?

Jahnson

Member
Oct 6, 2020
6
9
Wakuu salaamu! katika maisha Kuna matukio yanatutokea uenda yakawa ya kuogofya, kuchekesha au ya majonzi.

Ili tukio uwa nikikumbuka uwa nacheka lakini pia Kuna funzo ndani yake nilipata kupitia tukio hilo.
Kuna ndugu tulipoteana kwa miaka kadhaa, miaka 9 iliyopita nikapata mawasilino yake tukawa tunasawasiliana akaniambia anakaa kigamboni huko ndani ndani anajishughulisha na kilimo cha mboga mboga.

Wakati huo nimetoka kumaliza shule nipo mtaani nasikilizia mishe mjini Mambo bado magumu mtaani nikamwambia yule jamaa angu wiki ijayo nakuja kubadilisha mazingira kidogo na tuonane maana Ni miaka mingi hatujaonana, akanipa ramani Safi tu jinsi ya kufika kule. Kipindi kile kigamboni (sio pale ferry) nilikuwa naisikia tu sijawahi kufika kabla kwa iyo nilikuwa na matamanio kujua ipoje hiyo kigamboni.

Siku ikafika aisee unafika kibada unachukua bodaboda unaingia ndani kabisa Kuna kitongoji kinaitwa mwera unaingia ndan Zaidi aisee ni Kijiji kabisa hakuna umeme.nyumba zipo mbali mbali mashamba tu nikamuliiza mwenyeji nipo dar kweli! Uzuri wake upepo wa bahari Safi yaan hewa Safi kabisa.

Mkasa Sasa baada ya kukaa kama wiki 2 hivi nikamwambia mwenyeji wangu kesho mchana narudi mjini akasema mbona mapema nikatoa sababu' zangu pale akasema sawa, kawaida Kila asubuhi tunaenda shambani kwake kuvuna mboga mboga kuwauzia wachuuzi siku iyo akasema we tangulia.Hali ya hewa ilikuwa baridi na ukungu siku iyo katika ile njia Kuna miti ya miembe na mikorosho mingi tu nikiwa na vifaa vya kumwagilia maji na vingine huku baridi na ukungu angani Ni majira ya 12 kasoro asubuhi.

Kama nilivyosema ile njia ina miti ya mikorosho na maembe Sasa bwana ile pita pita nakuta embe limedodondoka katikati ya njia kushoto kwangu Kuna mti wa mwembe nikajua ili limedondoka kutoka mti mti huu ( ulikuwa msimu wa maembe) nikaliokota nikatia mfukoni Safari ikaendelea hatua 5 mbele nasikia kelele mwizi! Mwizi! Mwizi! Mume wangu mwizi wa maembe njoo huyu huku.. kutazama kushoto Kuna vichaka vichaka naona mtu kavaaa juba nyeusi kafunika kichwa kwa kitambaa cheusi nilishituka kwa mshang'ao kwa ule ukungu na mavazi yake meusi niliona Kama mzimu Kama sekunde 13 ndo akili inakaa sawa alikuwa mwanamke akija kwa Shari kubwa ..we ndo mwizi wetu unatuibia maembe Kila siku! nikajua hili tatizo .

Nikamwambia nimeliokota hapa njiani nilikuwa napita tu unaweza lichukua yule mama alikakataa katakata kulichukua uku akiendelea kumwita mumewe ...akawa anielewi nikasema njoja aje mumewe uenda akanielewa wote si wanaume tutazungumza, punde mumewe huyu hapa alikuwa anakuja mbio na fimbo mkononi..huku akisema yupo wapi yupo wapi. Jamaa kafika nikamwelezea Hali ilivyokuwa naye akagoma wewe ndo unatuibia Kila siku maembe Kwanza hatukujui we Ni mgeni nikajibu ndio nakaa nyumba ile nilikuwa napita tu kwenda shamba nikaona embe njian hapa na sio nimelitoa mtini sio shida nawapeni...wakagoma kata kata wanataka kunipeleka kwa mwenyekiti ishu ikawa ngumu nikasema twenden labda huko mwenyekiti ataelewa hoja yangu Safari ya shamba ikaishia hapo nikiwa na vifaa vyangu pamoja na walalamikaji wangu Safari ya kwenda kwa mwenyekiti ikaanza nikiwa na ushaidi wa embe mkononi.

Kufika kwa mwenyekiti kalala ikabidi wamuamshe walalalamikaji wakatoa malalamiko yao mwenyekiti hanijui pia nikasema mm mgeni mwenyeji wangu Ni fulani nilikuwa naenda shamba Kama unavyoniona na vifaa ivi katika kutembea njiani nikakuta embe ili limedondoka njiani kabisa nikaliokota ndo mwisho imekuwa Kama ivi. Mwenyekiti akatoa wito wa kuitwa mwenyeji wangu kufika akaulizwa ulimwambia mgeni wako utaratibu wetu hapa namna ulivyo akasema hapana . utaratibu pale kulikuwepo na tabia ya wizi wa maembe naama Kuna wachuuzi wanatoka mjini kuja kuyanunua so ni biashara waliwekeana Sheria hata ukikuta embe njiani lisilokuwa lako lipite tu kinyume chake fidia embe 1 elfu 30 wakataka kunipiga faini ya elfu 30 nikagoma wakasema tunakupeleka polisi station kibada.katika mvutano hule akatokea mzee flani ivi akasikilza ile kesi akawambia msameheni kijana walakini Ni mgeni na hakujua taratibu. Jamaa kasema sawa ila mke akakataa hapana alipe fidia ( huyu mama Ni mwenyeji wa dar es salaam mumewe Ni mtu wa kanda ya ziwa ) Aya niliyajua kupitia rafudhi yake na namna anavyoongea na kupitia mwenyeji wangu baada sekeseke ilo.
Basi yule mzee akaweka nasaa zake pale yule mama akakubali kishingo upande akachukua na lile embe lao kesi ikaisha.

Nilichojifunza katika ilo unapoenda ugenini zitambue taratibu zao / misingi yao waliyojiwekea usilete mazoea itakugharimu Kila sehemu Wana utaratibu wao Kuna sehemu hiki kinaruhusiwa ukienda kule kile ni marufuku nakumbuka miaka kadhaa kabla nilifika mikese ndani ndani kidogo Kuna jamaa yangu pia kajichimbia huko kule aisee maembe Aya Aya unalazimishwa kuangua toka mtini yaan unapita ktk nyumba ya mtu miti ile pale chukua Tani yako Ni free kabisa.muhimu tusiishi kwa mazoea Kila eneo lina Sheria/ taratibu zake Ni muhimu uzijue ili isikugharimu.
 
Tukio lako refu sijasoma hata... hahaaha

Sawa, mimi tukio ninalocheka mpaka leo ni siku jamaa yangu anasema mjomba usinipige ni kweli nataka kutibukwa (alikuwa na tatizo la kuanguka kifafa sasa kafanya kosa mjomba anataka kumchapa wamama zake wakawa wanamtetea kwa kusema huenda anataka kutimkiwa na kifafa kwahiyo kaka yao huyo asimchape dogo)

NB: kutimkiwa (hasa homa kama kifafa kichaa au maradhi mengine makuu yanayojitokeza na kutoweka) kikwetu tunasema kutibukwa
 
Back
Top Bottom