Ni tukio gani baya liliwahi kukutokea?

Ni tukio gani baya liliwahi kukutokea?

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,669
Reaction score
12,044
Kama kichwa kinavojieleza.

Ni tukio gani baya liliwahi kukutokea na kukuwekea historia mashani na kusema kamwe hutalisahau? Tukianza na mimi, sitasahau siku nilipokimbizwa na Tembo.

Ilikuwa ni katika eneo la bonde la mto Wami karibu na hifadhi ya taifa ya Saadan.Tulikwenda kutembelea eneo lile nikiwa na wenzangu lengo likiwa kujua mazingira ya bonde lile kama litatufaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Dooh!
Sasa si unajua tena hizi hifadhi zetu udhibiti wa wanyama pori ni mdogo sana. Basi wakati tupo pale kumbe kulikuwa na kundi la Tembo lilivuka kutoka hifadhini sisi hatukujua.

Lab!
Tembo wale sijui wanavichaa, mana walipotuona tu balaa likaanza.Kwa kweli sikunbuki kama niliwahi kutimua mbio katika maisha yangu yote kama siku ile.Mwenzetu mmoja alijipasua na visiki aliumia vibaya sana.Tangu siku ile sikurudi tena kule na sitaki kusikia hata na kilimo chenyewe eneo lile si salama kabisa.

Wewe je ni lipi lilikutokea.

Nawasilisha.
 
Tulipo vamiwa na majambazi na kuvuliwa nguo ilikua safari ya kutoka bukoba to kigoma
 
Back
Top Bottom