Ajira chache, wasomi ni wengi, kwahiyo lazima waweke masharti ili wachuje watu kidogo, ni sawa sawa na bodi ya mikopo kusema wenye dvsn 1 na 2 ndo wanapewa loan bt haimaanishi wnye dvsn 3 wamefeli. zaman mtu alikua anaajiriwa akiwa form 4 direct kazini, wnye form 6 moja kwa moja u assistant manager. sasa itafika kpnd itakua kigezo sio gpa tena ila wnye masters, kwahyo unaweza ukawa na gpa ya 4.5 lkn ukawa hauna soko.
Ila waajiri wanashindea kufahamu kitu kimoja, kuna watu wana gpa mbovu sn lkn wanajua kazi, hlf ni wachapa kazi, unaweza kuajiri mtu ana gpa kubwa lkn muozo tu kazini anasua sua hana analolijua.
Quality ya employee sio kujua kazi tu bali sababu ni nyingi sn, kuna nidhamu, usafi, jinsi ya kuongea na customers, jinsi ya kuingiliana na watu, uwezo wako wa kufanya maamuzi na hv ndo vitu vya msingi sn kazini, na ndo maana kampuni za wazungu interview zao ni kukupima uwezo wako wa kuliendea jambo ma sio ulifaulu vipi darasani.
Ushauri wangu kwa freshers, hakikisha ukitoka chuo unajua mambo hasa microsoft office excel, word na outlook. kwa fani zote hii kitu ni muhimu sna. na pia jenga fikra zako kwenye kufaulu tu na kusonga mbele, ondoa mawazo ya gpa na mawazo ya kufeli, ukiwa mzuri unachokijua na ulichosome basi hutalala njaa, madili mtaani mengi, huku unatafauta ajira unasonga mdogo mdogo.